Kupiga mswaki na kopo la kuogea

Kupiga mswaki na kopo la kuogea

Kuna haka katabia cha kutumia ndoo na kopo la kuogea kupigia mswaki

Kwa kweli hii tabia inanikwaza sana.
Mnaofanya hivyo badilikeni aisee. Hata kuweka mswaki juu ya mlango wa bafuni sio usafi kabisa
Sasa toa ushauri namna ya kufanya sio kulalamika tu.
Hoja ijitosheleze.

Tatizo ni nini?
Na kiutaratibu huwa inakuwaje?
Hitimisho.
 
Ni vema ukaintroduce huu ustarabu kwenu/kwako.
Wewe unataka tutumie jagi la maji ya kunywa?
Au unadhani kila nyumba ina sinki la kunawia/kuswakia??
Mambo mengine si ya kuyajadili hapa,just kumwambia mumeo/mkeo yatosha!!!))
kweli kabisa mkuu, hawa watumwa wa fikra kila kitu kwao ni uchafu tu. hivi usipotumia kopo la kuogea au ndoo ya kuogea unataka watumie nini? Alafu kila nyumba inautaratibu wake.
 
Nadhani busara ni kuwa na kopo lingine kwa ajili ya kupigia mswaki. Ndoo ya kuogea ambayo unaitumia pia chooni. Imagine unapomwaga chooni ni mara ngapi maji yanaruka na kurudi kwenye ndoo. Auunapoweka mswaki juu ya mlango wa bafu ni watu wangapi wameweka vyupi vyao hapo ulipoweka mswaki wako.
Kuna gharama gani kununua jagi kwa ajili ya kupigia mswaki?
 
kweli kabisa mkuu, hawa watumwa wa fikra kila kitu kwao ni uchafu tu. hivi usipotumia kopo la kuogea au ndoo ya kuogea unataka watumie nini? Alafu kila nyumba inautaratibu wake.
Hilo kopo/ndoo mnatumia wangapi kuogea, kuendea chooni na kufua vyupi alafu unaitumia kupigia mswaki.

Daah. Alafu mbaya zaidi kila mtu ana ustaarabu wake sasa
 
Kuna rafiki yangu mmoja alikua anaishi geto kisela kibachela yaani, yeye hatumii kopo la bafuni kupiga mswaki lakini anatumia kikombe ambacho hukitumia kuchota maji ya matumizi ya kawaida kwenye ndoo zingine. Nilipigwa na butwaa.

Lakini mtoa mada usipende kulalamika tu, come up with a solution.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom