Kuna nini nyuma ujenzi wa bwawa la Nyerere la kufua umeme

Naomba nipinge kwa nguvu hoja yako hapa
Kwani shida kubwa ya Afrika ni umeme pekee??
Kwani chanzo Cha nishati kwa Afrika nzima ni HEP pekee??
Hiyo hadithi ya River congo Hydroelectricity power kuwa ingekuja kusapply umeme umeiitoa wapii??

Stiglarz hainuki uharibifu wa mazingira hadi mvua za vuli kukosekana ukanda huo wa Morogoro????

Tusijaribu kuwapa majina mabaya wanaotushauri
Hizo gari chakavu mnazonunua ambazo zina pollute mazingira huwa mnazifikiria?
 
Je, ukweli ndio huu?

Vita ya mradi wa Rufiji sio ya kwanza Afrika (Dr Yahya Msangi (Phd), Togo West Afrika)

"HUENDA wengi hawajui visa vya mabwawa ya kufua umeme na historia ya Afrika. Nimeona bora niwaelimishe. Mabwawa haya yana kitu kinaitwa 'geo-politics' toka zamani na yapo mabwawa ambayo yamewahi kuhujumiwa ili yasijengwe

Makala ( ya Yahya Msangi Ph.D, Togo West Africa )imekaa zaidi ki propaganda haielezi kuwa baadhi ya mabwawa kama ktk nchi za Mozambique, Uganda , Zimbabwe na Zambia yalijengwa na wakoloni hata kabla ya nchi hizo kupata uhuru. Sasa ni nani ndani ya nchi hizo zilizokuwa makoloni ya wareno n.k walikuwa wanapinga miradi hiyo kabla hawajapata uhuru wao ?

Yahya Msangi. Regional coordinator of Occupational Safety, Health and Environment (OSHE) at ITUC Africa in Lome, Togo
http://www.ituc-africa.org
ITUC Africa
The African Regional Organisation of the International Trade Union Confederation (ITUC-Africa) is a Pan-African Trade Union Organization
 
Hii mada japo umeeleza ukwel lkn kuna machawa na mabwege yatakuja kupinga as if yanaundugu na hao watu weupe..wanaharakati ni watu wa hovyo sana
Zinazopingwa ni facts katika maelezo hayo. Mfano: hivi huyo Lumumba aliyetawala kwa muda wa miezi mitatu tu tena katika vita vya kugombea utawala, alipata muda gani kushughulikia hatua za ujenzi wa hilo bwawa la mto congo?

Na haya mabwawa mengine yalijengwa kabla au baada ya ukoloni?
 
Zinazopingwa ni facts katika maelezo hayo. Mfano: hivi huyo Lumumba aliyetawala kwa muda wa miezi mitatu tu tena katika vita vya kugombea utawala, alipata muda gani kushughulikia hatua za ujenzi wa hilo bwawa la mto congo?

Na haya mabwawa mengine yalijengwa kabla au baada ya ukoloni?

Kweli kabisa, msomi huyu makala (Yahya Msangi Ph.D, Togo West Africa ) yake haibebi uhalisia wa changamoto au upinzani ulikuwepo kuhusu miradi hiyo mingi wakati wa ukoloni. Kifupi mwandishi wa makala hii anataka kutufanya waTanzania wote hatuna udadisi kutaka kuelewa je yaliyomo ktk maandishi yake yanabeba ukweli na uhalisia au ni propaganda tupu.

CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM | Facebook

Na Dr Yahya Msangi (Phd) Togo West Afrika ... Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler's Gorge (Tanzania). ... Bwawa la mto Kongo na Stiegler's

 
Ziara ya kihistoria ya rais Samora Machel wa Mozambique kwenye bwawa la umeme la Cabora Bassa jimbo la Tete, nchini Mozambique ambalo lilijengwa na wakoloni wa Kireno wakati wakiikalia nchi ya Msumbiji.



Source : Yassin Amuji
 
Mengi yamezungumzwa kuhusu ujenzi wa hilo Bwawa. La hivi karibuni ni pale Waziri husika alipodai mkondrasi wa ujenzi, ambaye ana utaalamu, ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa, ati hana mtambo wa kubeba (winch) wenye uwezo wa kusimika milango ya kuzuia maji yenye uzito wa tani 26. Au ni hadithi ile ile ya wasiotaka bwawa hilo lijengwe.

Je, ukweli ndio huu?

Vita ya mradi wa Rufiji sio ya kwanza Afrika (Dr Yahya Msangi (Phd), Togo West Afrika)

"HUENDA wengi hawajui visa vya mabwawa ya kufua umeme na historia ya Afrika. Nimeona bora niwaelimishe. Mabwawa haya yana kitu kinaitwa 'geo-politics' toka zamani na yapo mabwawa ambayo yamewahi kuhujumiwa ili yasijengwe. Miongoni mwa mabwawa hayo ni Cahora Bassa (Msumbiji/Afrika Kusini) Aswan (Misri) Akosombo (Ghana), Blue Nile (Ethiopia), Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler’s Gorge (Tanzania).

Kati ya haya mabwawa saba, mawili yalishindikana kujengwa kutokana na ‘geopolitics.’ Bwawa la mto Kongo na Stiegler’s. Nchini Kongo Patrice Lumumba ambaye alitoa kipaumbele kikubwa na kuonyesha nia thabiti ya kujenga bwawa kubwa kabisa (urefu maili mbili) kukinga maji ya Mto Kongo, aliuawa kikatili na mradi husika ulikwama.

