Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

CIS hawana uhusiano na EPA .

Hizi ni fedha nyingine za wizi uliofanyika miaka ya tisini na hivyo hapa ni issue ya tofauti na EPA.
Nitaweka bandiko la CIS muda ujao then fuatilia kwa makini.

Mkuu Mpaka Kieleweke, asante sana na ninasubili kwa hamu sana.
 
BRAVO kambi ya upinzani Bungeni!!

Wakuu, naomba kama kuna mwana JF anayefahamu tofauti kati ya EPA na CIS (COMMODITY IMPORT SUPPORT) anieleweshe. Hotuba ya Mh. Slaa imeelezea jambo zito kuhusu CIS lakini mimi sijaelewa tofauti au uhusiano kati yake na EPA.

Hapa ndipo my boo - Mkjj huwa anamwaga data, naona amepunguza sana uchangiaji hapa jamvini sijui nini kinaendelea.

Mkjj tusaidie mwenzangu, tofauti ya EPA na CIS ni ipi.... Ningeeleza lakini sitaki kujikuta nimetumia laws za physics bureeeeeee...na nikachanganya vijana wetu wa DUPSA (sijui kama nimepatia) toka mlimani.
 
Mabilioni ya TCRA yaibua utata bungeni

Mwandishi Wetu Juni 25, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Ni za mahujaji, barabara ya Msata, Uwanja wa Ndege wa Mwanza

UTATA umeibuka serikalini kuhusu mabilioni ya fedha zilitolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya baadhi ya wabunge kuhoji zilivyotumika na sheria waliyotumia mawaziri kuagiza kutolewa kwa fedha hizo.

Habari zinaeleza kwamba Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POC) imejipanga kuhakiki matumizi ya fedha hizo zilizoelekezwa katika miradi ambayo haijafahamika kwa hakika kama imekwisha kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Habari zinaeleza kwamba TCRA ilitoa zaidi ya Sh bilioni 15 kwa maelekezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Miundombinu na Wizara ya Fedha, kwa ajili ya miradi mbalimbali ambayo haikuwa katika bajeti ya mamlaka hiyo.

Akichangia Bajeti ya Serikali wiki iliyopita, Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Susan Lyimo, alitaka maelezo kuhusu maagizo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu yalivyotumika kutoa fedha kutoka TCRA kwenda katika miradi ya barabara na uwanja wa ndege wa Mwanza, miradi ambayo haiko katika sekta ya mawasiliano. Lyimo ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

TCRA imeelekezwa kutoa fedha hizo na viongozi wa juu wa serikali kwa kuwa mamlaka hiyo ni mali ya Serikali na fedha hizo ni za Serikali.

Viongozi wanaotajwa kushiriki vikao vya kuidhinisha na kuomba fedha hizo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Miuondombinu, Andrew Chenge na Basil Mramba na aliyekuwa Naibu Waziri, Wizara ya Fedha, Abdisalaam Issa Khatib.

ALIYEKUWA Naibu Waziri, Wizara ya Fedha, Abdisalaam Issa Khatib
Miongoni mwa miradi iliyoombewa fedha kutoka TCRA ni mradi wa barabara ya Msata kwenda Bagamoyo kwa kiwango cha lami uliopatiwa Sh bilioni 7 kati ya Sh bilioni 10 zilizoombwa, mradi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza uliochotewa Sh bilioni 7.1 na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) waliopewa Dola za Marekani milioni 1 (Sh Bilioni 1.2).

Lowassa, Mramba na Abdisalaam walikutana na watendaji wakuu wa serikali akiwamo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Goodluck Ole Medeye, Machi 10, 2006 na kuelekeza mamlaka hiyo na idara nyingine kutoa fedha za haraka kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Msata hadi Bagamoyo.

"Kwa vile barabara kuu kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kaskazini ni muhimu sana kwa uchumi, Waziri Mkuu ameelekeza kwamba barabara kutoka Msata kwenda Bagamoyo ipewe kipaumbele na iwekwe lami haraka iwezekanavyo kwa kutumia fedha za TCRA na vyombo vingine vya serikali ambavyo fedha zake zinaweza kutumika," ameeleza mtoa habari wetu akinukuu mawasiliano ndani ya Serikali.

Kwa mujibu wa mtoa habari huyo Serikali ilijenga hoja hiyo kipindi cha matatizo ya usafiri katika barabara iendayo mikoa ya kaskazini baada ya daraja la Lugoba wilayani Bagamoyo kuzolewa na mafuriko na Waziri Mkuu aliagiza utekelezaji wa mradi huo uliopangwa kugharimu Sh bilioni 35, uanze mara moja.

