Salaam wanajukwa,
Ijumaaa hiyo kwa wale wenzangu na mimi ambao Magufuli hajatuathiri sana tukutane.
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Nimekua nikisoma story za watu nimekua nikishudia mwenyewe. Hata wewe unaesoma hapa na mpenzi wa jukwaa hili jaribu kupitia Thread za huku. Nyingi ni kuumizana, usaliti, kuzaa nje ya ndoa, kula mashemeji na mambo chungu nzima ya kuudhi na kuumiza.
Nimetafakari sana nikajiuliza kuna sababu gani mimi KUOA?
Nimekua nikiona rafiki zangu waliooa wakiwacheat wake zao, wadada rafiki zangu wakiwacheat waume zao marafiki zangu ambao hawajaoa wana wapenzi zaidi ya watatu na wanawapanga si mchezo.
Mimi mwenyewe nina wapenzi zaidi ya wawili na hawajuani na nikiwafatilia nao hao wapenzi wangu nao wana wapenzi wengine.
Binafsi nina mtoto nimezaa na mdada mmoja ila sijapanga kumuoa. Kila nikipata wazo la kuoa aisee nikikumbuka mambo ninayosoma na kushuhudia nakufa moyo sitamani kabisa ndoa.
Marafiki zangu karibia wote wameoa, wadogo zangu nao wanataka kuoa ila mimi bado najiuliza naoa kutafuta nini? Si niongeze mtoto mwingine na mwanamke mwingine halafu nilee tu watoto? Kwanini kuleta maumivu ndani ya nyumba?
BADO NAWAZA