SAM wa KILUNGU
Member
- Jan 22, 2011
- 52
- 13
Lowassa ni mbuge wa jimbo alilokuwa Sokoine, ni mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu, cheo alichokuwa nacho Sokoinne, ni mtu pia aliye kuwepo wakati wa Sokoinne...ni miongoni mwa watu wanaostahili kuwa katika kipindi hicho.Wakati tukielekea katika kumbukumbu ya kifo cha kipenzi cha watanzania wengi hayati Edward Moringe Sokoine naona mheshimiwa Lowasa yumo akimwelezea marehemu alivyokuwa
1. Kuna umuhimu wa Lowasa kuwemo? Hakuna viongozi wasafi wanaoweza kumsemea huyu mpendwa wetu?
2. Hilo tangazo nani analilipia? Kama ni serikali kwa nini atumie pesa ya walipa kodi kujisafisha?
Kwangu mi naona ni sawa na kuchanganya biskuti na matofali na kuweka ndani ya boksi.
Mbona Lowassa apewe nafasi ya kumsemea kiumbe wa watu ambaye hakuwahi kufikiria watanzania wanahitaji kuibiwa?
Kwanini TBC1 wanaonekana kumpa coverage kubwa Lowassa?
ASANTE