Kuna nini nyuma ujenzi wa bwawa la Nyerere la kufua umeme

Muandishi ni PhD kweli?? Hivi anajua maana ya bio diversity kweli? Hajui kwamba binadamu pia inategemea species tofauti ili tuweze kusurvive? Anafahamu mentallity ya binadamu ni bora kuliko ndege na wadudu ndio ilisababisha moja ya janga kubwa katika historia ya dunia?


Inaweza kuwapo sababu bora zaidi za kupromote mradi huu ila sio kwa sababu eti vipepeo sio bora kuliko binadamu, very illogical argument.
Nakubaliana na wewe kuwa muandishi na hata baadhi yao humu wanadhania labda hii dunia ni kwa ajili ya binadamu tu. Hivi Mwenyezi Mungu kama alitaka binadamu tu wawepo hapa asingeumba na hao viumbe wengine. Kila kiumbe kina umuhimu wake katika dunia hii yetu, kwa hivyo tusijifanye eti sisi ni wajuaji wa kuamua kiumbe gani kiondolewe na kipi kibaki.

Muandishi kwa kweli anahitaji kupata elimu kubwa kuhusu bioanuwai.
 
Hoja yako ina uzito kuwa uhai na ustawi wa binadamu unategemeana na hali ya "bio-diversity". Lakini, kwa jinsi Mungu (kama unaamini yupo) alivyomuumba binadamu kutawala dunia (nukuu imeambatanishwa), binadamu huyo ana uwezo wa kuweka mazingira rafiki kwa hao viumbe. Hivyo basi, "argument" yake inabaki kuwa "logicaL".

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Kutawala sio kuwaharibia makazi yao, hta Biblia unayonakili kuna mahali inakataza ukataji wa miti inayosupport maisha yetu.

Deuteronomy 20:19
When you besiege a city for a long time, making war against it in order to take it, you shall not destroy its trees by wielding an axe against them. You may eat from them, but you shall not cut them down. Are the trees in the field human, that they should be besieged by you?

So kama hoja ni Biblia then mpka hapo mmeshatenda dhambi.

Anyway hoja yangu haikua kidini bali kibaiolojia kwamba huwezi toa argument kwamba Vipepeo au miti haina thamani kuliko binadamu unless hatujui jinsi food chain inavyofanya kazi.
 
Construction of the dam began on Nov. 6, 1956, and was completed in 1959
Shukrani mkuu kwa facts ulizomwaga. Maana kuna mentality kwamba kila failure ya waafrika ni hujuma ya wazungu. Sasa cha kujiuliza hizo Hydro power walizojenga kabla ya uhuru ilikua kwa ajili ya nani?
 
Huyu waziri wa Twita awe na huruma hata kidogo, anataka kutuletea umeme wa solar na Upepo ilimradi tu anufaishe tumbo lake.
 
Nile ya Jinja ilijengwa

Grand Renaissance Dam ya Ethiopia imejengwa, tatizo ni misri wanahofia maji yanayotoka blue nile yatakua diverted kushibisha mradi so hapo hakuna beberu ila ni internal dispute tu.

Mbona Tanzania tumeruhusiwa kutumia maji ya ziwa victoria kusafirisha hadi kanda ya kati yatafika? Hao mabeberu mbona hawakuzuia?

Tatizo unakuta mnabuni mradi alafu mnategemea hela ya mzungu hapo lazima wawawekee uzia. Ila kama mna internal funding wala hatutolaumu mabeberu kila kitu.

Mfano TZ umeme wetu unategemea gesi zaidi ya 60% mbona mabeberu hawajazuia gesi? Ila waje kuzuia umeme wa maji ambao tunatumia below 40% pekee?

Tuache conspirancy theory na kila kitu kulaumu wazungu, tujitegemee kiuchumi kwanza tuache kupeleka mabakuli.
Wanaomiliki gesi ni wazungu ndio wanaowauzia serikali umeme kwa bei juu unafikiri watakubali bwawa lijengwe?
 
Wanaomiliki gesi ni wazungu ndio wanaowauzia serikali umeme kwa bei juu unafikiri watakubali bwawa lijengwe?
Wanauza umeme?? Au wanauza gesi?? Na kama ulitaka wazungu wasimiliki vitalu na refinery wewe una hizo trillion 20+ za kumudu uwekezaji wa kuchimba gesi?

Then kwanini wapinge Bwawa lisijengwe ilihali 60% ya umeme wa TZ unatumia gesi tayari?? Yaani hta bila Bwawa la Nyerere tayari Gesi inadominate sekta ya nishati sasa kivp waje kuogopa umeme wa maji?
 
Huyu waziri wa Twita awe na huruma hata kidogo, anataka kutuletea umeme wa solar na Upepo ilimradi tu anufaishe tumbo lake.
Hilo lipo kwenye ilani ya CCM na mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa. Yote yaliandikwa na JPM. In fact mpka umeme wa joto ardhi uliandikwa humo so mnamlaumu bure tu.
 
