Kupiga mswaki na kopo la kuogea

Kupiga mswaki na kopo la kuogea

Haya yote ni umasikini tu hakuna kingine, mtu hana sink chooni, hakuna maji ya uhakika kwamba mtu anaweza kuaccess maji hadi ndani, chumba kimoja bafu mtaa wa pili.

Nchi za kimaskini kuanzia serikali hadi watu wake.
 
kweli kabisa mkuu, hawa watumwa wa fikra kila kitu kwao ni uchafu tu. hivi usipotumia kopo la kuogea au ndoo ya kuogea unataka watumie nini? Alafu kila nyumba inautaratibu wake.
Huyo jamaa anasema hivyo badae chumvini anazama!!sasa yupi msafi?
 
Kuna haka katabia cha kutumia ndoo na kopo la kuogea kupigia mswaki

Kwa kweli hii tabia inanikwaza sana.
Mnaofanya hivyo badilikeni aisee. Hata kuweka mswaki juu ya mlango wa bafuni sio usafi kabisa
Tumieni vdumu acheni ubishi .na wale wanaopiga mswak nje tena kandokando ya njia huku wamevaa vbukta vfup na tumbo waz nao c ustaarab
 
SUALA HILI LA KAWAIDA SANA.
... Niliuliza hapo juu kuwa kama mtu uwwezi kuweka maji ya kupikia kwenye ndoo ya kuogea iweje uwe na ujasiri wa kuchota maji kwenye hiyo hiyo ndoo na kupigia mswaki
Hebu fuatana nami kidogo hapa.
....
Wewe ni mwanamke (mfano) utamaduni wako ni kuvaa sketi, gauni, browse nk sasa leo unanivalia suruali, shati zangu za kiume, T-shirt zangu nk, iweje uwe jasiri kuvaa nguo zangu wkt siyo sahihi?
...
USAFI:
Issue ya usafi wa matumizi ya vyombo kama kopo, mswaki, ndoo havina tatizo hata kidogo kutumika chooni.
>Ikiwa choo chako kinatumika na wawili/wa3 ambao mnatambuana na mmewekeana utaratibu mujarabu hakuna shida.
.....
Tatizo linakuja endapo umepanga choo/bafu ni kimoja tu so kila mtu na tabia yake, ila endapo unatumia mwenyewe haina shida.
 
Bila shaka bado unaishi na wazazi na hapo nyumban ni nyumba ya familia, yaan wazazi wakoShangaz,mjomba,mamdogo na watoto zao mabalehe na wali wote mmechanganyika humo

Au

Umepanga nyumba yenye wapangaji wenzako wengine wengi, na ni nyumba za uswahilili, chumba kimoja tuu, jiko, store ( kama ipo), ukumbi (sebule), choo na bafu mnatumia kwa pamoja sasa kuna ndoo moja ya chooni/bafuni na kopo moja

Kwa hali kama hii kweli sio ustaharabu kabisa, lkn mm nae tumia ndoo na kopo na mama yako mdogo tuu hapo tatizo lipo wapi?[emoji23]
Ni nyumba ya kupanga na kila mtu ana ndoo yake. Hii tabia nimeiona kwa wapangaji wenzangu na girls wawili ambao nimewahi kutoka nao
 
Badilika mkuu. Sio usafi kwa kweli. Na ndoo hiyo hiyo unatimia kufulia nguo za ndani na mswaki unaweka juu ya mlango wa bafuni.
Hiyo ndo inafuliwa pia inaoshwa mm hapo sijaona kama ni uchafu, labda kama mswaki kuuweka mlango wa bafuni hapo sawa ni uchafu
 
Kuna rafiki yangu mmoja alikua anaishi geto kisela kibachela yaani, yeye hatumii kopo la bafuni kupiga mswaki lakini anatumia kikombe ambacho hukitumia kuchota maji ya matumizi ya kawaida kwenye ndoo zingine. Nilipigwa na butwaa.

Lakini mtoa mada usipende kulalamika tu, come up with a solution.
huyu ni mimi Kabisa [emoji16][emoji16][emoji3]
 
Nyumba zetu za kupanga uswahilini mbona kawaida tu.
Dirisha la bafuni limejaa miswaki ya kila aina usipokuwa makini unajikuta umetumia mswaki wa baba Nyamizi jirani yako.!
Kuna wengine anaoga dawa za kienyeji kisha anasahau kikaratasi cha dawa dirisha la bafuni!
[emoji23][emoji28][emoji23] asee
 
Kwani ndoo ya kuogea na kopo ni vichafu??? Utaona vichafu endapo na wewe ni mchafu.
Mimi nikikupa ndoo yangu ya kuogea utakunywa na maji bila kujua. Na kopo la kuogea unanywea maji bila kujua ni kopo la kuogea.
Uchafu wako ndo unaokufanya uone ni uchafu ..[emoji23][emoji23] be smart
 
Kwani ndoo ya kuogea na kopo ni vichafu??? Utaona vichafu endapo na wewe ni mchafu.
Mimi nikikupa ndoo yangu ya kuogea utakunywa na maji bila kujua. Na kopo la kuogea unanywea maji bila kujua ni kopo la kuogea.
Uchafu wako ndo unaokufanya uone ni uchafu ..[emoji23][emoji23] be smart
Nakazia
 
Kwani ndoo ya kuogea na kopo ni vichafu??? Utaona vichafu endapo na wewe ni mchafu.
Mimi nikikupa ndoo yangu ya kuogea utakunywa na maji bila kujua. Na kopo la kuogea unanywea maji bila kujua ni kopo la kuogea.
Uchafu wako ndo unaokufanya uone ni uchafu ..[emoji23][emoji23] be smart
Unatumia choo cha aina gani? Una flash au ni cha kumwaga maji na ndoo? Hiyo ndoo unatumia kuogea tu au kwendea chooni na kufulia nguo za ndani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom