Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

kazi kweli kweli
kumekucha wiki ijayo hiyoo!!!!!!
mi naelekea zangu bungeni kuyapata mwenyewe
 
Kwa kweli amenena lakini nasikia wananchi hawamtaki eti kamwashia moto shemeji yao Mkapa...kweli huyu anastahili pongezi anadondosha hata tembo kwa unyoya.
Kazi inaendelea.
 
Maua haya yanachanuka na kukauka mapema wakati yakiwa na rangi nzuri za kupendeza.
 
Mh.Kimaro yuko kwenye ukweli ninaouamini kuwa 'pale tuliposahau misingi ya Azimio la Arusha ndipo tulipoanza kuitafuna nchi'

Ahadi za mwana TANU na miiko ya utumishi wa umma kwenye Azimio la Arusha vilikuwa nguzo tosha za kutengeneza jamii adilifu na viongozi adilifu.

The Beautyful ones are not yet Born
 
Saa ya ukombozi inakaribia, wenye mikanda fungeni mikanda yenu kwani nchi itapitia misukosuko mingi kabla ya kukaa sawasawa kwenye anga na kuruka kwa usalama, Mkapa & coy wamejiandaa kuakikisha hakuna change yeyote ili waendelee kula taratibu bila kupigiwa kelele msishangae kesho kimaro mambo yakawa magumu kwake.

Mzindakaya kamtetea mkapa na anataka asiandikwe, hawa ndo wanafiki tunaosema mpaka bunge linaisha tunawalist siku moja lazima watatueleza kama wananchi walipata wapi kiburi walichonacho leo wanaiba na kutaka wasiandikwe, lakini mtu akiiba kuku wanasema mchome moto.
 
The guy seems to be smart

Imagine Tanzania with Serikali ya Mseto

President = Mwakyembe

PM = Kimaro

Vice President = Anne Kilango

Minister wa madini = Kabwe

Fedha = Slaa

Governor BOT = ?????


Ufisadi utatoweka???????? Mwanga wa maisha bora utaonekana?????..........

''hapo ndipo utajua nini maana ya siasa''
 
mimi nilidhani kimaro ni weak na opportunist, nikafanya uchunguzi jimboni kwake.
inaonekana ameanza kuwatetea na kuwatumikia wanachi wake tangu mwanzo, mabadiliko yanaonekana.
kwa hiyo ni kweli nimtetezi wa wananchi, (kwa sasa) nieanza kusikiliza kwa umakini rasmi.
tunaomba tu apiganie haki na si kutumiwa nakambi fulani, kama ya sumaye au nyingine yoyote inayopenda outspoken ppl.
APIGANIE HAKI. tuko pamoja nae.
 
Mushi bwana umezidi kuwa cynical! Humuamini mtu yeyote sasa hivi, inabidi 2010 utinge bungeni mwenyewe!
 
Kwa kweli amenena lakini nasikia wananchi hawamtaki eti kamwashia moto shemeji yao Mkapa...kweli huyu anastahili pongezi anadondosha hata tembo kwa unyoya.
Kazi inaendelea.

Hao wananchi ni ueewa mdogo tu, wakipigwa shule wakafunguka macho watajua anawapigania wao. Ujue elimu ya darasa la saba imetudumaza kweli watanzania, na hii ndiyo siraha kubwa itumiwayo na CCM kutuburuza wapendavyo, kwani wanajua wananchi hawajui lolote wakipewa pilau tu basi!
 
Wakuu, heshima mbele.

Nimekua mfuatiliaji wa hii forum kwa muda mrefu kama observer, lakini hali ya taifa ilipo imenilazimu nianze kuchangia huu mjadala.

Huyu mheshimiwa inaonekana amekua mwiba... Binafsi leo nimeshuhudia matangazo LIVE ya bunge kupitia TBC1 yakikatishwa wakati alipokua anashusha makombora around saa moja na dakika kumi hivi jioni na badala yake yakawekwa matangazo. Ilianza kuzimwa camera wakati yeye anaongelea issue ya Tanzanite sorting, sauti ikabaki. Then wakakata na sauti yake.