Hata hivyo, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POC) chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Mbunge wa Mbarali (CCM), Esterina Kilasi, ilishitushwa na maelezo ya TCRA walipokutana na menejimenti ya mamlaka hiyo Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kuwa na wasiwasi kama kweli fedha zilizotolewa zimefanya kazi iliyokusudiwa.

Habari kutoka serikalini zinaeleza kwamba tayari TCRA wamekwisha kutoa maelezo ya jinsi walivyoshinikizwa kutoa fedha hizo wakiegemea kifungu cha 56 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, inayompa Waziri mhusika kuingilia utendaji wa mamlaka hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya maofisa wa Serikali wamepinga tafsiri ya sheria hiyo wakieleza kwamba Waziri mhusika ama kiongozi yeyote hana mamlaka ya kuingilia mambo ya fedha ya mamlaka hiyo bali anachoruhusiwa ni kusimamia mambo ya kisera zaidi na kutoa ushauri wa kiutawala na masuala mengine pale tu panapotokea utata mambo ambayo hayakutokea.

Kuhusu mradi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, habari zinaeleza kwamba mwishoni mwa Desemba 2006, Wizara ya Miundombinu chini ya Chenge iliialiagiza TCRA kutoa Sh 7,130,000,000/- kukarabati uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uganda.

Kutokana na msukumo kutoka serikalini, TCRA ililazimika kukopa benki ya Stanbic kuweza kutoa fedha za awali zilizotakiwa kwa haraka kutoa malipo ya awali ambayo kuna habari kwamba fedha zake zilitumwa nje ya nchi zikielezwa kutumika kumlipa mkandarasi wa uwanja huo ambao sasa utalazimika kufanyiwa ukaguzi kuona kama fedha zilizotolewa zilitumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Habari zinaeleza kwamba Kamati ya POC imepanga kufanya ukaguzi maalumu kutembelea miradi iliyopewa fedha na TCRA ili kujiridhisha kama fedha zilizotolewa zimefanya kazi iliyokusudiwa, kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo baada ya kukutana na watendaji wa mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Dodoma.

Gharama za Uwanja wa Ndege wa Mwanza uliopangwa kukamilika Novemba 2007, zilielezwa kuwa ni Sh bilioni 8.2 ikiwa ni pamoja na gharama za mkandarasi (Sh bilioni 7.7) na msimamizi mkuu aliyepangiwa kulipwa Sh 501,879,531.

Kwa mujibu wa habari hizo, TCRA iliagizwa tena na serikali kupitia Wizara ya Miundombinu kutoa dola za Marekani milioni moja (Takriban Sh bilioni 1.2), kwa ajili ya kugharamia safari ya mahujaji wa Tanzania na nchi nyingine waliokwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kutokana na matatizo ya kiutendaji ndani ya ATCL.

MAHUJAJI waliokwama Uwanja wa Ndege Dar es Salaam
Fedha hizo zilizoingizwa katika akaunti ya ATCL zilielezwa kugharamia mahujaji hao kwa ajili ya kulipia mafuta ya ndege; uongozaji na paking ya ndege; huduma za vyakula na malazi kwa wahudumu wa ndege; na huduma za uwanja wa ndege Dar es Salaam na Jeddah.

Hata hivyo, tofauti ya fedha nyingine fedha zilizotolewa kwa mahujaji zilielezwa kwamba zingelipwa serikali katika kipindi ambacho hakijaelezwa kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Enos Bukuku.

Habari zinaeleza kwamba TCRA ililalamika kukwama kutekeleza miradi yake muhimu inayolenga kuboresha utendaji wake kama mamlaka nyeti kutokana na kulazimika kuchangia miradi iliyo nje ya majukumu yake katika sekta ya mawasiliano lakini serikali iliendelea kulazimisha kuchota.

TCRA ilielezwa kutoa ahadi ya kuchangia Sh bilioni 27.54 kwa ajili ya 'ujenzi wa makao makuu' uliotajwa kugharimu Sh bilioni 30.6 lakini inaelezwa kwamba hadi sasa mamlaka hiyo imetoa chini ya Sh bilioni 10 hadi Mei mwaka huu kutokana na majukumu mengine yanayoikabili ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mitambo ya kusimamia masafa.

