Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Halafu huyu mtu ni kwamba anakula bure, anasafiri bure, anatibiwa bure, hospitali yeyote ile duniani, ana wapishi, madereva na magari, wabeba briefcase, shamba boi, house boi, ana mshahara kama wa Kikwete almost, nyumba ya bure anapewa I'm sure, wachunga ngo'mbe, wafua nguo za bure.

Lakini bado na mgodi wa wizi lazima awe nao...

Ukisoma management Abraham Maslow on hierarchy of needs classified needs in order of hierarchy. He started with lower level need ''Physiological needs i.e. food, shelter,etc, then Safety needs, ......., at last he ended with Self actualization need. This is the higher lever need that makes people behave the way they do. So pamoja na mambo yote tunayo mlipia jamaa bado hawezi kuachia mgodo inawezekana ndio unaokamilisha mahitaji yake (self actualization).

Kwaheshima yake angeurudisha tu huenda watanzania wangemsamehe
 
Halafu huyu mtu ni kwamba anakula bure, anasafiri bure, anatibiwa bure, hospitali yeyote ile duniani, ana wapishi, madereva na magari, wabeba briefcase, shamba boi, house boi, ana mshahara kama wa Kikwete almost, nyumba ya bure anapewa I'm sure, wachunga ngo'mbe, wafua nguo za ndani... bure.

UMESAHAU ANA MABIBI WA BURE
Mzee Ben tukiujua vema ukweli kuhusu lengo lake la kiuongozi katika nchii hii tungefunguka zaidi!!!!!!

Smear campaigns tuuu.....
 
Restuta James

Sakata la utekelezaji wa maazimio 21 ya Bunge kuhusu kampuni tata ya Richmond, uuzaji wa nyumba za serikali, ugawaji wa vitalu vya uwindaji na bei zake na taarifa ya uendeshaji wa Shirika la Reli nchini (TRL) ni mambo ambayo yatalitikisa taifa wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge utakaoanza Juni 6, mwaka huu.

Mengine yatakayotikisa ni taarifa ya kitengo cha makontena (TICTS), tamko la serikali kuhusu tume ya Rais iliyochunguza mikataba ya madini na hesabu za serikali kwa mwaka ulioisha.

Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge.

Alisema tayari serikali imeelezwa kuwasilisha utekelezaji wa mambo hayo kama ambavyo Bunge lilivyokuwa limeelekeza.

Hata hivyo, alisema mkutano huo wa Bunge utapokea taarifa ya shirika la Maendeleo ya petroli (TPDC), Shirika la simu (TTCL) na kuchambua taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2009/10, Dk. Kashalilah, alisema itasomwa siku ya Alhamisi ya Juni 11, saa 10:00 jioni.

Alisema kabla ya kusomwa kwa bajeti hiyo, asubuhi ya Juni 11, Waziri wa Fedha na Uchumi atawasilisha taarifa ya hali ya uchumi nchini na baadae jioni ndipo atawasilisha bajeti.

Hata hivyo, alisema tarehe hiyo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitawasilisha makadirio ya bajeti zake.

Mambo hayo yanaelezwa kulitikisa taifa kutokana na kwamba utekelezaji wa maagizo ya Bunge umekuwa ukitekelezwa kwa kasi isiyoridhisha na hivyo kuifanya serikali ibanwe kila mkutano wa Bunge jambo ambalo hata spika wa Bunge, Samuel Sitta alilionya alipokuwa akihitimisha mkutano wa Bunge uliopita.

Sakata la uuzaji wa nyumba za serikali limekuwa likielezwa kwamba lilitawaliwa na rushwa jambo ambalo Waziri wa Miundombinu, Ezekiel Chibulunje, alikiri alipokuwa akijibu swali katika mkutano wa Bunge uliopita.

Kuhusu Ticts, hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwishakiri kwamba kitengo hicho kinamkera na ni mzigo kwa taifa kwa sababu kimeshindwa kuleta ufanisi na kuahidi kuwa serikali ingechukua hatua.

Pinda alikiri kukerwa na Ticts katika mkutano wa Bunge uliopita alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Siraju Kaboyonga, katika utaratibu wa maswali ya papo kwa popo Bungeni.