After about fifteen minutes, matangazo ya bunge yakarudi tena LIVE TBC1. Wakati TBC1 haipo hewani, hata Star Tv nao hawakua wakionesha bungeni LIVE.

To me it was more than a coincidence. lakini nimeogopa kua judgemental on TBC1.

Wanaofaham zaidi wanaweza kutusaidia nini haswa kilitokea.


Nilisema na nitaendelea kusema TBC= Kilinda Ufisadi
 
Hii ni njama kubwa sana ambayo imepangwa na kupangika ili kurudisha imani ya CCM kwa wananchi, piga galagaza lakini hatutoboani macho ,rudi kijijini ponda wabunge wenzako washambulie uwezavyo na hata ikiwezekana toa misimamo mikali japo haitotekelezwa tutajua vya kuiyeyusha.
Ndivyo wandugu inavyotokea hivi sasa kama mnavyoona kwenye vikao vywa bunge CCM wengine ni wakali sana na wengine wanajibu ujeuri huku wabunge wa upinzani wakiwa wamekenua na kuona sasa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe wakae pembeni waangalie mwisho wakitahamaki kikao kimefungwa kitaendelea na mada nyengine.
Huu ni wakati wa vyama vya upinzani kugongomelea msumari mwengine nje ya vikao vya bunge ,wapite kijiji kwa kijiji mikutano isisimame leo kunapingwa hili kesho kunapingwa hili huku uwanja umejaa mangoma ya kienyeji kiasi wananchi nao wanashughulishwa katika harakati hizi sio kukaa na kungojea bungeni kumesemwa nini magazeti yamemnuu nani.
CCM wanatumia tactic hizi kusogeza muda wanabishana sana wakiharibu muda wa kutoa maamuzi ,wanaunda kamati wanazijadili Bungeni wanazijadili serikalini wanazijadili kwenye NEC ,yote si kwamba kuna la maana watakalo kuja nalo zaidi wataongeza kamati kuichunguza kamati kuichunguza kamati mpaka kiyama.
Wapinzani warudi kwa Wananchi na wao wachome na kuunguza huko mikoani
kiasi wabunge wakirudi makwao waone upinzani umeshachoma kila kitu na wananchi wanamtizama mbunge kwa jicho la utatuona kwenye uchaguzi.
 
Hii ni njama kubwa sana ambayo imepangwa na kupangika ili kurudisha imani ya CCM kwa wananchi, piga galagaza lakini hatutoboani macho ,rudi kijijini ponda wabunge wenzako washambulie uwezavyo na hata ikiwezekana toa misimamo mikali japo haitotekelezwa tutajua vya kuiyeyusha.
Ndivyo wandugu inavyotokea hivi sasa kama mnavyoona kwenye vikao vywa bunge CCM wengine ni wakali sana na wengine wanajibu ujeuri huku wabunge wa upinzani wakiwa wamekenua na kuona sasa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe wakae pembeni waangalie mwisho wakitahamaki kikao kimefungwa kitaendelea na mada nyengine.
Huu ni wakati wa vyama vya upinzani kugongomelea msumari mwengine nje ya vikao vya bunge ,wapite kijiji kwa kijiji mikutano isisimame leo kunapingwa hili kesho kunapingwa hili huku uwanja umejaa mangoma ya kienyeji kiasi wananchi nao wanashughulishwa katika harakati hizi sio kukaa na kungojea bungeni kumesemwa nini magazeti yamemnuu nani.
CCM wanatumia tactic hizi kusogeza muda wanabishana sana wakiharibu muda wa kutoa maamuzi ,wanaunda kamati wanazijadili Bungeni wanazijadili serikalini wanazijadili kwenye NEC ,yote si kwamba kuna la maana watakalo kuja nalo zaidi wataongeza kamati kuichunguza kamati kuichunguza kamati mpaka kiyama.
Wapinzani warudi kwa Wananchi na wao wachome na kuunguza huko mikoani
kiasi wabunge wakirudi makwao waone upinzani umeshachoma kila kitu na wananchi wanamtizama mbunge kwa jicho la utatuona kwenye uchaguzi.