Hii ni mara ya kwanza kuibuliwa kwa siri ya utolewaji wa fedha kutoka asasi mbalimbali pamoja na kuwapo taarifa kwamba asasi nyingi za serikali na umma pamoja na makampuni binafsi yamekua yakichangia kwa hiari ama kushinikizwa na serikali ama wanasiasa kuchangia miradi ama shughuli mbalimbali.
 
Source: Gazeti la RAIA MWEMA la tarehe 25 Juni 2008
http://www.raiamwema.co.tz
 
Barabara ya Msata- Bagamoyo imejengwa?
 
mwaka huu tutajionea mambo,
kila kukicha ni ufisadi tuu.
Swali langu ni Je,hizi pesa zote zitarudi lini ama ndio tunaambiwa uchunguzi unaendelea mpaka viongozi wana ng'oka madarakani?
 
Barabara ya Msata- Bagamoyo imejengwa?[/QUOTE]

Inawezekana Imejengwa au hata Haijajengwa, ila FEDHA zimetumika. Walaji ni walewale (EL, AC, BM) kinacholiwa ni kulekile (FEDHA) na wanaoingizwa mjini ni walewale (WATANZANIA).Mambo mwendo mdundo!!!
 
Akumbushia ahadi za mwana TANU.
Asema kuwa rushwa ni adui wa haki, asema kuwa ahadi zile ni muhimu na kila mbunge ameapa kuzilinda .

Asema wabunge wawe mstari wa mbele kupiga vita Ufisadi.

asema kuwa watanzania hawakuamini kuwa pesa za EPA ziliibiwa mpaka pale rais aliposema kuwa ziliibiwa na ni lazima wamuunge mkono kuhakikisha kuwa pesa hizo zitarudishwa.

anasema kuwa kuna watu wanasema kuwa kuna watu wanapayuka ,na hata wakipayuka ni haki yao na hata kama Microfone zikipasuka spika ataweka nyingine .
Asema kuwa kama wengine wanaongea kwa upole ,waseme maneno ya busara na yawaingie mafisadi mpaka rohoni mwao.

Asema kuwa kuna wabunge wanathubutu kuwatetea mafisadi ,hii ni aibu.

Asema kuwa nchi hii sio masikini na kama waarabu na mafuta yao basi sisi na madini yetu na hao wazungu wanaokuja hapa hawaji kutufanyia kazi,ila wanafanya kazi zao.

Asema kuwa hakuna usimamizi wa Tanzanite kwani hakuna anayehakikisha kuwa zinapatikana kiasi gani.

Alitembelea migodi ya Mererani na kukuta kuwa watanzania wanateseka sana kwani hata wakati wa kuchambua Tanzanite mikono yao inakuwa imefungwa na hata kama wakiwashwa hawawezi hata kujikuna .

Ataka ripoti ya tume ya Jenerali Mboma bungeni kuhusu kutatua mgogoro wa Kitalu B na C.

Amtaka waziri mkuu kupiga marufuku ununuzi wa fenicha kutoka nje ya nchi kwani hapa kwetu hatuna tatizo la mbao na hivyo akifanya hivy serikali itawekeza nchini kwani ndio wanunuzi wakubwa wa fenicha.

anaendelea kusema kuwa madukani kuna bidhaa feki nyingi sana asema kuwa waziri mkuu anatakiwa kulitupia macho.

Ununuzi wa magari ya serikali lazima yawe yananunuliwa kwenye pull na sio kila mmoja kujinunulia la kwake .
 
Ameonyesha kuwa kumbe anajiamini na anaweza kusema ukweli hata kama ataonekana mbaya.

Pili Mbunge wa Nkasi Poniano Nyami amesema kuwa ataleta hoja binafsi Bungeni kama serikali haitatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na SPM mgololo -kwa wale waliosoma hoja ya Dr.Slaa mtakumbuka hili la SPM.

lets wait another man is coming in front.........
 
Tunaomba Wabunge wenye uchungu na nchi yetu na wenye kuwahurumia wananchi wanaoteseka, waendelee kusimama kuwatetea wapiga kura wao ili nasi tuendelee kuwahesabu.....
 
Akumbushia ahadi za mwana TANU.
Asema kuwa rushwa ni adui wa haki, asema kuwa ahadi zile ni muhimu na kila mbunge ameapa kuzilinda .

