[emoji22][emoji17]Ukubwani huku my introvency naona ndo inazidi
Mimi ni maua, pets , kupika na social media
Naweza kumaliza likizo ya siku 28 nikiwa nimetoka nje mara 4 tu, nazo ni kanisani paap(napo nitatafuta kona nitakayokaa mostly mwenyewe.
Sipendi kwenda harusini wala kwenye watu wengi popote.
Nikifika vituoni, sokoni kuna namna nasikia kubanwa pumzi.
The only place ninajiona niko happy, full and peace ni nyumbani kwangu.
Inanipa peace ya kutizama mimea yangu, wanyama ninaofuga, nachora sometimes, nafuma occasionally yani kwa ujumla mimi najiona kabisa Ulimwengu unajikamilisha ndani ya nyumba.
Kipindi cha working from home was my best working moment.
Watu tuongee ila muwe huko huko mliko like this, sending email, kuchat(sipendi pia simu , iwe kupiga na kupigiwa)
Sipendi video calls(kama wewe sio mwenzi wangu usinipigie video call, sitaki kukuona sitaki unione while talking, just send a text nitakujibu, maana sipendi hata mlio wa simu. Hata yeye anajua sipendi video calls, na simu ni vile tu ndiyo mawasiliano.
Ninaweza kuwasiliana kwa maandishi zaidi(nina uwezo wa kuchat hata na watu 10 kwa muda mmoja na hakuna atakayefeel siko makini nae!)
Weird i know, but with my age sijioni nikibadilika.
Sina opportunity yoyote ninakosa, links zangu zinajikamilisha kunifanya niishi , as sina tu ndoto ya utajiri, ninataka tu kumudu maisha yangu binafsi na ya familia, which nimeweza hizo zingine sioni ni my cup if tea.
HAKUNA SIRI TENA!!Unaweza kushinda ndani kama jini nani sijui!, Halafu ukitoka nje dakika mbili tu unatamani tena kurudi ndani.. mbaya mbovu introvert tunaujinga huu.
Naweza nikawa nataka kutoka na wewe umekaa sehemu nayotaka kupita naweza nikasubiri mpaka utoke ndo namimi nipite!, mitabia myengine sijui ya wapi tu!..
Huku mitandaoni tumejazana maana ndo sehemu tunaweza hata kumtishia mtu kumdunda!, ila huku ana kwa ana hata kutukana tu ni kasheshe!.
Ndo viumbe pekee vinakaa mji fulani ila vinajua mitaa michache sana maana kutembeatembea sio pendeleo sana kwao!.
Mzazi mwenye mtoto wa aina hii usimsokote sana mwanao kumlazimisha achanganyikane na watu!, wakati wake ukifika atachanganyika na atachagua wakuchanganyika nao!.
Pili mfatilie ila usimfatilie sana mpaka ukaziba uhuru wake ambao ni amani yake!, utamkosesha kujiamini hata akiwa peke yako atakuwa anaona kama unamuangalia 24/7.
Usiruhusu mtu mwengine ambae hazijui hulka za mwanao amsumbue hovyohovyo bila sababu za msingi.
Jua vitu anavyovipenda ukiweza mpatie kadri uwezavyo kwa vipimo vya wastani, usimzidishie.
Introvert wengi wana hulka ya uoga na akikuwa hiyo hulka ikakomaa ndo inamvaa na kumsababishia "anxiety".
Hivyo hakikisha akiwa bado mdogo mpe kazi ambazo zitaongeza ujasiri wake, sanasana hakikisha anakuwa anafanya zile kazi ngumu kiasi na pia uwe unampa maneno ya kumtia moyo ya kwamba anaweza!. jitahidi kumsoma hali zake maana ni mabingwa wa kuficha!, hivi ndo viumbe vinaweza kutunza siri mpaka kufa!.
Mwisho kuwa makini na namna unavyoenenda nae maana anaweza akawa anakushinda hata utafakari!, usimtake ajielezee sana bali kama ni kitu cha kufanya muache afanye!, maana huwa si wazuri sana kwenye kujieleza ila kutenda wapo smart sana!.
The Mongolian SavageSijasoma uzi nasubiri nifturu kwanza.
Mufti kuku The InfinitySijasoma uzi nasubiri nifturu kwanza.
introvert huko majuu wengi wao ni huckers na data analyticsKijana wangu ni introvert, nilipata kazi sana kumuelewa huko nyuma, nimekuja kuelewa kua ni intovert akiwa secondary school, yani ulivuoongea vyote kuhusu intovert ni kama unamjua mwanangu, yani umemsema yeye kila kitu, hadi nikahisi au ana tatizo anaficha. Now hua namuacha tu na mambo yake japo sometimes anakera sana, mtoto gani anapenda kua peke ake mala nyingi, busy na cm au computer au chumbani kwake anaangalia tv, but is not good kiukweli, hata akiwa na tatizo huezi jua
MIN-me na @raraareree, unaweza ukadhani ni comments unatakiwa kuzijibu, kumbe ni likes, huwa nakasirika sana.Kuna ambao wana-like kila bandiko hapa JF, ninadhani hao nao ni miongoni mwao.,,,kazi kweli kweli.
Yaani, ilichukuwa muda mrefu wakwe zangu kunielewa. Nashukuru sijawahi kuwa fake au kulazimisha uchangamfu, wanaona poa tu na imenisaidia kuepuka lawama. Kusema kweli michanganyiko ya watu ipo very draining. Unahitaji muda mreeeeefu kukusanya nguvu tena kufanya shughuli inayohusisha kuchanganyika na watuNa kuna wengine wanakuogopa mpk akiwa anajambo anataka kulifikisha kwako anajiuliza aanzie wapi...🤣
HayaMimi ni extrovert ila mipaka nimewekea watu, baadhi hufikiri am an introvert.
Sitaki mazoea saaaana
mulemule...Sisi ndo wale tunahairisha appointments, Bora tulale nyumbani.
Sisi ndo wale tunabore ile mbaya tukikutana physical kama hatujakuzoea
Sisi ndo wale long distance relationship zetu zinalast kuliko kuishi wawili pamoja.
Sisi ndo wale mimea na wanyama inatuelewa zaidi kuliko binadamu
Sisi ndo gallery zetu zimejaa picha za mawe, milima, miti, wadudu, majengo, vyakula.
Sisi ndonwale tunajua mashairi ya nyimbo zote.
Sisi ndo wale tunasoma vitabu vingi kwa walati mmoja.
Sisi ndo wale tunaweza sana kazi za kibunifu na za mifumo.
KENZY ongeza na hizi
inawezekana!Kwahiyo JF wote ni introvert, maana mmetaja tabia zangu zote.