Inaitwa Good cop, Bad Cop...........
 
Date::6/26/2008
Wabunge wawajibike kwa maamuzi ya Bunge
Mwananchi

JUZI Mbunge wa Kyela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya iliyochunguza mchakato wa zabuni ya uzalisha umeme wa dharura, uliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond Development, Dk Harrison Mwakyembe aliwatolea uvivu wabunge wanaovunja taratibu za Bunge kwa kuanza kujadili upya maamuzi yaliyotolewa na Bunge.

Hoja ya Dk Mwakyembe ilijikita kwa baadhi ya wabunge wasiofuata kanuni za Bunge ama kwa makusudi ili kuwatetea na kulinda maslahi ya watuhumiwa au kutokujua, jambo ambalo ni sawa na kulivunjia heshima Bunge na wabunge kwa ujumla.

Suala la Richmond, ambalo lilitolewa maamuzi katika Mkutano wa Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu, baada ya kamati hiyo kufanya kazi yake na kutoa ripoti iliyoambanatana na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa, ambayo yaliridhiwa na Bunge na kuwa maamuzi rasmi ya chombo hicho cha kutunga sheria, bado linatafutiwa nafasi ya kujadiliwa katika Bunge kupitia kwa baadhi ya wabunge kwa lengo la kuwasafisha waliotumiwa kuhusika.

Si nia yetu kurejea yaliyozungumzwa na Dk Mwakyembe kuhusiana na suala hilo, ambalo limetafsiriwa kuwa baadhi ya watu waliojitokeza kufufua na kuwatetea watuhumiwa kabla hata serikali haijatoa ripoti ya hatua za kuwachukuliwa kama ilivyoagizwa na Bunge, ila tunataka kujua kama wabunge wanafahamu kanuni za Bunge zinasemaje kuhusu kuzungumzia maamuzi yaliyokwishatolewa na chombo hicho cha kutunga sheria nchini.

Kama tungetumia lugha ya Bunge, sisi tungesema tunaomba mwongozo wa Spika juu ya jambo hilo, kama ni haki wabunge kufufua hoja iliyotolewa maamuzi kwa namna inavyofanyika sasa, kwa mbinu inayotumiwa na ya baadhi ya wabunge kuchomekea ndani ya hoja nyingine suala hilo zito ambalo limeitikisa nchi yetu.

Tunajua kuwa wabunge na Watanzania wote wana uhuru wa kusema na kuhoji juu ya jambo lolote lililotolewa maamuzi iwe bungeni au serikalini, lakini katika majukwaa tofauti yalipotolewa, kwa sababu tunafahamu kwamba, maamuzi yote yaliyotolewa yanakuwa maamuzi ya pamoja ya chombo husika, kinyume chake ni kuvunja kanuni inayounda chombo hicho.

Si tu katika masuala ya Bunge, hata serikali ina utaratibu wake, kwani maamuzi ya vikao vya baraza la mawaziri yanakuwa ya serikali au mawaziri wote, hata kama mmoja wao hakukubaliana nayo akiwa kikaoni, lakini kama yamepitishwa yanakuwa yao na atayalinda, vinginevyo atakuwa anakwenda kinyume na anatakiwa ama kujiuzulu au kuondolewa kwenye wadhifa wake, kama ilivyotokea kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Pili, Augustine Mrema alivyopoteza nafasi zake serikalini baada ya kusema kinyume na maamuzi ya baraza la bawaziri bungeni.

