Kuvuja kwa video ya vijana wanaotuhumiwa kujihusisha na uchawi ni kinyume na sheria

Nkaburu

JF-Expert Member
Mar 23, 2023
660
784
Watanzania wenzangu poleni na mihangaiko na Shughuli zenu.

Jana katika peruzi zangu nilikutana na Thread ya Mjanja M1 ikionyesha Video ya watoto/vijana wadogo wakihojiwa na Polisi. Nilishangaa, na nikahuzunika, awali ya yote issue hiyo ikaibua maswali. Sasa najua hapa ni kwa wabobezi wa masuala mengi na nimeona isiwe tabu wacha niwaulize na labda mamlaka husika zikachukua hatua stahiki.

Mtazamo wangu ni huu:

Uvujaji wa ushahidi wa video ya kuhojiwa sio wa kimaadili na unadhuru, kwani unakiuka faragha na utu wa washukiwa, na kudhoofisha haki na uhalali wa uchunguzi na kesi

Swali:
Je, unadhani ni nani anayepaswa kuwajibishwa na kuwajibika kwa kuvuja kwa ushahidi wa video ya Interrogation? Maafisa wa polisi waliorekodi au waliofichua video hiyo au watu wengine, who obtained or published the Video au Umma uliotozama au kushea video hiyo?


Wewe una mtazamo na maoni gani?

Pia soma: Video: Vijana wakamatwa kwa uchawi | JamiiForums
 
Wanaohusudu na kusifia uchawi ni kundi la wapumbavu na uchawi wao haujawahi wasaidia kitu
 
Sioni kosa hapo sababau wengi wetu hatuamini na still tunaichukulia km mchezo wa maigizo.
 
Back
Top Bottom