Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,233
- 12,744
Argentina wamemchagua Javier Milei kuwa Rais wao mpya. Ni jamaa mwenye msimamo mkali wa kulia. Moja ya malengo yake ya kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na mfumuko wa bei ni kuiua pesa ya Argentina(Peso), kuvunja benki kuu na kuanzisha matumizi ya Dola ya Marekani kama pesa rasmi ya nchi. Jamaa ni msomi wa uchumi hivyo bila shaka anajua anachokifanya.
Ni nini faida na hasara za nchi kuamua kuanza kutumia dola ya Marekani kama pesa ya nchi?
Ni nini faida na hasara za nchi kuamua kuanza kutumia dola ya Marekani kama pesa ya nchi?