Nyie Wahudumu wa Mabaa na Makaunta

Nyie Wahudumu wa Mabaa na Makaunta

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
3,015
Reaction score
4,403
Kichwa cha Habari

Nyie Wahudumu wa Mabaa, Makaunta na Mahoteli

Ushamba, Utapeli na Upumbavu Wenu Ndio Unao piga Vita Biashara za Watu

Hivi nyie wahudumu wa mabaa, makaunta, na wafanyakazi wa mahotelini huwa mnamiliki akili timamu au kuna vitu vimeoza ndani ya vichwa zenu?

Mna tabia za kishamba, za hovyo na za kipumbavu ambazo hazivumiliki hata kidogo!

Unakuta poyoyo mmoja amekaa kaunta, mteja anafika anaulizia bei ya pombe kali au chakula. Chupa inayouzwa Tsh 20,000 kwa bei halali ya eneo hilo, muhudumu mjinga na mlafi anamwangalia mteja usoni, anapiga hesabu za kishamba halafu anatamka kwa kujiamini: "Hiyo ni 35,000!
Unazani umekuwa mjanja? Unajiona umepata cha juu, Mteja kwa kuwa ni mstaarabu na hataki shida analipa.

Lakini siku akirudi tena akamkuta muhudumu mwingine asiye na ugonjwa wa akili kama wako, anauliza bei ile ile anaambiwa ni Tsh 20,000!
Aibu ya mwaka! Utapeli wa kishamba na wa kijinga kabisa

Matokeo yake mteja anagundua alikutana na tapeli wa mtaani badala ya mfanyakazi, anakata mguu na haikanyagi tena hiyo sehemu. Na huu upuzi haupo bar peke yake, hadi jikoni mambo ni yale yale ya hovyo! Supu ya Tsh 3,000 mteja anatapeliwa kuuziwa Tsh 5,000, siku akirudi anakuta bei tofauti. Huu utahira na ulimbukeni mtaacha lini.

Hivi nyie wapuuzi mnaofanya uozo huu mnamfanyia nani ujanja, Mnafikiri mnamkomoa mteja au mnamwibia bosi? Hamjui kuwa huo uwizi wenu wa kijinga ndio unaua biashara za watu na kuwafilisi? Mtu amewekeza mabilioni yake kujenga eneo la maana, halafu limbukeni mmoja aliyetoka kijijini juzi na sanduku la bati anakuja kuua uwekezaji wote huo kwa tamaa za Tsh 5,000 na 10,000 za kijinga

Huu uwazi, ushamba, na ukosefu wa nidhamu umejaa mpaka kwenye mahoteli makubwa. Watu mmejaa tamaa za kijinga na ukosefu wa uaminifu uliopitiliza. Badala ya kulinda ajira zenu, mpo busy kupiga dili za kitoto ambazo hata hazibadili maisha yenu zaidi ya kuwanunulia sigara na vocha za buku buku

Biashara ikifa na mwenye eneo akafunga kufuli, nyie ndio wa kwanza kuanza kutangatanga mtaani kama mbwa waliokosa wenyewe mkilalamika maisha magumu.

Badilikeni, achaneni na utapeli wa kishamba, mnajiaibisha na mnaharibu biashara za watu waliowahurumia na kuwapa kazi.
 
Ndio maana nikienda kunywa bar nikinywa vile vifunimo hua nakusanya mfukoni hua siibiwi ovyo ovyo
 
Back
Top Bottom