Wakati tukielekea katika kumbukumbu ya kifo cha kipenzi cha watanzania wengi hayati Edward Moringe Sokoine naona mheshimiwa Lowasa yumo akimwelezea marehemu alivyokuwa
1. Kuna umuhimu wa Lowasa kuwemo? Hakuna viongozi wasafi wanaoweza kumsemea huyu mpendwa wetu?
2. Hilo tangazo nani analilipia? Kama ni serikali kwa nini atumie pesa ya walipa kodi kujisafisha?
Kwangu mi naona ni sawa na kuchanganya biskuti na matofali na kuweka ndani ya boksi.
Mbona Lowassa apewe nafasi ya kumsemea kiumbe wa watu ambaye hakuwahi kufikiria watanzania wanahitaji kuibiwa?
Kwanini TBC1 wanaonekana kumpa coverage kubwa Lowassa?

Nimefuatilia jinsi TBC1 ilivyofanya kazi ya kuripoti vikao vya CC na baadaye NEC Dodoma na kugundua kwamba bado TBC1 wanafanya kazi kwa maelekezo/ushabiki wa Lowassa.
Kwanza kwa Dodoma na Dar es Salaam matukio makubwa hurushwa moja kwa moja na zaidi kama yanamhusisha Rais ama tukio lenye mvuto kwa jamii. Kwa vikao vya Dodoma na baada ya NEC kuruhusu waandishi wa habari na TBC1 kurekodi badala ya kurusha live inatia shaka.
Pili baada ya kurekodi, inasikitisha sana sisi tuliokuwamo katika hiyo Press Conference tumeshangazwa na TBC kukatiza alipoishia Chiligati na kutomtoa kabisa Nape alipokua akiwataja moja kwa moja kina Lowassa, Rostam na Chenge.
TBC1 fanyeni kazi, Lowassa hasafishiki na habebeki na hata kama akifanikiwa kuwa kiongozi endeleeni na kazi bila kujali, na kama munamjali Rais ajaye (kama akipata) na kumwacha Rais aliyepo.
Tulidhani baada ya kuondoka Tido itakua yameisha maana Tido alimhoji Pinda na kumpa Lowassa nafasi ya kumalizia ili amfunike, lakini na sasa munaendelea kuonyesha kwamba munaandamwa na kivuli cha Lowassa. Fanyeni kazi acheni unazi wa aibu hasa kwa mafisadi.