Nimeona matangazo ya ajira ya uhamiaji kuwa wanahitaji kidato cha 4 waliopata divishen 4 kuanzia pointi 28 mpaka 31 nikajiuliza sana.
Hivi taifa hili akili huwa tunazipeleka wapi? kwa nini uwe specific kutoa upendeleo kwa waliofeli? unaipeleka wapi jamii yetu kwa upendeleo wa aina hiyo?
Tangazo hilo nimeliona wizara ya mambo ya ndani upande wa uhamiaji.
Lakini kwa kumbukumbu zangu wizara hii huwa inaibuka na mambo ya ajabu ajabu tu, nakumbuka mwenyekiti wa parole ndugu Augustine Mrema naye aliwahi kuomba ujenzi wa reli SGR watumike wafungwa. Mimi nilimshangaa Mrema, mtu ambaye aliwahi kugombea Urais wa nchi hii unawaza vile? Kwamba wakati una vijana wengi wako mitaani hawana ajira unatoa kipaumbele kwa wafungwa kwenye ajira maana yake ni kuwaambia vijana wakafanye uhalifu wafungwe ndipo wapate ajira.
Ndiyo maana yake maana kama unawanyima vijana walioko mtaani ajira na unatoa jira kwa wafungwa unakuwa unapeleka ujumbe kwa vijana kuwa wakawe waarifu ndiyo wapate kazi na uhalifu utaongezeka maana vijana waliokata tamaa kwa kukosa ajira ni wengi na ukiwaonyesha wafungwa wanapewa kipaumbele watafuta kufungwa ili kupata ajira.
Tukirudi kwenye mada yetu ya kutoa kipaumbele kwa waliofeli.
Wapo wachache wanaodai ukimuajiri aliyefaulu anafanya kazi miaka michache na kutaka kwenda kusoma. ninasema wapuuzi wachache tena ambao hatuwezi kuwasikiliza tunapotaka kufanya maendeleo katika nchi hii.
Tunalo tatizo kubwa sana la ajira katika nchi hii kwa kuwa na vyuo vingi na shule nyingi zikizalisha wahitimu kila mwaka na wengi wanakosa ajira na kuishia kufanya shughuli za kipuuzi mitaani. watu hawa wanaweza kuajirika popote na wakakaa makazini kwa masharti ya mwajiri.
Mbona kuna watumishi wameajiriwa na kukaa kazini miaka zaidi ya 5 bila kupanda vyeo wala mishahara na humu kuna watu walikuwa na elimu kubwa lakini wakawa wanafanya kazi za chini.
Nina ndugu yangu amesoma ana masters ya business admnistration na kwa sasa anafanya kazi ya mtendaji wa kata
Halafu kuna mpuuzi mmoja sehemu anasema wasomi ukiwaajiri hawafanyi kazi hivyo tuajiri waliofeli??????
Hawa hawatujengei taifa bali kulibomoa