Ninaungana mkono na wewe 100%. Ukitembelea miji mikubwa duniani miundo mbinu yao ilipangwa na kujengwa miaka takribani 100 iliyopita. Hii ni kwasababu viongozi wao wanauchungu na nchi yao, wanauzalendo, na wanafanya kazi kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.
Wengi wa viongozi wetu ni wabinafsi, wanajifikira wao na familia zao. Kiongozi anafikiria ajilimbizie mali itakayo msaidia yaye, wanae na wajukuu zake. Bila kufiria kuwa wale masikini waliowazunguka wanae na wajukuu wanaweza kuwapora hizo mali.
Mfano ukiangalia swala la elimu; tangia awamu ya pili watoto wa wanasiasa walituacha kabisa kule St Kayumba, walisoma English Medium kwasababu elimu ya St Kayumba si nzuri kwao lakini ni nzuri kwa wapiga kura. Sasa hivi tunalalamika kazi zote nzuri zinachukuliwa na Wakenya, wakati wenzetu waliwekeza St Kayumba zote zilikuwa English Medium.
Ukweli ambao wa Afrika hatuujui ni kuwa wazungu wamefikia hapo kimaendeleo baada ya kupambana kwa dhati na changamoto ambazo sisi tunazikimbia huku kwetu......lakini wao mpaka kesho wanapambana nazo....juzi hapa tumeshuhudia wananchi wa ufaransa wakiandama maelfu kwa maelfu wakiishinikiza serikali yao iwafanyie jambo fulani.....hawa ni wazalendo wanaojua thamani ya taifa lao hawazikimbii changamoto zao bali wanapambana nazo kwenye taifa lao......
Hakuna asiyejua kuwa nchi za kiafrika zina matatizo ya kiuongozi....watawala hawawajali watawaliwa..bali wanajijali wao....lakini hao viongozi hawajashushwa kutoka mawinguni bali tumewaweka sisi wenyewe madarakani kwa nia njema kabisa.......sasa kama tuliwaweka sisi wenyewe tunashindwaje kiwatoa kama wako nje ya matarajio yetu kiutendaji......uwezo wa kuwangoa tunao hata kama ikitughalimu damu zetu lakini wajukuu zetu wanatakiwa waikute kesho njema........
Hayo maisha bora huko ulaya tunakokimbilia chanzo chake ni rasilimali za huku barani afrika.....kuna makampuni kibao ya wazungu yanakwapua na kukwiba rasilimali zetu huku kwetu kwa mwamvuli wa uwezekezaji na kwenda kuneemesha kwao.......wakati sisi huku tupo tayari hata kuuza mali zetu ili tupate nauli ya kwenda utumwanai tena kwa nguvu zote....muda huo huo tunapishana na ndege zao killa uchao zikija kuangalia fursa katika ardhi zetu.......
Ndio maana mpaka leo haishangazi kukuta mzungu katoka kwao masikini lakini akishafika huku anakuwa tajiri wa kupindukia.......
Kitu ambacho wengi hawakijui ni kuwa maendeleo tunayoyaona huko ughaibuni na hali bora za maisha yanawezekana hata yakawa hapa kwetu......kama tu tutaaamua kutulia na kuzijenga nchi zetu na kukabiliana na changamoto zetu wenyewe.....maendeleo na maisha bora yana gharama zake na wakati mwingine vina gharimu uhai wa wachache kwa neema au manufaa ya walio wengi..........
Kila mtu anajua ni jinsi gani mzungu anavyomdharau mtu mweusi hata awe wa aina gani lakini ukitazama kati kati ya mstari ni kuwa mbaguzi wa kwanza ni mtu mweusi kwa kuwa yeye ubaguzi wake umepita kikomo kwani mpaka anajibagua yeye mwenyewe...na kujidharau kana kwamba yeye ni mnyama na sio binaadamu......ushahidi upo kwenye michango ya uzi huu jinsi gani wanavyoonyesha ufundi wa kuzitukana nchi zao bila ya hawa wala soni......nina hakika kama kuna mzungu anayefuatilia uzi huu lazima atakuwa anacheka kwa kejeli.....yaani anajisifia miundombinu na huduma bora za kijamii kwa nchi za wenzako...!!!??
Utu na thamani yako katika ulimwengu huu vinaanza na wewe mwenyewe.....wazungu wamefika hapo walipo kwa kuthamini vya kwao na kuviheshimu na kuvitunza kwa uzalendo wa hali ya juu sana.........
Maendeleo hayawezi kuja katika bara letu kwa kukimbilia kwenda kufanya kazi utumwani kwani kwenda kufanya kazi huko ni mnajenga uchumi na maisha ya huko utumwani.....haishangazi kuona kuwa kuna wazungu wanalipwa malipo ya kujikimu bila hata ya kufanya kazi kwa kuwa watumwa bado wapo na wanazalisha kodi kubwa kwa ujira mdogo sana........mpaka leo haishangazi kukuta nchi nyingi za ulaya kama sio zote wameweka kodi kubwa sana kwa wageni......lengo ni kuhakikisha hutoki na kitu nchini kwao huku jasho lako likijenga uchumi wao.......
Mahali pekee ambapo mwafrika anajisikia yupo nyumbani ni kwenye ardhi ya AFRIKA.......
HOME SWEET HOME.....