Mbali na ngazi hizo, hata kwenye vyama vya siasa, kikiwemo Chama Cha Mpainduzi (CCM), wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), wana taratibu zinazolinda maamuzi yanayotolewa kwenye vikao vyao, ambayo mmoja wao akikiuka kwa kuyapinga nje vya vikao hivyo, huchukulia hatua ikiwemo ya kupoteza ujumbe wake kwenye kikao husika. Kwa mjumbe anayefanya kosa kama hilo, CCM huitwa: "Huyu si mwenzetu".

Sasa, kwa mazingira ya namna hiyo, tunahitaji kupata mwongozo wa Spika, kwamba ni halali au si halali kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kujadili maamuzi yaliyokwisha amriwa kwenye mkutano halali, ambao wabumge husika walishikiri, walipata nafasi ya kutoa mawazo yao na hatimaye kupigiwa kura ambayo iliungwa mkono na wabugne wengi, kuuhalalisha na kisha kuiagiza serikali kuufanyia kazi?

Suala si hoja ya Richmond tu, bali hata kwa hoja nyingine zinazowasilishwa bungeni zikitolewa maamuzi je, ni halali kuzifufua kwa mtindo unaotumiwa sasa na baadhi ya wabunge kwenye suala la Richmond na hata la EPA au kuna njia mbadala ya kubatilisha maamuzi.

Tunadhani kwamba, kama wabunge hao wanaona yalifanyika makosa katika maamuzi yaliyofikiwa walitakiwa kufuata taratibu za Bunge kwa kuwasilisha hoja ya kuomba kujadili upya maamuzi yaliyofikiwa pamoja na kurejea taarifa na mchakato mzima wa kamati husika.
 
Mzindakaya alipuliwa bungeni

na Mwandishi Wetu, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


WABUNGE wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameeleza kusikitishwa kwao na tabia ya baadhi ya wabunge wenzao kuwashambulia wenzao wanaotoa maoni yao kuhusu viongozi wakuu serikalini na wale waliostaafu.

Mtu wa kwanza kueleza dukuduku lake hilo alikuwa ni Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo ambaye katika mchango wake alioutoa juzi jioni wakati anajadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopitishwa jana jioni, alisema kuwa anaamini michango inayotolewa na wabunge hailengi mtu bali inazingatia umuhimu wa hoja.

Mbunge huyo ambaye ni mke wa mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM) alisema wabunge wamekuwa wakichangia mijadala mbalimbali bungeni, lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanasaidiwa kupiga hatua za maendeleo na si vinginevyo.

"Lengo na nia (ya kutoa hoja hizo) ni moja tu kuhakikisha Mtanzania anatoka hatua moja kwenda nyingine," alisema Shellukindo kauli ambayo ilionekana waziwazi kukosoa hoja zilizotolewa na Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) au Mbunge wa Kyela, Harrison Mwakyembe (CCM).

Aliwataka watu wanaodhani kuwa yanayosemwa bungeni na baadhi ya wabunge yanamlenga mtu fulani kuachana na fikra hizo kwani hilo si lengo la kauli hizo.

Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi kwa kuwalaumu baadhi ya wabunge na viongozi kwa kusema kuwa wameshindwa kufikiri na kuwa wabunifu, na ndiyo maana mambo mengi yanakwama.

"Hata hapa bungeni watu hawafikiri, wanasubiri mtu aseme halafu wao wanadakia hoja," alisema Shellukindo pasipo kufafanua.

Muda mfupi baadaye, Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumnyoshea kidole Rais mstaafu Benjamin Mkapa wakati wa mkutano uliopita wa Bunge, alisimama na kusisitiza hoja hiyo ya Shellukindo.

Akizungumza huku akinukuu, vifungu kadhaa katika ahadi za wanachama na viongozi wa CCM, Kimaro alisema anaamini kila mbunge anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu mambo anayoyatetea pamoja na yale anayotumwa na wapiga kura wake.

Miongoni mwa ahadi alizonukuu Kimaro, ambaye hoja yake hiyo dhidi ya Mkapa imezua maneno ya kumpinga ndani ya vikao vya CCM na miongoni mwa wabunge wenzake wa CCM, ni zile zisemazo; ‘Nitaitumikia nchi yangu kwa nguvu na moyo wangu wote’, ‘Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa’, ‘Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu au cha mtu mwingine kwa manufaa yangu binafsi’ na ile isemayo ‘Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko’.

