- Thread starter
- #81
Kuna vichwa havitakiwi kupewa nafasi ya kuamua kwa ajili ya taifa.Chuki ni mbaya acha....mnalilia ajira zikitolewa mnavimba mpaka mnataka kupasuka...kama ajira zinawahusu four div 28-31 wewe si usubiri zikitoka za 1&2 ukaombe mkuu.
Halafu hao necta wanapopanga madaraja ya ufaulu hawajawahi kusema kwamba div four ni failure acha kupotosha umma,unaweza kufaulu sana lakini ukafeli katika utendaji wa kazi.
Wameamua kutoa ajira kwa form 4 huku wakijua nyie wasomi mpo cha msingi subiri zikitoka zinazowafaa wasomi wetu.
unapotoa kipaumbele cha ajira kwa div 4 point 28 mpaka 31 na ukawaacha kuanzia pointi 27 kushuka chini na wengi wako mtaani hawana ajira unapeleka taarifa gani katika jamii kuwa kusoma sana hakuna maana? kwamba kufaulu siyo justification ya utendaji sasa kufeli ndiyo justification?
kwa nini wasiseme tunaajiri kidato cha nne na wale wa kidato cha nne wote walioko mtaani wajitokeje kugombania na wao wawachambue kulinganisha sifa mbalimbali ikiwemo elimu, lakini hawa wamekwisha wabagua wenye ufaulu mzuri kwa kuwaonyesha hawana sifa. kama mtu ana div 4 ya pointi 26 au 27 hana sifa.
mimi sielewi kama mnajua mnachokitetea au wale wenye maslahi na hili?