Asema wabunge wawe mstari wa mbele kupiga vita Ufisadi.

asema kuwa watanzania hawakuamini kuwa pesa za EPA ziliibiwa mpaka pale rais aliposema kuwa ziliibiwa na ni lazima wamuunge mkono kuhakikisha kuwa pesa hizo zitarudishwa.

anasema kuwa kuna watu wanasema kuwa kuna watu wanapayuka ,na hata wakipayuka ni haki yao na hata kama Microfone zikipasuka spika ataweka nyingine .
Asema kuwa kama wengine wanaongea kwa upole ,waseme maneno ya busara na yawaingie mafisadi mpaka rohoni mwao.

Asema kuwa kuna wabunge wanathubutu kuwatetea mafisadi ,hii ni aibu.

Asema kuwa nchi hii sio masikini na kama waarabu na mafuta yao basi sisi na madini yetu na hao wazungu wanaokuja hapa hawaji kutufanyia kazi,ila wanafanya kazi zao.

Asema kuwa hakuna usimamizi wa Tanzanite kwani hakuna anayehakikisha kuwa zinapatikana kiasi gani.

Alitembelea migodi ya Mererani na kukuta kuwa watanzania wanateseka sana kwani hata wakati wa kuchambua Tanzanite mikono yao inakuwa imefungwa na hata kama wakiwashwa hawawezi hata kujikuna .

Ataka ripoti ya tume ya Jenerali Mboma bungeni kuhusu kutatua mgogoro wa Kitalu B na C.

Amtaka waziri mkuu kupiga marufuku ununuzi wa fenicha kutoka nje ya nchi kwani hapa kwetu hatuna tatizo la mbao na hivyo akifanya hivy serikali itawekeza nchini kwani ndio wanunuzi wakubwa wa fenicha.

anaendelea kusema kuwa madukani kuna bidhaa feki nyingi sana asema kuwa waziri mkuu anatakiwa kulitupia macho.

Ununuzi wa magari ya serikali lazima yawe yananunuliwa kwenye pull na sio kila mmoja kujinunulia la kwake .

Safi sana hii watetezi wa mafisadi na mafisadi wanataka kuwashinda watetezi wa maslahi ya Watanzania lakini nao hawakubali kushindwa wakiendelea hivi wanaweza kushinda na hatimaye mafisadi watafute upenyo wa kutokea. Sasa tusubiri nani ataamua kumshambulia Kimaro toka kundi la mafisadi. Hongera sana Kimaro endelea na msimamo wako huo huo.
 
mwaka huu bungeni kumoto

huenda sasa watu wakaanza kuogopa kugombea ubunge.

ilikuwa ishaanza kuhesabika ubunge ni kula tu sasa kazi ipo
 
Kuna uwezekano wa watu kupungua uzito bila kufanya "dieting".
 
................Amtaka waziri mkuu kupiga marufuku ununuzi wa fenicha kutoka nje ya nchi kwani hapa kwetu hatuna tatizo la mbao na hivyo akifanya hivy serikali itawekeza nchini kwani ndio wanunuzi wakubwa wa fenicha................

Mh Kimaro hongera kwa mengine uliyoyazungumza/uliyoyasema...........isipokuwa kwa hilo hapo juu sikubaliani nawe ktk ulimwengu wetu wa sasa "free market" wa EPA i.e Economic Partnership Agreement na masoko mengine ambayo Tanzania ni mwanachama...........Jambo la msingi ndugu Kimaro ungeiomba Serikali itoe incentives + subsidy kwa wakulima wetu..............na hili litawezekana pale Serikali itakapoamua kudhibiti UFISADI kwa nguvu zote.........

.....kuna njia nyingi tu zingine kwa ajili ya kupambana na tatizo la bidhaa kutoka nje........hiyo itahitaji mada yake........

.......otherwise...and once again hongera kwa kusema wazi
 
hongera kwa kuweza kuongea maneno kama hayo ndani ya bunge ilihali ni mbunge wa ccm.
wananchi tunaomba yasiwe maneno matupu, uhakikishe na vitendo pia vinafuatia
 
Hongera Kimaro. Ulianzia kwa BWM na sasa unakandamiza huku? Endela bwana huu ni mwaka wa kupambana na mafisadi mpaka kieleweke. Ile spirit uliyotoka nayo huku upinzani iendeleze huko huko chama cha mafisadi Tanzania.
 
Mwaka mgumu sana huu kwa waanafiki, maana mpaka hili bunge liishe ni ugonjw wa moyo tu saaafi sana Kimaro tulijua kuwa yanakuja na bado ndio kwanza yameanza!
 
Back
Top Bottom