NIPASHE JUMAPILI
 
Kama Bunge lingeweza kutumia meno ambayo linayo, na siyo ushabiki wa kisiasa tungetegemea serikali kujiandaa kujibu hizo kikamilifu. Kwa kuwa Bunge letu limejaa unafiki, na ushabiki wa kisiasa hatutegemei kwa serikali kujihangaisha. Kwa hiyo hoja ya Taifa kutikisika sidhani kama itatokea, usanii tu, na wabunge wanaupigia makofi na meza. Kukiwa na hoja ya maana kwa maslahi ya taifa, na inaibana serikali wataitisha kura, ambapo wapinzani ni wachache kuweza kubadili mwelekeo. Tutaweza kuwatikisa hawa watu kwa kuwavote out wote ifikapo 2010, na hilo lipo ndani ya uwezo wetu, hapo ndipo tuna uhakika wa kuwatikisa, hivyo vingine ni viini macho tu.
 
Kama Bunge lingeweza kutumia meno ambayo linayo, na siyo ushabiki wa kisiasa tungetegemea serikali kujiandaa kujibu hizo kikamilifu. Kwa kuwa Bunge letu limejaa unafiki, na ushabiki wa kisiasa hatutegemei kwa serikali kujihangaisha. Kwa hiyo hoja ya Taifa kutikisika sidhani kama itatokea, usanii tu, na wabunge wanaupigia makofi na meza. Kukiwa na hoja ya maana kwa maslahi ya taifa, na inaibana serikali wataitisha kura, ambapo wapinzani ni wachache kuweza kubadili mwelekeo. Tutaweza kuwatikisa hawa watu kwa kuwavote out wote ifikapo 2010, na hilo lipo ndani ya uwezo wetu, hapo ndipo tuna uhakika wa kuwatikisa, hivyo vingine ni viini macho tu.

...Na kwa kawaida haya ni maneno ya magazeti tu ya kuuzia magazeti yao. wanaandika vitu ambavyo hata wao wenyewe wanajua kuwa haviwezi kutokea katika bunge hili. Wanaleta tu msisimko usiokuwepo. Kwani mwezi wa nne si magazeti hayo hayo ndio yaliandika 'Bungeni kuwaka Moto'! kuhusu hoja hizo hizo? Kuna moto wowote uliwaka???
 
Nimekuwa nikisikia nyimbo za aina hiyo kila zinapobaki siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge.Nahisi ni mbinu inayotumika ku-justify hayo mamilioni wanalipwa for nothing....na kama kawaida ya magazeti yetu yanakimbilia kuandika kwa herufikubwa "BUNGE KUWAKA MOTO KIKAO KIJACHO".qUESTION IS,WHY NOT DURING KIKAO KILICHOPITA?
 
Bunge letu linaanza vikao vyake leo asubuhi. Naomba wadau tupeana habari na kujadili hoja mbali mbali zitakazo tolea.
 
Bunge budget meeting opens today

Polycarp Machira

The 16th meeting of the National Assembly and budget session for 2009/10 starts here this morning, and is scheduled to end on July 31.

Parliament Principal Information Officer Ernest Zulu said yesterday The Executive Agencies (Amendment) Bill, 2009) would be read for the first time.

He said President Jakaya Kikwete would also speak to elders and MPs later in the day.

Zulu said the budget would be tabled on Thursday afternoon and shortly thereafter, Parliament would be adjourned.

Unlike the norm where legislators broke off until Monday, this time round the house would resume business on Friday and start the budget debate on Monday, he said.

“Members of Parliament will start debate on the budget speech from next Monday to next Wednesday,” said Zulu.

Zulu said estimates for various ministries, starting with the Prime Minister’s Office would be debated during the second week of the House's longest session, just after the main budget had been endorsed.

The government would issue treasury notes on reports of the permanent parliamentary committees, including Public Accounts Committee (PAC), Local Authorities Accounts Committee (LAAC) and the Public Organisations Committee (POC) in the third week of the session, he said.

The House would select a representative to Southern Africa Development Community-Parliamentary Forum (SADC-PF) on July 31 before its adjournment.

Zulu said that following an agreement by East African Community parliaments, Tanzania’s budget would be read simultaneously with presentation of the Kenyan and Ugandan annual financial estimates.

“The budget will be read simultaneously with those of other East African countries of Uganda and Kenya, and also probably of Rwanda and Burundi,” he said.