Alisema mbunge au mwananchi yeyote anapotoa maoni yake, hapaswi kushambuliwa kwa sababu anafanya hivyo akilindwa na katiba, sheria na kanuni zilizopo.

"Kwa hiyo hapa bungeni ni ukweli, fitina ni mwiko, tukisimamia hilo maisha bora yatapatikana… hakutakuwa na kutafutana… CCM si mali ya mtu, ni ya wanachama," alisema Kimaro.

Alisema kuwa kila mtu anapaswa kula jasho lake mwenyewe, lakini inashangaza kuwa siku hizi vitendo vya rushwa, wizi na ubadhirifu wa fedha za serikali, vimegeuka kuwa wimbo wa taifa.

"Kila Mtanzania na kiongozi lazima akemee mambo haya. Rais na Waziri Mkuu wanakemea, lazima tuwaunge mkono kama tusipowaunga mkono, nani mwingine atawaunga?" alihoji mbunge huyo.

Kimaro aliwataka watu wanaosikiliza tuhuma zinazotolewa kutoona kuwa zinalenga kumchafua mtu kwani hata ilipoelezwa awali kuwa fedha za EPA zimeibwa, watu hawakuamini hadi rais alipotangaza kuwa ni kweli sh bilioni 133 za EPA zilikuwa zimeporwa.

Alisema yeye amejitolea kumuunga mkono rais katika suala hilo na kamwe hatorudi nyuma.

"Wapo watu hapa wanasema, wana sauti zao kubwa wengine wanapayuka… waache wapayuke, kama microphone zitapasuka Spika ataweka nyingine...Wenye kusema taratibu nao waendelee kusema na sauti zao zichome kama mwiba...Wengine wanasema sungura ni mdogo, jamani Tanzania ni ndovu mkubwa tuna kila kitu humu, lakini wanakula wachache, Tanzania ni nchi nzuri," alisema.

Katika kauli yake, Mzindakaya aliwanyooshea kidole wabunge wanaomtuhumu Mkapa na kusema kiongozi huyo mstaafu amefanya mambo mengi kwao, ikiwamo na kufanikisha ujenzi wa jengo la kisasa la Bunge.

Aidha, aliishangaa serikali kwa kuendelea kukaa kimya wakati kiongozi huyo akituhumiwa na kuchafuliwa na watu pamoja na vyombo vya habari.
 
Kwa hili Mzindakaya amekurupuka

Kulwa Karedia
Tahariri
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WIKI hii mzimu wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond umeibuka tena bungeni, baada ya baadhi ya wabunge kuamua ‘kuwasafisha' baadhi ya mawaziri walioachia ngazi kutokana na kashfa ya ufisadi.

Hatua ya kuwasafisha ‘watuhumiwa' hao imeonekana kuwakera wabunge wengine na wananchi kwa ujumla, jambo lililoonekana wazi kuwa baya.

Lakini wakati wabunge wakiwa wanatafakari suala hilo, Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya, naye aliamua kuvunja ukimya wake, baada ya kuitaka serikali kutoa tamko juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Hatukatai kwamba Mkapa alijijengea umaarufu ndani na nje ya nchi kutokana na msimamo wake, lakini kama kuna madhambi aliyafanya basi kuna kila sababu ya kujadiliwa, hasa baada ya kustaafu kwa kuwa sheria ya kinga ya viongozi haipo upande wake.

Ngoja nieleze namna sheria hiyo inavyofanyakazi: kinga ya viongozi inakuwapo pale tu kiongozi huyo hasa Rais aliye madarakani anapochukua uamuzi mbaya au mzuri kwa manufaa ya taifa na wananchi wake.

