Kusudi la kuwepo duniani ni lipi?

Kusudi la kuwepo duniani ni lipi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,939
Reaction score
61,732
Ni kuwepo duniani ili kutafuta hela, kushindana au ni kuwepo duniani ili tuishi?

Nimejaribu kufanya utafiti mdogo na kugundua kuwa, watu wengi wanatumia nguvu kubwa ya kutafuta hela, vyeo, kushindana ukubwa, wingi wa mali n.k; sasa nikawa najiuliza hawa kweli wanajua kusudi la kuwepo duniani?

Mimi nipo zangu hapa kijijini nimejilalia kwenye kitanda changu cha ngozi ya fisi, huku nikisikiliza milio mbalimbali ya ndege pamoja na kutukuza sifa na uumbaji wa Mungu.

Kwa mazingira haya naona kabisa, mimi ninaishi.

Je wewe, unafikiri kusudi la uwepo wako hapa duniani ni kufanya unacho kifanya?​
 
Kusudi la kuwepo duniani ni moja ya maswali makubwa na ya kale zaidi katika historia ya mwanadamu. Jibu la swali hili halina mwelekeo mmoja, bali limegawanyika katika mitazamo mikuu minne: Kiroho/Kudini, Kifalsafa, Kibaolojia, na Kisaikolojia.
 
Mtazamo wa Kiroho na Kidini (Spiritual Perspective)Kwa watu wengi wenye imani, kusudi la maisha linatoka kwa Muumba (Mungu).

Kumwabudu na Kumtukuza Mungu: Katika dini kuu (kama Ukristo na Uislamu), mwanadamu yupo duniani ili amjue Mungu, amwabudu, na kuishi kwa kufuata maelekezo yake.Kuwahudumia Wengine (Upendo):

Dini zote zinasisitiza upendo, kufanya matendo mema, na kuwasaidia wasiojiweza kama sehemu ya kukamilisha ibada.

Maandalizi ya Maisha ya Baadaye: Dunia inachukuliwa kama shule au daraja la mpito kuelekea maisha ya milele (Ahera au Peponi).
 
Hakuna kusudio lolote, ndio maana watu hufa na husahaulika. Yaani kabla ya uwepo wa binadamu dunia ilikuwepo na hata baada ya kuangamia kwetu dunia itaendelea kuwepo. Hiyo ni nature tu.
 
Ni kuwepo duniani ili kutafuta hela, kushindana au ni kuwepo duniani ili tuishi?

Nimejaribu kufanya utafiti mdogo na kugundua kuwa, watu wengi wanatumia nguvu kubwa ya kutafuta hela, vyeo, kushindana ukubwa, wingi wa mali n.k; sasa nikawa najiuliza hawa kweli wanajua kusudi la kuwepo duniani?

Mimi nipo zangu hapa kijijini nimejilalia kwenye kitanda changu cha ngozi ya fisi, huku nikisikiliza milio mbalimbali ya ndege pamoja na kutukuza sifa na uumbaji wa Mungu.

Kwa mazingira haya naona kabisa, mimi ninaishi.

Je wewe, unafikiri kusudi la uwepo wako hapa duniani ni kufanya unacho kifanya?​
Kwanza kabisa, kusudi ni nini?

Maana ya kusudi ni nini?
 
Katekisimu ya kanisa katoliki inatufundisha hivi.

Mungu katuleta duniani ili tufanye nini?

JIBU.
Mungu katuleta duniani ili,
1.Tumjue
2. Tumpende
3. Tumtumikie
4. Na mwisho tupate kufika kwake juu mbinguni.

Kila category hapo ina unyumbulifu wake mpana sana.

Mf. 1. Tumjue kupitia maandiko matakatifu, sala na ibada.

2.Tumpende Mungu kupitia kushika na kutenda yaliyo mema kwake yeye na Jirani zetu wakiwemo kobazi na atheist.

3. Tumtumikie kupitia kazi za mikono yetu katika vipaji na karama alizoweka ndani yetu.

4. Mwisho wa yote sifa na utukufu virudi kwake, ukiwemo ww mwanadamu. Mwanzo wetu ni yeye na mwisho wetu ni yeye pia.
 
Back
Top Bottom