Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Mbali na hilo tatizo la kuzimwa midomo inaelekea kuna pia tatizo la uelewa mdogo miongoni mwa waandishi wa habari wanaotumwa kufuatilia matukio fulani fulani; kwa mfano kwa siku nzima jana watangazaji wa TBC walikuwa wakitangaza kwamba wanasubiri kikao cha NEC kiisha, hili watangaziwe sekretariati mpya.
Inavyoelekea kwao kutangaziwa wajumbe wa halmashauri kuu haikuwa muimu, na kweli wajumbe wa kamati hiyo mpya hawakupewa kipau mbele katika matangazo yao. Aidha hiyo jana TBC ilikuwa ikitangaza mara kwa mara orodha ya watu waliowahi kushika wadhifa wa katibu mkuu wa CCM.
Katika tangazo hilo ilikuwa inajengwa hisia ya kuwa cheo cha katibu mtendaji, kama mtendaji mkuu wa CCM alivyojulikana hapo mwanzo ni sawa na cheo cha katibu mkuu kilichobuniwa hapo baadaye, na kutwaliwa na marehsmu Kawawa kama katibu mkuu wa kwanza wa CCM.