stable-negro
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 509
- 347
Kama maziwa yanapatikana mitaani na nyama mabuchani, kuna haja gani ya kufuga ng'ombe???
dah!! huu msemo alikuwa anapenda sana kuutumia lecturer wetu Mr. Zera....nimejikuta nimemkumbuka ghafla
Kama maziwa yanapatikana mitaani na nyama mabuchani, kuna haja gani ya kufuga ng'ombe???
Mimi mwenyewe naona haina haja ya kuolewa as long as napata vyote ninavyovitaka bila kubanwa na mtu anayeitwa mume,Mkuu nitoe katoka mtizamo hasi unilete kwenye chanya, kwanini nioe?
Na miaka yakewe ni KE au ME?
Hawa vijana shida tuHumu duniani kuna kuumwa mara magonjwa mbali mbali, mara kuna ajali zinatokea kila siku, mara kuna kukosa hela sometimes, mara kuna kugombana na watu Saa ingine huna kosa, kuna kusingiziwa kesi Saa zingine polisi, mara kuna kukosa hela yaani tabu tupu!
Kuna marafiki zako wengi wamepitia hayo, wengine kuumwa, wengine kukosa hela, wengine ajali nk
Sasa niambie kuna faida gani wewe kuishi? Kwwnn usighaili kuishi ukajiua zako tu
Dada asante sana kwa Ushauri na mawazo yako. hata mie bado niko katika dillema. natamani sana kuoa lkn kila nikikumbuka au nikiona matendo mabaya wafanyinayo wanandoa hakika sitamani tena kuwaza kuoa, japo uwezo wa kutunza mke na watoto namshukuru Mungu amenijalia lkn sasa kuchukua uamzi aisee nashindwa kabisaMimi mwenyewe naona haina haja ya kuolewa as long as napata vyote ninavyovitaka bila kubanwa na mtu anayeitwa mume,
pia kuolewa inamaanisha lazima niwe najishusha kwa mume, niwe nakaa nyumbani kwa muda mwingi, na cu compromise uhuru wangu mwingi tu for the sake of ndoa,
nikaona ni ujinga, ila nikatafakari tena upya nikasema mume ndio anaweza kuwa rafiki yako wa muda mrefu hata kama aki cheat, ndio watu mtakuwa wote hadi uzeeni na ku share matunda ya malezi yenu, nikaona kuolewa ni bora kwa maslahi ya muda mrefu
Salaam wanajukwa,
Ijumaaa hiyo kwa wale wenzangu na mimi ambao Magufuli hajatuathiri sana tukutane.
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Nimekua nikisoma story za watu nimekua nikishudia mwenyewe. Hata wewe unaesoma hapa na mpenzi wa jukwaa hili jaribu kupitia Thread za huku. Nyingi ni kuumizana, usaliti, kuzaa nje ya ndoa, kula mashemeji na mambo chungu nzima ya kuudhi na kuumiza.
Nimetafakari sana nikajiuliza kuna sababu gani mimi KUOA?
Nimekua nikiona rafiki zangu waliooa wakiwacheat wake zao, wadada rafiki zangu wakiwacheat waume zao marafiki zangu ambao hawajaoa wana wapenzi zaidi ya watatu na wanawapanga si mchezo.
Mimi mwenyewe nina wapenzi zaidi ya wawili na hawajuani na nikiwafatilia nao hao wapenzi wangu nao wana wapenzi wengine.
Binafsi nina mtoto nimezaa na mdada mmoja ila sijapanga kumuoa. Kila nikipata wazo la kuoa aisee nikikumbuka mambo ninayosoma na kushuhudia nakufa moyo sitamani kabisa ndoa.
Marafiki zangu karibia wote wameoa, wadogo zangu nao wanataka kuoa ila mimi bado najiuliza naoa kutafuta nini? Si niongeze mtoto mwingine na mwanamke mwingine halafu nilee tu watoto? Kwanini kuleta maumivu ndani ya nyumba?
BADO NAWAZA
Mkuu mimi sijui kiswahili saaana. ila nahisi kama umenielewa kabisa nini namaanisha, na mie pia nadhani nimekuelewa ulivyosema,Mimi naona unajielewa sana na uko mhalisia na unaishi kwenye ulimwengu wa walimwengu.
Siyo kila mtu anafaa kuwepo kwenye ndoa.
Mkuu mimi sijui kiswahili saaana. ila nahisi kama umenielewa kabisa nini namaanisha, na mie pia nadhani nimekuelewa ulivyosema,
ahsante sana. haya Mambo ni magumu saaana kaka. ndoa zimekua ni kama michezo ya kuigiza hivi.
ndoa inafungwa leo kesho kutwa mwenye ndoa anafumaniwa. ni hatari sana
yeesNaam kaka, mie nimekupata vyema kabisa na nimeupenda mchukuo wako wa mambo.
Ndoa nyingi mno ni maigizo matupu na huu ujio wa simu za mkononi na mitandao ya kijamii ndo umerahisisha kuifanya hiyo taasisi kukosa maana.
Mkuu Ngabu hizi ndoa hapana. wewe jaribu hata kusoma kwenye hili jukwaa tu, angalia kwa washikaji zako.
angalia kwa viongozi wa dini.
rudi viongozi wa kiserikali.
naichukia ndoa
Acha kusaliti nawe hutasalitiwa maana,mungu hukupa yule wa kufanana nae upo hapo
Utani au dharau juu ya neon MUNGU ningekusihi uache,MUNGU sio Magufuli hata umfanyie mzaha na mjadala ndani ya Jf,ukiona umemzoea sana endelea mkuu.Hahahaa kaazi kweli kweli!
Hivi kweli hadi karne hii watu bado mnaamini huo upuuzi wa mungu hivi mungi vile?