Mama yetu sijui hata kama huwa anapata muda wa kusoma vitu kama hivi au anasubiri ushauri wa Waziri wa Twita.
Kwahiyo hata SGR tusijenge kwasababu tu ina gharama kubwa kuliko MGR zilizopo? Angalienu ufanisi sio gharama pekee. Otherwise hta flyover msingejenga maana ni gharama kuliko barabara za chini!!
 
Mengi yamezungumzwa kuhusu ujenzi wa hilo Bwawa. La hivi karibuni ni pale Waziri husika alipodai mkondrasi wa ujenzi, ambaye ana utaalamu, ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa, ati hana mtambo wa kubeba (winch) wenye uwezo wa kusimika milango ya kuzuia maji yenye uzito wa tani 26. Au ni hadithi ile ile ya wasiotaka bwawa hilo lijengwe.

Je, ukweli ndio huu?

Vita ya mradi wa Rufiji sio ya kwanza Afrika (Dr Yahya Msangi (Phd), Togo West Afrika)

"HUENDA wengi hawajui visa vya mabwawa ya kufua umeme na historia ya Afrika. Nimeona bora niwaelimishe. Mabwawa haya yana kitu kinaitwa 'geo-politics' toka zamani na yapo mabwawa ambayo yamewahi kuhujumiwa ili yasijengwe. Miongoni mwa mabwawa hayo ni Cahora Bassa (Msumbiji/Afrika Kusini) Aswan (Misri) Akosombo (Ghana), Blue Nile (Ethiopia), Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler’s Gorge (Tanzania).

Kati ya haya mabwawa saba, mawili yalishindikana kujengwa kutokana na ‘geopolitics.’ Bwawa la mto Kongo na Stiegler’s. Nchini Kongo Patrice Lumumba ambaye alitoa kipaumbele kikubwa na kuonyesha nia thabiti ya kujenga bwawa kubwa kabisa (urefu maili mbili) kukinga maji ya Mto Kongo, aliuawa kikatili na mradi husika ulikwama.

Bwawa lile kama lingefanikiwa kujengwa, lingekidhi mahitaji yote ya umeme Afrika na Ulaya na bado kungekuwa na ziada. Sehemu ambapo bwawa hili lingejengwa, ndio yenye maji mengi na yaendayo kwa kasi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Lumumba angefanikiwa, kusingekuwa na haja ya nchi nyingine yoyote Afrika kujenga bwawa au kununua mitambo ya kufua umeme.

Kwa kuzuia ujenzi wa bwawa lile, mabeberu walifanikiwa kuzuia maendeleo ya bara zima la Afrika, kwani kusingekuwa na kijiji au nyumba Afrika ingekosa umeme. Viwanda vingechomoza mpaka vijijini.

Afrika ilizuiwa wakati Ulaya iliyotoka kwenye vita ikiruhusiwa kujenga mabwawa tena ya kuchangia! Sababu kubwa ikipigiwa chapuo ni kuwa, mradi utakuwa na hasara na kwamba Kongo haikuwa na uwezo kutekeleza mradi ule!

Ilipofika zamu ya Stiegler’s hadithi ikabadilishwa. Si tu kwamba uchumi wa Tanzania haumudu mradi huo (japo Cuba na China walijitolea) ikaingizwa hadithi ya uhifadhi vyura na vipepeo! Eti, itaathiri Selous! Eti, itapunguza watalii.

Stiegler’s ikakwama! Sasa Stiegler’s inajengwa, lakini hadithi ni zile zile! Wanaojiita wanaharakati wa mazingira wanadai mradi huo utaathiri Selous, wanadai una gharama kubwa, wanadai kuna viumbe adimu Selous! Yaani chura, popo, vipepeo ni adimu na wana thamani kuliko Watanzania! (sikiliza mmoja wao)

Wakati Misri inakusudia kujenga Aswan, Israel akisaidiana na Marekani walikuja juu! Wakamsakama Gamal Abdul Nasser! Lakini, Farao akasimama wima ikajengwa. Akina Israel wakaja Afrika Mashariki kutuambia tukatae, maana watatumia maji yetu! Yani maji ya Ziwa Viktoria na Mto Nile! Wakatuhamasisha tujenge miradi mikubwa ya maji ili yanayoenda Misri yapungue!

Ukweli ni kwamba, maji ya Nile yanazidi mahitaji ya Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan na Misri. Bado tunatumia chini ya 50% ya maji. Mengi yanaishia Bahari ya Mediterranean ambako hata Israel inanufaika nayo. (Kwa wasiojua maji ya Mto Nile siyo ya Ziwa Victoria). Hatimaye Nasser akapoteza maisha baada ya kushindwa vitani. Lakini, bwawa la Aswan lipo na ndio msingi wa Maendeleo ya Misri.