Kwa mfano, Rais anaweza kuruhusu vita endapo nchi husika inavamiwa au inaporwa ardhi. Hapo hata watu wakifa ama kudhurika baada ya utawala, Rais huyo atakuwa na kinga. Lakini si kwa Mkapa, alitumia rasilimali za nchi kwa maslahi yake na sasa taifa linaingia hasara kwa sababu hiyo.

Aliruhusu wawekezaji katika madini na akakubali watendaji wake waingie mikataba hiyo mibaya, hali inayofanya rasilimali za taifa kuchukuliwa na Wazungu kwa mrahaba na kodi ndogo.

Katika nchi zilizoendelea, hata kama rais ni mtu maarufu akitoka madarakani kama kuna madhambi aliyafanya huwa yanaibuliwa, sasa itakuwaje sisi tunyamaze? Huu si muda tena wa kulindana.

Kiongozi safi aliyejijengea sifa nzuri hatarajii serikali imlinde, ni sifa hizo hizo kutoka kwa wananchi wake aliowangoza zitakazotumika kumlinda na kumtetea, sasa inakuwaje Dk. Mzindakaya akarupukie suala hili?

Kibaya zaidi, Dk. Mzindakaya ni miongoni mwa viongozi walio wahi kushika nafasi tofauti katika nchi, tena ni mmoja wa wabunge wa siku nyingi, sasa anaitaka serikali kuvinyamazisha vyombo vya habari vinavyomwandika Mkapa.

Sisi wenye taaluma ya uandishi tunasema kauli ya Mzindakaya hatuwezi kukubali ikapita hivi hivi, lazima ‘tuitendee haki' kwa vile ameonekana dhahiri kuingilia uhuru wao.

Dk. Mzindakaya huyo huyo amesahau alivyokuwa mwiba mkali katika utawala wa Mkapa hadi kusababisha aliyekuwa Waziri wa Viwanda wakati huo Idd Simba kujiuzulu!

Simba alijiuzulu wadhifa huo baada ya Dk. Mzindakaya kushusha makombora mazito bungeni dhidi ya waziri huyo kuhusu sakata la uingizaji wa sukari.
Kauli ya Dk. Mzindakaya inanikumbusha msemo wa Kiswahili usemao ‘mla ndizi husahau ila mtupa maganda hasahau'. Hii inaonyesha wazi kwamba mwenzetu amekwishasahau.

Kama kawaida hakuishia hapo, aliendelea na kulipua mabomu yake kila wakati wa mkutano wa Bunge ulipokaa mjini Dodoma, na kusababisha baadhi ya wabunge kuingiwa wasiwasi katika vikao hivyo.

Hapana shaka wakati mzee Mkapa akiiongoza nchi hii, alifanya mambo mengi mazuri na mabaya. Lakini kwa vile wakati huo alikuwa madarakani, ilikuwa vigumu kumjadili. Lakini sasa kwa uwazi yanaonekana, kutaka serikali iwazuie wabunge na wanasiasa kulizungumzia hili, si kuwatendea haki.

Dk. Mzindakaya asitake kutuhudaa, Watanzania tunamuomba aache Mkapa mwenye ajitokeze na kujibu tuhuma zinazomwandama, kama alivyofanya hivi karibuni akiwa kijijini kwao Lupaso, Masasi Mtwara.

Miongoni mwa tuhuma anazotuhumiwa Mkapa ni pamoja na kuwa mfanyabiashara kwa anuani ya Ikulu, kukopa fedha nyingi kwa jina la moja ya kampuni zake kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kujipatia mgodi wa mkaa wa mawe Kiwira kwa njia zisizoeleweka na mengine mengi. Majibu ya yote haya anayo mhusika mwenyewe. Na si mwingine bali ni mzee Mkapa mwenyewe.

Sisi tunasema kwamba kama Mkapa alifanya mazuri yataendelea kuwapo daima milele kama watangulizi wake walivyofanya, tena Watanzania watamuenzi kwa matendo mema.

