Kusudi la kuwepo duniani ni lipi?

Kusudi la kuwepo duniani ni lipi?

Sababu ya wewe kuwepo duniani ni kwamba wazazi wako wamekutana wakatunga mimba yajo, ukazaliwa.

Hiyo ndiyo sababu.
Kabla ya binadamu kuwepo duniani, ni viumbe vipi vilikuwepo kabla?
 
Umeuliza swali zuri sana.

Ukichambua hili swali umelipata baada ya kugundua kua vitu kama mali na vyeo vyote ni vinginevyo, na matokeo yake umeona ndani na kina cha kiini cha maisha.

Lengo la kuja duniani, ni mwanadamu kujipa uzoefu wa nyama au kuishi maisha katika mwili/vessel.

Binaadamu ana miili mitatu, mwili wa nje"physical body", mwili wa akili "mind", na mwili wa roho "etheric au astral body" sasa asilimia kubwa ya wwatu wengi tunaishi katika mwili wa nyama na akili, miili ambayo ndio inatutawala, na kuendeshwa na nguvu za chini zaidi kama tamaa, wivu, ubinafsi n.k

Vitabu vya dini vinasema Mungu alimuumba mwanadamu katika mfano wake, hii inamaanisha binaadamu ni reflection ya Mungu, hivyo binaadamu = Mungu, lakini binaadamu akijiita Mungu itakua sio sawa maana anaingia katika mtego wa EGO au SELF, na kuishi katika hali ya uMimi, huu ni mtego ambao hupelekea mtu kujiona ni bora zaidi kuliko wengine, na hivyo kuharibu kabisa lengo la uwepo wa mwanadamu.

Unazaliwa ukiwa ni kiumbe tu, Tunakuita mwanadamu, ila kuanzia unapozaliwa jamii inaanza kukupangia kwa kukupa jina, na kuoneshwa ndugu uliowakuta, utaingizwa katika mifumo ambayo huwezi kuchoropoka, mifumo kama dini, elimu n.k ni mifumo ambayo ipo kwa ajili ya kukuweka kama MSUKULE i.e kutumikia wengine, na kusahau lengo lako kuu la kuwepo hapa duniani ambalo ni kuishi kwa furaha, Maisha ya mbinguni au peponi ni symbolism ya maisha ya kujitambua kiroho na lengo lako hapa duniani. Na kuishi motoni ni kuishi katika hali ya uoga, kukinzana na sheria za ulimwengu, kuendekeza tamaa, wivu vinavyopelekea kukosa furaha na matokeo yake unaishi katika hali ya uhaba.

Katika ulimwengu ambao wewe muandika mada si lolote na si chochote maana yake wewe ndio alpha, mwanzo na omega mwisho, kinachoamua wewe ni mwanzo na ndio mwisho ni uwezo wako wa kukataa mifumo iliyoanzishwa isikutawale mwili wako wa akili "Mind", unapofanikiwa hili mwili unajijengea mazingira ya miili yako yote mitatu kua aligned au kusimama kwa umoja na kufanya kazi pamoja "UTATU MTAKATIFU"

Sasa ili kufikia hiyo hatua, ni lazima uanze kuvua mavazi yote ya kiimani, itikadi na "identity" yote kwa ujumla na ufahamu wako uwe kama mtoto tena, sio kusahau bali kukumbuka kua wewe sio chochote katika ulimwengu huu, na ukishatambua hilo maana yake hata yale mambo mazuri unayofikiria kufanya na unashindwa hakutakua na kizuizi cha kuyafanya sababu dhana zote za kuonekanaje hazitakuwepo tena n.k na hii itapelekea wewe kuishi kwa furaha na uhuru mpana bila kusumbuana na wengine kabisa.

Vitu kama meditation lengo sio kwenda popote, lengo ni kujipa utulivu mkubwa wa kuona kua haya maisha tunaishi kwa kuyaigiza ila haipaswi kulazimisha kuvaa vazi la igizo, Kujipa utulivu na kutambua kua matatizo tunayoyavaa sio halisi, kujipa utulivu kiasi unaanza kuuliza haya maswali, Katika dunia ya leo watu wengi wanaogopa utulivu sababu hawataki kujibu swali la uwepo wao hapa duniani. na kitu cha ajabu ni kua majibu ya maswali yote uliyonayo unayo wewe mwenyewe, unahitaji kukumbuka tu na Ulimwengu kila siku unakukumbusha ila bado haujajipa utulivu wa kutosha ukazingatia.

Dini hazijibu hili swali kwasababu dini zimejengwa kupitia "Experience za watu wengine", Yesu, muhammad, buddha, hermes trismegistus n.k ni watu ambao walifanya safari ya kiroho na kufikia hatua au hali ya uungu, hii ni hali unayoweza kuifikia na kila mtu ana uwezo huo huo.

Nimechoka kuandika.
 
Back
Top Bottom