Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Asante sana mpita njia kwa post hii.
Kwa Dr. Slaa, kwa mara nyingine tena umeonyesha usivyoogopa kusema ukweli.
Kwa kuwa kuna wasiwasi kuwa hotuba hii haikutolewa live, waTZ wengi watakuwa wameikosa. Ni vyema basi kambi ya upinzani ikaichapisha na kuisambaza. Mimi kwa uwezo wangu mdogo, nitatoa copy mbili niwape wananchi ili wasome kwa kupokezana huko vijijini.
Mwisho nawaasa wabunge wa CCM, suala hili wasilichukue kisiasa ati kwa kuwa limesemwa na mpinzani. Huku nje ya Bunge watu wameamka kwelikweli, mbunge asije kujikuta anaenda jimboni kwake anasulubiwa kwa alivyotetea ufisadi Bungeni.
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA NA WASOMI WAACHE WOGA.
 
hivi hili bunge litaisha kweli kabla hatujampata hata fisadi mmoja?

Subiri kesho utakia wanakaa kama kamati ya chama na JK yuko Dodoma kusawazisha mambo. Baada ya hapo mchezo uko palepale!!! VIVA Dr. SLAAA VIVA
 
Keep it up doctor I will have to spare sometimes for the Speech and get to read it properly.

Mungu twakuomba chipusha akina Slaa wengine maradufu apa Tanzania
 
kuna kipi cha kukeep up? huyu ni mamluki tu anatumiwa kwa manufaa ya watu wengine
 
sasa nainakili kwenye flash, tukutane kesho, hakuna kulala, na hao waliozima tv tutaonana watueleze kama waliishiwa betri au...
 
Hata wakikaa kikao cha dhararu haisaidii maana mwanaume ametoa dataz tupu..ni ile stuff inayoitwa concentrated.
Hata huyo PM atajibu nini sasa hapo maana ni cheche tupu. Kila point ni moto mkali..
Kama mchangiaji alivyosema hapo juu zinahitajika select committe zaidi ya 10 ili kutoa majibu!!
 
Dr eheeee Dr Slaa. Wewe ni brave kweli. Haya mengine yanazidi kuongezeka ati. Nchi hii tumeshaiuza na pesa ziko mikononi mwao. Warudishe ndiyo salama yao.
 
Subiri kesho utakia wanakaa kama kamati ya chama na JK yuko Dodoma kusawazisha mambo. Baada ya hapo mchezo uko palepale!!! VIVA Dr. SLAAA VIVA

Walishakaa hicho kikao cha kamati ya chama leo, sijui wamezungumza nini huko, nendelea kufukunyua, nikizinyaka data zao, zitafika hapa kwa kasi ya ajabu
 
Hata wakikaa kikao cha dhararu haisaidii maana mwanaume ametoa dataz tupu..ni ile stuff inayoitwa concentrated.
Hata huyo PM atajibu nini sasa hapo maana ni cheche tupu. Kila point ni moto mkali..
Kama mchangiaji alivyosema hapo juu zinahitajika select committe zaidi ya 10 ili kutoa majibu!!

Kweli PM atakuwa na wakati mgumu kujibu, labda na yeye aanze kuingiza politics lakini kama atafanya hivyo atakuwa anajishushia hadhi yake.
Lakini kwa upande mwingine serikali imejitakia haya matatizo yenyewe. Hoja nyingi zilizotolewa na Dr Slaa zilishazungumzwa na media kwa muda mrefu sana, serikali ikaweka pamba masikioni na kujifanya haisikii, hivyo haikujibu kitu. Sasa yameshaingia kwenye official channels, sijui watafanyaje!
 
Baada ya kusoma kwa utulivu shule yote ya Dr. Slaa, najiridhisha kuwa hakuna majibu yatakayotoka hapo. Yani nimeumia, mfano mdogo ni issue ya kubinafsisha Mgololo. Hivi kweli hawa jamaa ni watanzania. Wanafanya haya kutuona raia ni wajinga ama wanapata wapi huu ujasiri. Yani hapa nina hasira hata siwezi endelea tena na kazi....
 