Bwawa la Akosombo nalo halikubaki salama. Ni moja ya mambo yaliyowaudhi Waingereza hadi wakasuka mapinduzi ya kumng'oa Kwame Nkurumah. Lakini, mwana wa Afrika alijenga bwawa hilo. Bwawa la Akosombo ndio kiini cha Maendeleo ya Ghana, linauza umeme Togo, Benin, Cameroon na Nigeria!

Cahora Bassa nalo halikumuacha Samora Machel salama! Likitumika kudhoofisha uchumi na harakati za ukombozi Msumbiji. Wakubwa walilipinga! Afrika Kusini ya makaburu ikawezeshwa kujenga vinu vya nyuklia ili bwawa likihujumiwa aumie msumbiji peke yake! Hao hao wakaja kuwanyang'anya vinu vya nyuklia ilipoonekana ANC itatwaa madaraka! Hawataki ngozi nyeusi imiliki nyuklia!

Bwawa la Blue Nile nalo lilipingwa mno! Lakini, Zenawi akafumba masikio. Linajengwa kwa kasi sasa kwa msaada wa China. Ethiopia inasonga mbele kwa kuwa imeongeza umeme. Sasa wana treni ya umeme.

Hata nia ya Uganda kujenga bwawa Jinja nayo ilipingwa!

Hii ndio historia ya mabwawa Afrika! Wakubwa hawataki tupate umeme. Wanajua umeme utazalisha Viwanda na tutatumia rasilimali zetu wenyewe. Bahati mbaya, Afrika haina uhaba wa vibaraka! Toka enzi za Lumumba, Nasser, Nkurumah! Mara zote na kote watajitokeza kuwaunga mkono mabeberu. Wanatumia sababu zile zile za enzi za akina Lumumba. Tuwapuuze! (Sikiliza Hayati Magufuli)
Blah blah. Ni mradi wa kipuuzi wa karne. Yani tuangalie metrics. Takataka kubwa linazalisha MW 2100 tu. Wakati gesi na upepo vinazalisha mara nyingi zaidi kwa gharama ndogo. Pia ni backward thinking za kishamba kutegemea maji karne hii ambayo kuna climate change. Maji ni unreliable. Kichwa kibovu tu kinachowaza miaka 60 nyuma ndio kinaweza kushabikia upumbavu kama huo. Yani kiufupi lile ni li swimming pool kubwa tu. Yani katiba yetu ingekuwa inawajibisha viongozi, angetapika kodi zetu. Nonsense.
 
Kuna watu ambao siku wakikutana na Mungu uso kwa uso, wana kesi nzito sana za kujibu. Ngoja tu watambe na haya maisha ya miaka 120, halafu mengine ya FOREVER nayo yapo pia yanawasubiri na huko ndiyo tutajua nani ni mbabe kati ya mwenzake. Yaani ni watu wanaumiza sana halafu unakuwa huna hata uwezo wa kuwadhibiti. Hakuna kitu kinaumiza hapa duninani kama kufanyiwa jambo la kijinga na mtu halafu wakati huo huo unakuwa huna uwezo wa kumdhibiti, inaumiza sana
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hizi nadharia za kusingizia mabeberu ndio kikwazo cha maendeleo yetu waafrika hazina nafasi kwa fikra za sasa.
Matatizo ya mwafrika yanasababishwa na mwafrika mwenyewe.
 
Kiburi ya china ni kuzalisha Umeme kwa bei ya chini sana na wa uhakika
 
Kuna kitabu kinaitwa Makuwadi wa soko huria kimeeleza kwa kina hujuma juu ya mradi wa rufiji
 
Naomba nipinge kwa nguvu hoja yako hapa
Kwani shida kubwa ya Afrika ni umeme pekee??
Kwani chanzo Cha nishati kwa Afrika nzima ni HEP pekee??
Hiyo hadithi ya River congo Hydroelectricity power kuwa ingekuja kusapply umeme umeiitoa wapii??

Stiglarz hainuki uharibifu wa mazingira hadi mvua za vuli kukosekana ukanda huo wa Morogoro????

Tusijaribu kuwapa majina mabaya wanaotushauri
Mtoa Mada ameongea mambo ya ukweli. Hakuna beberu anayetaka azidiwe na nchi yoyote ya Africa. Wazungu wanataka daima Africa iwe chini yao. Haiingii akilini eti uharibifu wa mazingira upi? Hao nao ni mamluki wa mabeberu wasioitakia mema Africa. Anasimama mbunge na kutetea upuuzi hta hana haya. Yaani pori lote lile lina uwiano gani na hako ka bwawa? Hilo bwawa ni ndogo, ni kama shimo la mhanga kati Kati ya pori kubwa wala hakina madhara yoyote. Acheni hujuma
 
Back
Top Bottom