Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

yaani takukuru ina uchafu? hii haingii akilini. Haiwezekani taasisi nyeti kama hii iwe na matatizo ya kupaswa kuchunguzwa. Masilingi hana hoja kwenye hili. Haiwezekani kila taasisi inayotuhumiwa jambo baya basi ianze kujichunguza! Mbuna hajashauri Ikulu ijichunguze? Mbona watu wamesema kuhusu wabunge kugongana na hawajataka wachunguzwe!
 

Takukuru, Ikulu na taasisi yoyote ile ya umma aliye mbele hajulikani. Wananchi tumepoteza imani na vyombo hivi maana ni uwongo tu kila kukicha bila woga wala aibu. Halafu wenyewe pamoja na kuwa wanafahamu kwamba Watanzania hatukubali uwongo wao bado tu wanasema uwongo. Hakuna hata mkubwa mwenye busara akawaambia jamani eh! Watanzania hawakubaliani na hadithi tunazowapa tubadilishe mwelekeo au tubadilishe hadithi yetu!!! Hii ni siri ya serikali, ile ni siri ya serikali, siri siri siri....🙁. Serikali imewekwa madarakani na Watanzania sasa mnafanya siri dhidi ya wale tuliowaweka madarakani!? Mkjj kwa maoni yangu hakuna cha kuchunguza ni kufukuza kazi wote tu maana kazi tuliyowapa imewashinda.
 
Basil Msongo, Dodoma
Daily News; Tuesday,July 01, 2008 @00:04

MBUNGE wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi (CCM), ametaka ufanyike uchunguzi kuhusu kauli za Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kuwa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hawaelewani, na kwamba fomu za mali za viongozi zilizopo kwa Spika wa Bunge zinatofautiana na zilizopo katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Amesema ikithibitika ni uongo, Mbunge huyo aombe radhi. Masilingi alisema kauli ya Kabwe kuhusu Takukuru lazima itolewe maelezo na akahoji Kabwe amefahamu vipi kuwa kuna mgawanyiko mkubwa na mgongano baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati hafanyi kazi huko.

Masilingi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema anaamini Kabwe ana uhakika na aliyoyasema na kwa kuwa hafanyi kazi Takukuru lazima wafanyakazi wa taasisi hiyo wamemueleza hayo. Alisema lazima pia uchunguzi ufanywe kufahamu Kabwe amefahamu vipi kuwa kuna fomu za mali za viongozi wa umma zilizopo katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambazo zinachezewa na ni tofauti na zilizopo katika Ofisi ya Spika wa Bunge.


Masilingi lazima ujue kwamba watu wanauchungu sana na jinsi mnavyogawana hiki kidogo tulichojaliwa na Mungu. Na ndiyo maana wameamua kuto information ili wasikilizwe kilio chao. Tena UKOME kabisa kutoa kauli za kutishatisha. Lengo ni nini wakati anasema hawa viongozi wa TAKUKURU hawaelewani je huna habari kwamba vijana wanaoonekana wanapenda haki wanahamishiwa mbali sana kama kuwaadhibu. TAKUKURU inafanya yale yale aliyokuwa anafanya IGP Mahita kila askari akitaka haki fulani adhabu yake Lindi au Mtwara kwani huko Lindi na Mtwara hakuna watu? Acheni kabisa kufanya haki kama kigezo cha kuwanyamazisha wanaharakati.
 
Last edited:
Mmhhh!!! TAKURURU???? hiyo si ndo imeoza kabisa.Nakumbuka pale Singida afisa mmoja wa takururu alimkamata polisi mmoja akipokea rushwa,lakini baada ya kupewa rushwa na polisi huyo kesi ikaisha.Yaani mimi huwa naugua kizunguzungu
 
Masilingi nae kaongea leo.. eeeeh mpigieni vigelegele na makofiiiiiii, kumbe na yeye yupo!!! Haya anaweza kukaa sasa kwenye yale makochi mazuri ya jengo letu jipya la bunge (japo na makochi haya yameshawangiwa, labda wafikirie kujenga jengo jipya na hayo ya sasa yatumike kuanzisha nursery school).
 
kama takukuru imeshindwa kutoa ufumbuzi wa hizi rushwa kubwa mapaka leo. wana matatizo.
Hakuna haja ya kusemwa bungeni.
ni wazi.
Hatujaona makundi ya watu kufutiwa kesi, au kupewa adhabu kwa rushwa kubwa.
Au wanasera ya usiri?
tunataka mtu akisafishwa tujue, na mtu akiadhibiwa tujue pia.
Kwani utu wa hao vibosile ni tofauti na wa hao mahakimu wanaoandukwa kwenye magazeti wakikamatwa na laki mojamoja?
 