The government plans to use 9.51tn/- (USD7.3bn) in the coming fiscal year budget, about 32 per cent up from last year’s.

Only 29 per cent of the budget will be devoted to development, a 4 per cent cut from last year’s allotment.
In 2008/09, the government budget was 7.2tn/-, with 2.4tn/-, or 33per cent, allocated for development expenditure, mainly in infrastructural projects, poverty reduction and human resource development investment.

Even with this year’s massive 9.51tn/- budget, only 2.2tn/- has been alloted for development expenditure, marking a decrease not only in the portion of the budget that the sector takes up, but also in the actual value of that portion.

As the government cuts down on development expenditure, it has noticeably upped its recurrent expenditure, by 1.99tn/- to 6.69tn/- or 42 per cent of the budget.

THE GUARDIAN
 
HABARI kubwa leo ni jakaya alikuwa ahutubue bunge ..laakini last touches wamesema kuwa atahutubia wabunge kupitia wazee wa mkoa wa dodoma...hii ina maana kuwa hotuba yake haitaweza kujadiliwa rasmi na wabunge kwa kuwa haijatolewa bungeni...

watu wanajiuliza kisa cha kikwete kukimbia wabunge .....na zaidi inahusishwa na kebehi alizopewa na spika wa bunge mara ya mwisho alipohutubia ...hatua iliyopelekea ikulu kususa kupeleka copies za hotuba ya rais kama fomalities zinavyotaka ili waijadili....ile ilikuwa hotuba pekee kutolewa na rais bungeni na isijadiliwe[tangu tupate uhuru]...
 
HABARI kubwa leo ni jakaya alikuwa ahutubue bunge ..laakini last touches wamesema kuwa atahutubia wabunge kupitia wazee wa mkoa wa dodoma...hii ina maana kuwa hotuba yake haitaweza kujadiliwa rasmi na wabunge kwa kuwa haijatolewa bungeni...

watu wanajiuliza kisa cha kikwete kukimbia wabunge .....na zaidi inahusishwa na kebehi alizopewa na spika wa bunge mara ya mwisho alipohutubia ...hatua iliyopelekea ikulu kususa kupeleka copies za hotuba ya rais kama fomalities zinavyotaka ili waijadili....ile ilikuwa hotuba pekee kutolewa na rais bungeni na isijadiliwe[tangu tupate uhuru]...
Kwa hiyo taasisi hii (Ikulu) haitaki kuambiwa ukweli ila kusifiwa tuu. Jee tutafika?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete leo hii anatarajia kuongea na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania katika eneo la kilimani mjini Dodoma, Je tutarajie nini kutoka kwenye hotuba hiyo?

Kilimo
Hali ya uchumi wa dunia, stimulus package kutoka serikalini
Mauaji ya albino
Ziara yake ya Marekani kumtembelea President Obama
Ufisadi papa
Au kutakuwa na jingine jipya?..

Ni nini ungependa kiwekwe kwenye hotuba yake hiyo ya leo.?

MJ
 
Nadhani leo atazungumzia mambo yafuatayo;

1. Mtikisiko wa uchumi duniani: Effect zake kusababisha kushindwa kutekelezwa kwa mipango mingi ya serikali
2. Maelezo ya kina kuhusiana na Bajeti ya 2009/2010. Sababu zilizopelekea kufikia bajeti hiyo (sijui kama ana maelezo ya kuridhisha)
3. Mwelekeo wa uchumi wa Tanzania - 2009/2010
4. Hali ya kisiasa nchini

Sidhani kuwa atazungumzia mambo mengi ambayo ni muhimu kama;
1. Ufisadi unaoikumba nchi kwa sasa na jinsi serikali yake inavyoishughulikia
2. Mbinu mbadala za kufufua uchumi ambazo zinaendana na hali ya uchumi duniani na pato la Taifa
3. Hali ya ulinzi na usalama wa Taifa
4. Ukiukwaji wa sheria unaofanywa na wananchi na hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa
5. Utekelezwaji wa ahadi zake na ilani ya chama chake
 
Hata kama ataongelea hayo mliyotaja hapo juu atayaongelea kisiasa na kutakuwa hakuna jipya kwenye utekelezaji. Bla blah tu
 
Walio karibu na TBC watupatie michemsho ya ulimi na ndizi.
 
Back
Top Bottom