Hotuba nzuri ni kweli watanzania hawajaisikia na kuiona leo live?sasa ujumbe utawafikiaje?maana some time magazeti hayaandiki kila kitu!SASA NI MWISHO WA MAFISADI KATIKA NCHI YETU!
 
Mh Dr. Slaa na Mh. Rais JK NAWAPONGEZA sana kutufikisha hapa tulipo.

Dr Slaa(k/upinzani) nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuyasema bila ya woga yote mliyoyataka muyaseme kama kambi ya upinzani. mungu awazidishieni maisha naamini hipo siku mtanifikisha mtanzania mie mahali ambapo napenda niwe.

Mh. Rais JK shukrani zangu zangu kubwa sana kwako kwa kuruhusu hali kuwa kama ilivyokuwa sasa,maana bila ya wewe sina fikirii kwamba mtanzania kama mie ningepata kuyajua haya, kwanza yani hata siamini,kweli Dr Slaa kanyanyuka na kutoa hotuba yote hii bungeni, aina hii ya ruksa ninaziona kwako tu,sikuziona hata kwa mwenye jina lake la ruksa. kwahilo unastaili HONGERA toka kwangu!

mungu tubariki Watanzania
 
Hongera Dk Slaa,sasa hivi tunataka wabunge wote waige mfano kwa Dk maana yeye anafanya kazi ipasavyo,mambo aliyo eleza kwenye ile hotuba yana tia hasira maana wahusika wenyewe kila siku wanaishia kusafishana tu badala ya kujibu tuhuma au kuchukua hatua kali kwa wezi na mafisadi
 
Inatia hasira sana, sishangai JMushi kuhimiza watu waingie msituni....probably it's a better and quicker solution. Com' on TZ!
 
Inatia hasira sana, sishangai JMushi kuhimiza watu waingie msituni....probably it's a better and quicker solution. Com' on TZ!

Huko msituni jmushi mwenyewe ameanza kupaogopa na sasa ameanza kuwakana wapinzani wenzake kuanzia zitto hadi slaa, msituni kunataka moyo hasa ukichukulia uwezo wa vijana wetu wa JWTZ.
 
Huko msituni jmushi mwenyewe ameanza kupaogopa na sasa ameanza kuwakana wapinzani wenzake kuanzia zitto hadi slaa, msituni kunataka moyo hasa ukichukulia uwezo wa vijana wetu wa JWTZ.

Wakiongozwa na Masaka. Msijadili tena hili ndugu zangu, mafisadi Tanzania ni wengi yanahitaji moyo.

Nafikiri hili ndilo litatukwamisha katika kufikia suluhisho. INawezekana ukimugusa kiongozi yeyote aliyeko serikalini utakuta ana kasoro.

Hivyo ndio maana bado baadhi ya watu tuna wasi wasi na watawala wetu kama wanaweza kutuondolea matatizo tuliyo nayo.

Tunajitahidi saaaaaaaaaaaaaana kuvumilia tutaendelea kuvumilia.

Kama hatutachukua hatua za haraka mafisadi mwisho wa siku wataanza kutuuza sisi watanzania tukiwa hai.

Hii ripoti imetuonyesha mengi.
 
BRAVO kambi ya upinzani Bungeni!!

Wakuu, naomba kama kuna mwana JF anayefahamu tofauti kati ya EPA na CIS (COMMODITY IMPORT SUPPORT) anieleweshe. Hotuba ya Mh. Slaa imeelezea jambo zito kuhusu CIS lakini mimi sijaelewa tofauti au uhusiano kati yake na EPA.
 
CIS hawana uhusiano na EPA .

Hizi ni fedha nyingine za wizi uliofanyika miaka ya tisini na hivyo hapa ni issue ya tofauti na EPA.
Nitaweka bandiko la CIS muda ujao then fuatilia kwa makini.
 
Back
Top Bottom