Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Kwa wanafunzi mashuleni kuwe na mtaala wa kufundisha somo hili. Zamani kuna mada katika somo la Sayansi Kimu au maarifa ya nyumbani lilizungumzia misingi ya uchumi na faida za kuweka akiba.
Kwa wale wenye vyeti na hata stashahada za uchumi mnaweza kufundisha jumuia za kanisani I, msikitini au hata mtaani. Inasikitisha kuona raia wengi hawana tabia ya kujiwekea akiba hata katika kile kidogo wanachopata.
Mtaani wengi wanacheza vikoba, mfano tu kuna vikoba vya 2,000 kwa siku, 5,000 kwa wiki na vingine 20,000 kwa mwezi. Unakuta mama anaishi bila amani akiwaza Pa kupata 2,000 kila asubuhi. Wengine hujirahisisha kwa ngono zembe ili apate 2,000 ya leo na ya kesho hajui itatoka wapi. Hapo bado anadaiwa 5,000 kila Jumamosi.
Kutokana na vipaumbele kutofautiana wengi hawaoni hata faida ya vikoba, ni shida tu. Hela ya kikoba inapaswa itoke baada ya matumizi kama chakula na kodi ya nyumba kukamilika. Sasa unapotegemea mzunguko kulipia kodi na kununua chakula ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Elimu ya pesa ingeendana ba elimu ya uraia, wananchi wanapaswa kufahamu umuhimu wa serikali kukusanya kodi na ni nini wategemee kutoka serikalini kutokana na matumizi ya kodi yao.