Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Naona hapa ndio watajulikana akina nani wanatetea mafisadi na nani anatetea wananchi!! Bravo Kimaro.
 
Hongera Kimaro na nategemea uazidi kuwapa mwamko wale wabunge wengine ambao wako hivi hivi tu....Wale wasio na msimamo na wale wabebao mafisadi bila haya.....Kina Mzindakaya.

Nashangazwa na kina Mzinda kuja katika bunge letu tukufu na kuwasafisha mafisadi.....hawana hata haya wamefanya bunge letu break point?
 
Last edited:
mstari unazidi kuchorwa ardhini.. wenye kuvuka wanavuka, na mchanga umeshikwa kiganjani mwenye kuputa apute... lakini kuanzia wiki ijayo kitaanza kueleweka. Mmehabarishwa.
 
Mimi bado sijaona cheche zozote kwenye kauli za Kimaro.
Alichosema hakina tofauti na alichosema Mama Killango na Anna Abdallah...Kwamba pesa zirudishwe na pia kuna wanaopinga ufisadi ila kwa upole!

Hata hivyo ni siasa tu!

Kwani at the same time ameongea maneno ya Anna Abdala kwamba kuna wabunge wasiozungumza kwa ukali ila na wao wanapinga ufisadi!

Kwa maana hiyo ujumbe wake ni wa kuwaunganisha ccm esp baada ya Killango na Anna Abdallah kulumbana...Mmoja akisema pesa zirudishwe kama alivyosema Kimaro...Na mwingine akisema kuna wale wanaojidai wanauchungu kwa kuzungumza kwa ukali kama alivyosema Anna Abdallah na Kimaro kusema the same!

Kwa kifupi Kimaro ni Kilabdallah!
Kwamba yeye ni nusu killango na nusu Anna Abdalla!
Politics and more politics!
Ushahidi uko wazi...Atakayesema MAFISADI WAKAMATWE NDIYE WA KUUNGWA MKONO!
Ni ushauri tu.
 
A journey of a million miles starts with a single step!!
 
Ameonyesha kuwa kumbe anajiamini na anaweza kusema ukweli hata kama ataonekana mbaya.

Pili Mbunge wa Nkasi Poniano Nyami amesema kuwa ataleta hoja binafsi Bungeni kama serikali haitatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na SPM mgololo -kwa wale waliosoma hoja ya Dr.Slaa mtakumbuka hili la SPM.

lets wait another man is coming in front.........
MWAKA WA SHETANI,NANI ALAUMIWE?Hakika mungu wetu kaamua kutupigania watz
 
Mimi bado sijaona cheche zozote kwenye kauli za Kimaro.
Alichosema hakina tofauti na alichosema Mama Killango na Anna Abdallah...Kwamba pesa zirudishwe na pia kuna wanaopinga ufisadi ila kwa upole!

Hata hivyo ni siasa tu!

Kwani at the same time ameongea maneno ya Anna Abdala kwamba kuna wabunge wasiozungumza kwa ukali ila na wao wanapinga ufisadi!

Kwa maana hiyo ujumbe wake ni wa kuwaunganisha ccm esp baada ya Killango na Anna Abdallah kulumbana...Mmoja akisema pesa zirudishwe kama alivyosema Kimaro...Na mwingine akisema kuna wale wanaojidai wanauchungu kwa kuzungumza kwa ukali kama alivyosema Anna Abdallah na Kimaro kusema the same!

Kwa kifupi Kimaro ni Kilabdallah!
Kwamba yeye ni nusu killango na nusu Anna Abdalla!
Politics and more politics!
Ushahidi uko wazi...Atakayesema MAFISADI WAKAMATWE NDIYE WA KUUNGWA MKONO!
Ni ushauri tu.

Subira yavuta heri! Pamoja na kuwa CCM kuwa chama cha mafisadi bado kuna baadhi yao humo ni wazuri na kila wanapofanya juhudi za kutetea maslahi ya nchi ni lazima tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa. Kuwakatisha tamaa kutawafanya hata wale wanaotaka kuingia upande wakutetea maslahi ya nchi kufikiria mara mbili mbili kama siyo mara 10 10, maana watasema angalia fulani na fulani walizungumza hapa bungeni kutetea maslahi ya Watanzania lakini hawakupata support yoyote toka kwa wananchi bali Watanzania waliwazodoa tu!! Kuwa na subira!
 
mwaka huu bungeni kumoto

huenda sasa watu wakaanza kuogopa kugombea ubunge.

ilikuwa ishaanza kuhesabika ubunge ni kula tu sasa kazi ipo

...So much from Mtu wa pwani, whose moto was "tuachieni CCM ina wenyewe" nimeanza kuamini the worst is over
 
Subira yavuta heri! Pamoja na kuwa CCM kuwa chama cha mafisadi bado kuna baadhi yao humo ni wazuri na kila wanapofanya juhudi za kutetea maslahi ya nchi ni lazima tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa. Kuwakatisha tamaa kutawafanya hata wale wanaotaka kuingia upande wakutetea maslahi ya nchi kufikiria mara mbili mbili kama siyo mara 10 10, maana watasema angalia fulani na fulani walizungumza hapa bungeni kutetea maslahi ya Watanzania lakini hawakupata support yoyote toka kwa wananchi bali Watanzania waliwazodoa tu!! Kuwa na subira!

We the PEOPLE or "Yuo" to be specific...Said the same thing during Killango's statements!

And i told you guys to be sceptical!

TRUST BY VERIFY!

Niki verify statements zake sioni jipya!

Hata hivyo kama tulivyofanya kwa Killango..Then ni wazi tutafanya tena kwa Kimaro!

However...We should be aware that time is running out na bado fisadi hajaguswa!
 
Wakuu, heshima mbele.

Nimekua mfuatiliaji wa hii forum kwa muda mrefu kama observer, lakini hali ya taifa ilipo imenilazimu nianze kuchangia huu mjadala.

Huyu mheshimiwa inaonekana amekua mwiba... Binafsi leo nimeshuhudia matangazo LIVE ya bunge kupitia TBC1 yakikatishwa wakati alipokua anashusha makombora around saa moja na dakika kumi hivi jioni na badala yake yakawekwa matangazo. Ilianza kuzimwa camera wakati yeye anaongelea issue ya Tanzanite sorting, sauti ikabaki. Then wakakata na sauti yake.

After about fifteen minutes, matangazo ya bunge yakarudi tena LIVE TBC1. Wakati TBC1 haipo hewani, hata Star Tv nao hawakua wakionesha bungeni LIVE.

To me it was more than a coincidence. lakini nimeogopa kua judgemental on TBC1.

Wanaofaham zaidi wanaweza kutusaidia nini haswa kilitokea.
 
wakuu, Heshima Mbele.

Nimekua Mfuatiliaji Wa Hii Forum Kwa Muda Mrefu Kama Observer, Lakini Hali Ya Taifa Ilipo Imenilazimu Nianze Kuchangia Huu Mjadala.

Huyu Mheshimiwa Inaonekana Amekua Mwiba... Binafsi Leo Nimeshuhudia Matangazo Live Ya Bunge Kupitia Tbc1 Yakikatishwa Wakati Alipokua Anashusha Makombora Around Saa Moja Na Dakika Kumi Hivi Jioni Na Badala Yake Yakawekwa Matangazo. Ilianza Kuzimwa Camera Wakati Yeye Anaongelea Issue Ya Tanzanite Sorting, Sauti Ikabaki. Then Wakakata Na Sauti Yake.

After About Fifteen Minutes, Matangazo Ya Bunge Yakarudi Tena Live Tbc1. Wakati Tbc1 Haipo Hewani, Hata Star Tv Nao Hawakua Wakionesha Bungeni Live.

To Me It Was More Than A Coincidence. Lakini Nimeogopa Kua Judgemental On Tbc1.

Wanaofaham Zaidi Wanaweza Kutusaidia Nini Haswa Kilitokea.
mmh Sijui Ila Hawa Star Tv Huwa Mara Nyingi Hawaonyeshi Bunge Jioni.
 
Wana JF ambao mko nyumbani kama mkiweza mtuwekee vi-clip hapa hata za kurekodi na simu tupate angalau nafasi ya kuwaona hawa waheshimiwa na kupima wanayoyasema kama yana hisia ndani au debe tupu.
 
Kama kuna mtu ana video hizo awasiliane nami na tutasaidia jinsi ya kuziupload ili watu wengine waweze kuziona. Sijui ilikuwaje TV zetu zote tatu zilizokuwemo kwenye JumpTV zikaamua kuchomoa zote! Labda waliona tunafaidi sana.
 
Sasa Mkuu umenena, kama kesho kuna bunge au jumatatu nafikiri wakereketwa wenzetu watakutumia clips.
 
Kama kuna mtu ana video hizo awasiliane nami na tutasaidia jinsi ya kuziupload ili watu wengine waweze kuziona. Sijui ilikuwaje TV zetu zote tatu zilizokuwemo kwenye JumpTV zikaamua kuchomoa zote! Labda waliona tunafaidi sana.

Kulikuwa na matatizo ya umeme hapabungeni, wakati Kimaro anazungumza umeme ulikatika nadhani ikawaka jenereta ya dharura na ndio maana matangazo yakakata kwa muda, sidhani kama ilikuwa ni hujuma
 
We the PEOPLE or "Yuo" to be specific...Said the same thing during Killango's statements!

And i told you guys to be sceptical!

TRUST BY VERIFY!

Niki verify statements zake sioni jipya!

Hata hivyo kama tulivyofanya kwa Killango..Then ni wazi tutafanya tena kwa Kimaro!

However...We should be aware that time is running out na bado fisadi hajaguswa!

Mush,kama ungekuwepo Bungeni ukasikia na tone ya Kimaro, ninaamini ungekwua na mawazo tifauti kwa sababu alichokisema ukikisikia moja kwa moja kina tofauti sana na hiki tunachokiandika ili wenzetu mlio nje muelewe kinachoendelea.
Pia, ukioanisha maneno ya Kimaro jioni na yale yaliyosemwa na Mzindalaya asubuhi (ipo thread yake niliianzisha) utabaini kuwa there is something going on.
Pia juzi Naibu Spika alitamka ndani ya Bunge kuwa katika kipindi hiki kilichosalia hadi uchaguzi mkuu "MOTO UTAWAKA BUNGENI".
Nadhani kwa pamoja, kauli hizi na mambo mengine yanayotokea, yanaashiria kitu fulani kikubwa ingawa hakijafika katika level ambayo wewe unaitaka(ya Mkapa kuguswa moja kwa moja au kukamatwa). Lakini nikipima hali ya mambo hapa, nadhani ni suala lamuda tu, tutafika hukohuko unakokuzungumza wewe.
 
Hii ni bullshit ,mangapi tumeyasikia ya kutema cheche,bungeni hapatatosha,wengine hapatakalika na mijineno mikubwa mikubwa mwisho wake wale wanotoa cheche wote huingia mitini na haijulikani wamekwenda wapi,angalau ukiona kura moja imepinga utajua kuwa ni yeye ,lakini hakuna hata kimoja hatujasikia bajeti kupigwa na chini wala mtu kuweka shilingi ,hatujaona hatua kuchukuliwa ,wala wahusika kukamatwa ,sasa hizi tararira naona nazo mwisho wake zitakuwa kero kwa wananchi.
Hivi ni faida gani inapatikana kwa hawa watu kusema mpaka kutoa vumbi la mate na sasa wanafikia kutoa cheche na mwishoni utasikia wamegeuka yule mnyama wa kufikirika wa kichina aitwae Dragon ,inasemekana anatoa moto anapopandisha hasira ,ndio wabunge wetu wanakoelekea huko ,lakini matokeo yake yanabaki palepale ya kufikirika ,hakuna litakalosemwa likatolewa cheche tukaona cheche hizo zimewaunguza wahusika kikweli kweli kiasi cha kufikia Wananchi kusema sasa Bungeni sio cheche tena sasa kunawaka moto na wahusika wote wanaotajwa tajwa kuhusika na Ubadhirifu wameanza kuungua na nguo zao kushika moto na wale waliokuwa karibu na ufisadi nao wameanza kupata joto ,ndio hapo ndipo tunapotaka kuwafikisha wananchi waseme na kutoa kauli zinazoashiria kuwa bunge lao sasa lipo katika kujali maslahi ya Taifa ,hapo ndipo wabunge wenyewe watakapoweza kutembea kifua mbele kwenye mitaa ,hapo ndipo itakapoonekana kuwa mbunge ana nguvu ndani ya bunge.
Sio mbunge ajione ana nguvu ndani ya bunge ,tunahitaji mwananchi wa kawaida akiri kuwa mbunge ana nguvu ndani ya bunge au wabunge wana nguvu ndani ya bunge ,kwani mbunge ni mtumwa wa wananchi sasa ili mbunge ahishimike ni lazima mwananchi akubali kuwa mtumwa wake anafanya kazi aliyompa au aliyomtuma.
 
Mush,kama ungekuwepo Bungeni ukasikia na tone ya Kimaro, ninaamini ungekwua na mawazo tifauti kwa sababu alichokisema ukikisikia moja kwa moja kina tofauti sana na hiki tunachokiandika ili wenzetu mlio nje muelewe kinachoendelea.
Pia, ukioanisha maneno ya Kimaro jioni na yale yaliyosemwa na Mzindalaya asubuhi (ipo thread yake niliianzisha) utabaini kuwa there is something going on.
Pia juzi Naibu Spika alitamka ndani ya Bunge kuwa katika kipindi hiki kilichosalia hadi uchaguzi mkuu "MOTO UTAWAKA BUNGENI".
Nadhani kwa pamoja, kauli hizi na mambo mengine yanayotokea, yanaashiria kitu fulani kikubwa ingawa hakijafika katika level ambayo wewe unaitaka(ya Mkapa kuguswa moja kwa moja au kukamatwa). Lakini nikipima hali ya mambo hapa, nadhani ni suala lamuda tu, tutafika hukohuko unakokuzungumza wewe.

Ahsante sana MN, subira yavuta heri lazima tuwe na subira pamoja na kuwa tunayachukia yanayoendelea ndani ya nchi yetu, vinginevyo bila kuwa na subira basi tunaweza kuchinjana wenyewe kwa wenyewe..Mungu apishilie mbali.
 
Mush,kama ungekuwepo Bungeni ukasikia na tone ya Kimaro, ninaamini ungekwua na mawazo tifauti kwa sababu alichokisema ukikisikia moja kwa moja kina tofauti sana na hiki tunachokiandika ili wenzetu mlio nje muelewe kinachoendelea.
Pia, ukioanisha maneno ya Kimaro jioni na yale yaliyosemwa na Mzindalaya asubuhi (ipo thread yake niliianzisha) utabaini kuwa there is something going on.
Pia juzi Naibu Spika alitamka ndani ya Bunge kuwa katika kipindi hiki kilichosalia hadi uchaguzi mkuu "MOTO UTAWAKA BUNGENI".
Nadhani kwa pamoja, kauli hizi na mambo mengine yanayotokea, yanaashiria kitu fulani kikubwa ingawa hakijafika katika level ambayo wewe unaitaka(ya Mkapa kuguswa moja kwa moja au kukamatwa). Lakini nikipima hali ya mambo hapa, nadhani ni suala lamuda tu, tutafika hukohuko unakokuzungumza wewe.

ccm Walishakaa kikao chao wote na kina Mkapa na MAFISADI WOTE!
WAMEKUJA NA PACTS!
Niliwaambia waje na PLAN B kwani A Jmushi kaiua!
Hii inawezekana ni PLAN B YAO!
Ni makubaliano yao ya pamoja kuwa watajitahidi kukinusuru chama!
Ila hakitaweza kunusurika kama lugha bado ni zile zile!
Hawa wabunge wamerogwa ama?
Ripoti zote za ukaguzi zinakubalika kisheria mahakamani!
Ni ushahidi usiohitaji mbwembwe za maneno wala kamati!
Kama ni kweli hawa watu wana nia nzuri...Then based on USHAHIDI WOTE HAWA MAFISADI WANGESHAKUWA JELA TAYARI.
 
Akumbushia ahadi za mwana TANU.
Asema kuwa rushwa ni adui wa haki, asema kuwa ahadi zile ni muhimu na kila mbunge ameapa kuzilinda .

Asema wabunge wawe mstari wa mbele kupiga vita Ufisadi.

asema kuwa watanzania hawakuamini kuwa pesa za EPA ziliibiwa mpaka pale rais aliposema kuwa ziliibiwa na ni lazima wamuunge mkono kuhakikisha kuwa pesa hizo zitarudishwa.

anasema kuwa kuna watu wanasema kuwa kuna watu wanapayuka ,na hata wakipayuka ni haki yao na hata kama Microfone zikipasuka spika ataweka nyingine .
Asema kuwa kama wengine wanaongea kwa upole ,waseme maneno ya busara na yawaingie mafisadi mpaka rohoni mwao.

Asema kuwa kuna wabunge wanathubutu kuwatetea mafisadi ,hii ni aibu.

Asema kuwa nchi hii sio masikini na kama waarabu na mafuta yao basi sisi na madini yetu na hao wazungu wanaokuja hapa hawaji kutufanyia kazi,ila wanafanya kazi zao.

Asema kuwa hakuna usimamizi wa Tanzanite kwani hakuna anayehakikisha kuwa zinapatikana kiasi gani.

Alitembelea migodi ya Mererani na kukuta kuwa watanzania wanateseka sana kwani hata wakati wa kuchambua Tanzanite mikono yao inakuwa imefungwa na hata kama wakiwashwa hawawezi hata kujikuna .

Ataka ripoti ya tume ya Jenerali Mboma bungeni kuhusu kutatua mgogoro wa Kitalu B na C.

Amtaka waziri mkuu kupiga marufuku ununuzi wa fenicha kutoka nje ya nchi kwani hapa kwetu hatuna tatizo la mbao na hivyo akifanya hivy serikali itawekeza nchini kwani ndio wanunuzi wakubwa wa fenicha.

anaendelea kusema kuwa madukani kuna bidhaa feki nyingi sana asema kuwa waziri mkuu anatakiwa kulitupia macho.

Ununuzi wa magari ya serikali lazima yawe yananunuliwa kwenye pull na sio kila mmoja kujinunulia la kwake .

Nikweli kabisa baadhi ya migodi haikaguliwi na serikali yetu. Ajabu na kweli!!

Mimi nawafahamu vijana wengi walioajiriwa na ile kampuni iliyoletwa na serikali ya mkapa kutoka, kama sikosei, uingereza iliyokuwa inafanyakazi kwa kushirikiana na serikali. Kampuni hii yenye jina la Alexstewart and Gorvernment co-operation, ilimaliza mkataba wake baada ya baadhi ya wabunge wetu kuipigia makerere ambapo vijana wote waliokuwa wameajiriwa na kmpuni hii walihamishiwa wizara ya nishati na madini. Mpaka sasa bado wanafanya kazi hiyo ya kukagua mwenendo wa uchimbaji wa madini hapa nchini. Kila mgogi unaokaguliwa umepangiwa vijana wawili ambao hufanyakazi kwa utaratibu wa kubadilishana. Kila mmoja hukaa mgodini kwa wiki 9 kabla hajabadilishana na mwenzake ambaye naye hufanya kazi wiki 9 kabla mzunguko haujajirudia. Hawa vijana wote wana-degree ya chuo kikuu cha dar es salaam, katika fani ya chemical and process engineering.

Chakushangaza ni kwamba, baadhi ya migodi ukiwemo ule wa TanzaniteOne(Mererani) na ule wa almasi Mwadui haikaguliwi na wala haimo kwenye orodha ya migogi inayokaguliwa au itakayokaguliwa.

Huu ndio utendaji wa serikali yetu ya ccm iliyojaa kila aina ya ufisadi!

KWA MTINDO HUU BADO TUNA SAFARI NDEFU KUYAFIKIA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

MUNGU TUPE SIRAHA IMARA YA KUPAMBANA NA MAFISADI.
 
Back
Top Bottom