Nani asiyeelewa jinsi Dk. Mzindakaya alivyokuwa moto wa kuotea mbali kabla ya kuwezeshwa na serikali ya Mkapa kwa kupewa mkopo uliyomwezesha na kuendeleza rachi yake ya mifugo mkoani Rukwa?

Ukweli ulio wazi; serikali ya Mkapa ilimwezesha kwa kumpatia mkopo wa mabilioni ya shilingi.

Mkopo huu aliutumia kujengea machinjio ya ng'ombe na kiwanda cha kusindika nyama, je, fedha kiasi chote hiki kumilikiwa na mtu mmoja ni haki, ikizingatiwa kuwa ni mali ya wavuja jasho wa nchi hii?

Tunasema sasa umefika wakati mzuri wa Dk. Mzindakaya kujitokeza na kutoa ufafanuzi wa kutosha au mazingira yaliyofanya apate mkopo huu mnono.

Dk. Mzindakaya aliwahi kusema: "Baada ya benki kadhaa kukataa kumpatia mkopo hakukata tamaa, kwani alibisha hodi katika benki ya Standard Chartered iliyompatia mkopo wa sh bilioni 9.7 wa muda mrefu. Mkopo huo umetolewa chini ya udhamini wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)".

Ndiyo maana nasema kwamba Dk. Mzindakaya amekurupuka kwa hoja hii, sasa anapaswa kueleza ukweli wa mambo juu ya mikopo yake hii aliyopata wakati wa utawala wa Mkapa.

Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa ambacho kama Watanzania wangepewa zaidi ya watano au kumi, basi tunaamini umaskini uliokithiri ungeweza kupungua miongoni mwetu.


karedia2005@yahoo.co.uk
0756 511 845
 
Labda akili yangu inakwenda kinyume nyume lakini kauli ya Mzindakaya nilivyoielewa mimi ni kwamba serikali iseme neno kuhusu tuhuma hizi. Na pale serekali itakapoamua kusema jambo linaweza likawa kukubaliana na kashfa hizi na uamuzi utakaochukuliwa(which will never happen under this sun)au kukanusha na kuwaambia wananchi na waandishi wa habari wafunge midomo ambavyo pia ni vigumu.

Matamshi ya huyu bwana yanahang mahali.
 
"you can fool some people some times, but you can't fool all the people all the time"

CCM amkeni watu wameshachoka msiisuburi aibu, kubalini yaishe, siasa zenu zinapeleka nchi pabaya
 
Nafikiri beatrice shellkindo ametoa maoni yanayotoa ukweli halisi hasa kwa wabunge wanaoshindwa kufanya walichotumwa na wananchi wao bungeni.

Ni aibu mbunge kushabikia ufisadi na kutumia bunge kutetea maovu.
 
Zitto azua jambo bungeni
Basil Msongo, Dodoma
Daily News; Tuesday,July 01, 2008 @00:04

MBUNGE wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi (CCM), ametaka ufanyike uchunguzi kuhusu kauli za Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kuwa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hawaelewani, na kwamba fomu za mali za viongozi zilizopo kwa Spika wa Bunge zinatofautiana na zilizopo katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Amesema ikithibitika ni uongo, Mbunge huyo aombe radhi. Masilingi alisema kauli ya Kabwe kuhusu Takukuru lazima itolewe maelezo na akahoji Kabwe amefahamu vipi kuwa kuna mgawanyiko mkubwa na mgongano baina ya wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati hafanyi kazi huko.

Masilingi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema anaamini Kabwe ana uhakika na aliyoyasema na kwa kuwa hafanyi kazi Takukuru lazima wafanyakazi wa taasisi hiyo wamemueleza hayo. Alisema lazima pia uchunguzi ufanywe kufahamu Kabwe amefahamu vipi kuwa kuna fomu za mali za viongozi wa umma zilizopo katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambazo zinachezewa na ni tofauti na zilizopo katika Ofisi ya Spika wa Bunge.