Post Zionajirudia mno...

Mod kama inawezekana Merge hii Thread na Zitto azua Jambo Bungeni iliyoanzishwa na Bubu ataka kusema...

Tuweze jadili katika cmstari mmoja.

Heshima mbele.
 

Mkuu Mtata sana wewe...

Nadhani ujumbe umefika kwa Walengwa. Pamoja
 
Masilingi ndugu yangu, tangu ulipo temwa kwenye kabineti umejirundika kwenye migomba na rubisi huko Muleba hata hujui kinacho endelea TZ yetu?

Hivi kweli hujui TAKUKURU kuna mgawanyiko mkubwa? Jitahidi basi walau uwe unatembelea JF uwe update kidogo na kinacho endelea nchini kwako! vinginevyo wakati ukuta ndugu yangu utajikuta uko nje kabisaaaa ya dunia yetu Tanzania!
 
Mashilingi Hana Jipyaa, Jimbo Lake Linanyelelewa Na Tibaigana, Wote Ni Walevi Wa Rubisi. Anachozungumza Zito Ndicho Kilichoko Moyoni Mwa Watanznia Wote. Polisi Rushwaa, Takukuru Rushwaaa, Tume Ya Maadili Rushwaaa! Rais Rushwaaaa! Sijui Tuanze Na Nani? Labda Kanisa Na Misikiti Itusaidie Tena
 

Haya niliyategemea baada ya kusoma ile speech ya zitto. kazi imeanza tena, kijana mwenzetu anafanya wazee mafisadi kujiabisha hadharani. Nasubiria kuona game plan ya ccm kwenye hili.

Credibility ya Pinda imekwisha kabisa na sasa wanatafuta "mtoto wa mkulima" mwingine asafishe njia.

Kazi kweli kweli
 
Huyu Kilaza hivi ni Mashilingi au Vijisenti? yaani katika nondo zote zile alizopigilia Zito kuhusu Meremeta, huyu Kilaza alichoona ni muhimu kuzungumzia kwa gharama za walipa kodi ni mgongano kati ya wafanyakazi wa TAKUKURU na sio mapesa ya MEREMETA ambayo ndio msingi wa hoja ya Zitto. Kama huyu jamaa aliwahi kuwa waziri wa utawala bora enzi za Mkapa sasa ndio naanza kuelewa, ilikuwaje kashfa zote hizi za KIWILA, EPA, MEREMETA na matakataka mengine yaliweza kutokea bila ya serikali kushtuka.
 
Takukuru haina maana yoyote na ingebidi ni vema ikavunjwa. Mlarushwa na mafisadi wako serikalini ambayo ndi inamteuwa PCCB. sasa PCCB itamchunguza serikali. Itaanzia wapi?. PCCB haikuanzashwa kwa matakwa ya ananchi bali kwa shinikizo la nchi wahisani.
 
Masilingi huyu si yule mbunge wa Muleba?
Kwanza usafi wake yeye tu unatia shaka. Alikuwa waziri wa takukuru wakati wa BWM na anajua wazi kuwa haya ni malalamiko ya kweli kwani aliyaacha bila ya kuyashughulikia akitegemea atarudi kwenye cabinet. Bahati yake mbaya alisoma vibaya alama za nyakati kama wafanyavyo wana ccm wote. Akalalia kwa Sumaye akidhani atakuwa ndiye president na akakuta hesabu imetibuka.
Hata hivyo ni huyu huyu ambaye wakati wa uchaguzi inasemekana wakati wa kula (Kura)za maoni ya chama chake cha majizi alitembea usiku kucha akigawa pesa kwa wajumbe yeye mwenyewe! ili ateuliwe kugombea kupitia ccm kwani ajui tunamfahamu? Sijui yeye tumweke kundi gani Fisadi/Kafisadi?
 
...Masilingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii anataka kuturudisha mwaka 47 nini?? Kama Takukuru wanachemka hataki watu waseme!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…