KERO Elimu Bure ni nini? Je, ni sawa wazazi kuendelea kuchangishwa pesa za chakula, mpishi, usafi na mitihani ya kujipima?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna shule ya Msingi inaitwa Gulukakwalala iliyopo Ilala, kabla mtoto hajaingia darasani lazima atoe Tsh. 1,200 ambayo ni Tsh 1,000 ya chakula na Tsh 200 ya uji kila siku, ambapo kama huna hela hiyo mtoto hawezi kuingia darasani.

Sasa hivi wanasema kila mwezi mzazi atoe Tsh 2,000 ya mpishi na usafi na tsh. 1000 ya mtihani wa kujipima

Kwa hiyo kila mwezi lazima kulipa 24,000 + 1,000,+ 2,000= 27,000

Shule nyingine inayolipisha wazazi ni Maarifa ya G/Mboto. Pale pia mtoto asipokwenda na hela ya chakula ni fimbo.

Na kuna uthibitisho wa mama aliyekuwa akinieleza changamoto hizi na kutokutaka kujulikana kudai mtoto mtoto wake kucharazwa fimbo 6 kisa kwenda bila hela ya chakula na anasema hawataki mtoto kwenda na chakula chake mwenyewe.

Je, elimu bure hii tafsiri yake ni nini? Naomba tuone namna gani kuwasaidia hawa wazazi husasani wenye kipato cha chini dhidi ya hii michango.
 
Hela ya bando unayo ila kulipia mwanao chakula huna?
 
Malalamiko kama haya Huwa yanaonesha jinsi gani hatuwapendi watoto wetu, au jinsi gani uelewa wetu juu ya dhana na nia ya serikari kutoa elimu bila mzazi kutoa ada inavyopotoshwa. Mtoto wwako mwenyewe, chakula ukichanga anakula yeye, halafu unalalamika? Hii ni ajabu. Duniani hapa hakuna elimu ya Bure😳
 
Lengo la serikali kwa sasa ni watoto wale shuleni lakini kwa akili ya watanzania akiwemo huyu jamaa inaonesha ni jinsi gani hatuelewi mambo yanavyoenda
1. Mtoto ni wako mwenyewe ila unaona karaha kumlipia chakula ale eti elimu bure. Kama ungekuja na sababu kuwa wanachanga hela afu walimu ndio wanakula hapo tungekuelewa
Ninachojua mimi ni kwamba anakosoma mwanangu bado hawajaanza kuchangisha pesa ya chakula lakini kila siku nampa hela ya kula (kununua kwa wanaokuja kuuza shule) kwa akili ya mleta mada inaonekana hata mwanae huwa hampi hela ya kula
2.unaona tabu kuchangia 1000 ili mwanao afanye mitihani? Mbna hapo walimu wana dhamira njema kabsa la kukuza taaluma.
(Watu kama ninyi ni wale waliosoma ktk mazingira magumu na kwasababu ulisoma mazngira magumu unataka hata na watu wengine wote wasome kama wewe badilika budha)
 
Ili swala lipo kisasa mno...Kwani watoto wa wao wanakwambia Elimu ni Bure wapo private wanalipa Ada kubwa mno... Kwa mwaka unakuta mtoto analipa 1.8 millioni alafu mtoto wa mpiga kura yupo anasomea shule za Elimu Bure...na mzazi akiamia achangie mchango kidgo wa Chakula, Remidial ....in return mtoto wa shule hiyo ya kata au hizo shule za Elimu Bure anamaliza miaka yake 7 au 4 na matokeo ya ya Daraja F...alafu hao waliokuwa wanalalamikia michango wanaanza kulaumu serikali .
Hivyo Elimu Bure inatengeneza kizazi tawaliwa na kizazi tawala( PRIVATE SCHOOLS).
Hivi tuongee ukweli Kuna mtoto wa Mbunge au mtoto wa makuu ya Mashirika anasomea hizi shule za Elimu Bure?
 
Mingine ni miradi ya waalimu hii.

Unagombana na waalimu hapa bila kijua,mtoto hajapewa 1200 mzazi kakosa.anachapwa.
Kwa sasa ni afadhali mtoto asifikie shule kabisa,kuliko kufika bila hiyo hela.

Ccm wameacha masikini tuuane.
 
Kuna shule ya Msingi inaitwa Gulukakwalala iliyopo Ilala, kabla mtoto hajaingia darasani lazima atoe Tsh. 1,200 ambayo ni Tsh 1,000 ya chakula na Tsh 200 ya uji kila siku, ambapo kama huna hela hiyo mtoto hawezi kuingia darasani.

Sasa hivi wanasema kila mwezi mzazi atoe Tsh 2,000 ya mpishi na usafi na tsh. 1000 ya mtihani wa kujipima

Kwa hiyo kila mwezi lazima kulipa 24,000 + 1,000,+ 2,000= 27,000

Shule nyingine inayolipisha wazazi ni Maarifa ya G/Mboto. Pale pia mtoto asipokwenda na hela ya chakula ni fimbo.

Na kuna uthibitisho wa mama aliyekuwa akinieleza changamoto hizi na kutokutaka kujulikana kudai mtoto mtoto wake kucharazwa fimbo 6 kisa kwenda bila hela ya chakula na anasema hawataki mtoto kwenda na chakula chake mwenyewe.

Je, elimu bure hii tafsiri yake ni nini? Naomba tuone namna gani kuwasaidia hawa wazazi husasani wenye kipato cha chini dhidi ya hii michango.
Kabla hatujaenda mbali tuanzie hapa-:
-Wewe unayetaka serekali ifanye kila kitu unalipa kodi kiasi gani? ( Matumizi yako kwa mwezi + na kodi unayolipa direct kutoka kwenye shughuli zaki zinazokuingizia kipato)
 
Wazazi tuwapende watoto wetu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wakiwa shule wanapata chakula. Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
Wewe ni mwalimu?

Mtoa mada anauliza ni nini naana ya elimu bure?

Serikali ni wapumbaf kutoa kauli ya elimu bure, hawakuelewa requirememts za wanafunzi yakiwemo hayo mahitaji yanayoshadadiwa na walimu wa baadhi ya shule bila wazazi kupewa muongozo wa kufuata toka Wizara ya elimu?
 
Back
Top Bottom