Kushindwa hakuumizi sana, lakini kushindwa kunakotokana na usaliti inauma kuliko kitu chochote

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Kwema Wakuu!

Katika vita vya kisiasa kuna kushinda na kushindwa. Kushindwa ni sehemu ya ushindi ikiwa mlipigana kwa umoja na ushirikiano kwa pamoja kama jeshi imara.

Lakini kushindwa kunakotokana na usaliti sio tuu inaumiza bali pia inaua nafsi na roho.

Fikiria mtu uliyekuwa unamuamini na kumpa nafasi nyeti sana, ukamtunza na kumlinda kama mtu muhimu katika kikosi chako. Hakuwa chochote lakini wewe ukampandisha. Alipigwa mishale wewe ndiwe uliyekuwa kinga yake.

Kuna wakati ulivunja mpaka sheria za ufalme kwaajili yake ili kumlinda. Kuna wakati uligombana na wakubwa wenzako kwaajili yake.

Vita ikabadilika na sasa unaona adui yu mbioni kukushinda, unaamua tathmini na kuangalia kikosi chake kuona kama kuna chanzo cha Anguko ambacho ni msaliti. Kumbe umechelewa. Unakuja kugundua yule uliyemuamini ndiye ambaye amekugeuka, amekusaliti na ndiye chanzo cha Anguko lako. Ndiye chanzo cha wewe kusulubishwa, kuuawa na kuangikwa msalabani.

Usaliti unauma nyie acheni tuu.

Taikon mara nyingi hata ninapopambana na adui zangu. Nikimshinda kwa kupitia Watu wake wa karibu waliomsaliti ninawachukia zaidi waliomsaliti adui yangu kuliko adui yangu mwenyewe.

Hiyo ndio vita ya siasa. Rafiki ni adui aliyekaribu kama nilivyowahi kuandika.

Na kama walivyosema wakubwa wengine kuwa "Trust no one"

Nawatakia jumapili njema.
 
KUMANISHA NINI!!!

Rafiki yako uliyemuamini, uliyemsaidia kwa namna ambayo huwezi eleza, uliyemlinda kuliko yeyote, uliyeumia kwaajili yake. Katika vita yako anakuwa mlango wa adui kukumaliza. Kumbe alikuwa anaku-snitch mgongoni mwako.

Kisiasa umepasuka. Na hili hutokea mara kwa mara
 
Back
Top Bottom