Kuna movie inayoitwa 'hornet' nimetoka kuicheki hapa karibuni, na pia niliona imerushwa kwenye channel ya maisha magic bongo ya dstv hapa juzi usiku ikiwa imewekewa script za kiswahili. Hii movie inaonekana imetolewa na serikali ya marekani na katika maelezo yake ya awali inaonekana ni confidential (yaani maudhui yaliyomo kwenye hiyo movie yalikuwa yamefanywa kama jambo la siri).
Katika hiyo movie kuna matukio ya watu kuvamiwa na vyombo na viumbe kutoka sayari za juu na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Nikiihusianisha hii movie na maono yangu ya huko nyuma naona kuelekea mwisho wa dunia kuna viumbe kutoka sayari za juu watavamia duniani na ndo itakuwa mwanzo wa kuanza kwa machafuko na ghasia kila mahali ambazo zitakuwa nje ya uthibiti wa mifumo ya kawaida ya binadamu na inawezekana kabisa watashirikiana na waabudu shetani wa hapa duniani (illuminants and the likes).
Hii pia imenifanya kujua kwamba kuna mipango timilifu ambayo inaratibiwa na ibilisi na mawakala zake kuelekea mwisho wa dunia.
Nakaribisha wajuvi na wale wanaoangalia haya mambo kwa jicho la kiroho kwa ajili ya michango yenu.