Masilingi aliyasema hayo baada ya Kabwe kumaliza kuchangia hoja ya makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2008/2009 iliwasilishwa jana bungeni mjini Dodoma. Kabwe alisema taarifa za mali za viongozi wa umma zinachezewa katika sekretarieti hiyo na hivyo suala hilo lichunguzwe pamoja na kuchunguza tofauti ya fomu zilizopo huko na zile alizonazo Spika wa Bunge.

“Siri zetu zote, mali zetu zote, madeni yetu yote zinafahamika....” alisema Kabwe na pia akawaeleza wabunge kuwa kuna umuhimu wa kuiangalia upya Takukuru kwa kuwa kuna matatizo makubwa ndani ya taasisi hiyo. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, viongozi wa taasisi hiyo hawaelewani na watumishi wa chini, kuna Kamati ya kuwawinda wanaoisema Takukuru na kwamba mgawanyiko huo unasababisha Takukuru ishindwe kushughulikia kesi za ufisadi.

Pia alisema Bunge linapaswa kupitia upya sera na Sheria ya Usalama wa Taifa kwa kuwa hivi sasa Idara hiyo hairuhusiwi kuchukua hatua, inatoa ushauri tu. “Pesa za EPA ziliibwa kwa cash, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa inafahamu,” alisema Kabwe na kusema kuwa Meremeta haihusiani na Usalama wa Taifa hivyo serikali kupitia Bunge lazima iwaeleze ukweli Watanzania akidai kuwa Meremeta ni wizi wa waziwazi.

Masilingi alisema anavyofahamu hakuna tofauti ya rushwa kubwa na rushwa ndogo, anafahamu kuna watu wanaoichukia Takukuru na isipokuwapo taifa litaangamia. Alisema watu wanawatuhumu wenzao kuwa ni mafisadi nao wachunguzwe wasije wakasakwa wanaotuhumiwa kumbe wengine wapo, na akasema kuna mafisadi na vifisadi.

“Mimi sichukii mtu akisema fisadi fisadi, tusije tukasema fisadi fisadi tukawapita mafisadi,” alisema Masilingi na kuitaka Takukuru ichunguze kwa makini kabla ya kuwakamata watuhumiwa. Alisema watumishi wa umma wanapaswa kujiamini, wasiogope kujenga maghorofa au kununua magari ya kifahari kwa sababu ya hofu ya kuitwa mafisadi.

Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika wizara hiyo, Grace Kiwelu alisema wananchi wengi hawaamini kuwa Takukuru ni chombo cha kupambana na rushwa, bali taasisi ya kulinda mafisadi.

“Kambi ya upinzani inaitaka serikali ianzishe mchakato wa kuichunguza Takukuru yenyewe kwa lengo la kujisafisha, kuona kama yenyewe ni safi, jambo ambalo kimsingi linaashiria kuwa haiko safi ndiyo maana inashindwa kuchukua hatua kwa watuhumiwa mbalimbali,” alisema.

Mbunge wa Kibaha Mjini, Dk. Zainab Gama (CCM), alisema inapaswa kufuatilia taarifa za rushwa serikalini, mahakamani na kwamba hata kama zinawahusu wabunge wachunguzwe. Dk. Gama alisema kuna umuhimu wa kuwa na kamati ya Bunge inayoshughulikia rushwa kama ilivyo kwa Kamati ya Bunge ya Ukimwi, na pia Takukuru wawe wanatoa taarifa bungeni kuhusu utendaji wao.
 

Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika wizara hiyo, Grace Kiwelu alisema wananchi wengi hawaamini kuwa Takukuru ni chombo cha kupambana na rushwa, bali taasisi ya kulinda mafisadi.

“...serikali ianzishe mchakato wa kuichunguza Takukuru yenyewe kwa lengo la kujisafisha, kuona kama yenyewe ni safi, jambo ambalo kimsingi linaashiria kuwa haiko safi ndiyo maana inashindwa kuchukua hatua kwa watuhumiwa mbalimbali,” alisema.

Wow.......!

Nimekubali.
 
Back
Top Bottom