Bwawa lile kama lingefanikiwa kujengwa, lingekidhi mahitaji yote ya umeme Afrika na Ulaya na bado kungekuwa na ziada. Sehemu ambapo bwawa hili lingejengwa, ndio yenye maji mengi na yaendayo kwa kasi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Lumumba angefanikiwa, kusingekuwa na haja ya nchi nyingine yoyote Afrika kujenga bwawa au kununua mitambo ya kufua umeme.

Kwa kuzuia ujenzi wa bwawa lile, mabeberu walifanikiwa kuzuia maendeleo ya bara zima la Afrika, kwani kusingekuwa na kijiji au nyumba Afrika ingekosa umeme. Viwanda vingechomoza mpaka vijijini.

Afrika ilizuiwa wakati Ulaya iliyotoka kwenye vita ikiruhusiwa kujenga mabwawa tena ya kuchangia! Sababu kubwa ikipigiwa chapuo ni kuwa, mradi utakuwa na hasara na kwamba Kongo haikuwa na uwezo kutekeleza mradi ule!

Ilipofika zamu ya Stiegler’s hadithi ikabadilishwa. Si tu kwamba uchumi wa Tanzania haumudu mradi huo (japo Cuba na China walijitolea) ikaingizwa hadithi ya uhifadhi vyura na vipepeo! Eti, itaathiri Selous! Eti, itapunguza watalii.

Stiegler’s ikakwama! Sasa Stiegler’s inajengwa, lakini hadithi ni zile zile! Wanaojiita wanaharakati wa mazingira wanadai mradi huo utaathiri Selous, wanadai una gharama kubwa, wanadai kuna viumbe adimu Selous! Yaani chura, popo, vipepeo ni adimu na wana thamani kuliko Watanzania! (sikiliza mmoja wao)

Wakati Misri inakusudia kujenga Aswan, Israel akisaidiana na Marekani walikuja juu! Wakamsakama Gamal Abdul Nasser! Lakini, Farao akasimama wima ikajengwa. Akina Israel wakaja Afrika Mashariki kutuambia tukatae, maana watatumia maji yetu! Yani maji ya Ziwa Viktoria na Mto Nile! Wakatuhamasisha tujenge miradi mikubwa ya maji ili yanayoenda Misri yapungue!

Ukweli ni kwamba, maji ya Nile yanazidi mahitaji ya Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan na Misri. Bado tunatumia chini ya 50% ya maji. Mengi yanaishia Bahari ya Mediterranean ambako hata Israel inanufaika nayo. (Kwa wasiojua maji ya Mto Nile siyo ya Ziwa Victoria). Hatimaye Nasser akapoteza maisha baada ya kushindwa vitani. Lakini, bwawa la Aswan lipo na ndio msingi wa Maendeleo ya Misri.

Bwawa la Akosombo nalo halikubaki salama. Ni moja ya mambo yaliyowaudhi Waingereza hadi wakasuka mapinduzi ya kumng'oa Kwame Nkurumah. Lakini, mwana wa Afrika alijenga bwawa hilo. Bwawa la Akosombo ndio kiini cha Maendeleo ya Ghana, linauza umeme Togo, Benin, Cameroon na Nigeria!

Cahora Bassa nalo halikumuacha Samora Machel salama! Likitumika kudhoofisha uchumi na harakati za ukombozi Msumbiji. Wakubwa walilipinga! Afrika Kusini ya makaburu ikawezeshwa kujenga vinu vya nyuklia ili bwawa likihujumiwa aumie msumbiji peke yake! Hao hao wakaja kuwanyang'anya vinu vya nyuklia ilipoonekana ANC itatwaa madaraka! Hawataki ngozi nyeusi imiliki nyuklia!

Bwawa la Blue Nile nalo lilipingwa mno! Lakini, Zenawi akafumba masikio. Linajengwa kwa kasi sasa kwa msaada wa China. Ethiopia inasonga mbele kwa kuwa imeongeza umeme. Sasa wana treni ya umeme.

Hata nia ya Uganda kujenga bwawa Jinja nayo ilipingwa!

Hii ndio historia ya mabwawa Afrika! Wakubwa hawataki tupate umeme. Wanajua umeme utazalisha Viwanda na tutatumia rasilimali zetu wenyewe. Bahati mbaya, Afrika haina uhaba wa vibaraka! Toka enzi za Lumumba, Nasser, Nkurumah! Mara zote na kote watajitokeza kuwaunga mkono mabeberu. Wanatumia sababu zile zile za enzi za akina Lumumba. Tuwapuuze! (Sikiliza Hayati Magufuli)
Asante Mwengeso kwa mada hii.Kwa uongozi tulio-nao sasa na background yake(from NGOs) na main backer wao(Kikwete),sina shaka yeyote kwamba hii ni kweli.Time will tell,ilà mficha maradhi kifo humuumbua.Wataumbuka tu.
 
Asante Mwengeso kwa mada hii.Kwa uongozi tulio-nao sasa na background yake(from NGOs) na main backer wao(Kikwete),sina shaka yeyote kwamba hii ni kweli.Time will tell,ilà mficha maradhi kifo humuumbua.Wataumbuka tu.
Watanzania tunaduwazwa na wanasiasa.

Wanasiasa wa Chama Tawala wanatudanganya na Siasa za ulaghai kwa visingizio lukuki km ati ukame ndio sababu za upungufu wa maji na uzalishaji umeme.

Wanasiasa wa upinzani wao wanahubiri Katiba Mpya ili iwasaidie kuingia madarakani.
 
Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme.

Ukiuliza watu wawili - watatu unaweza futa post nzima.

JF ni jukwaa la majadiliano na kuelimishana. Hivyo basi toa maelezo kuhusu hili ulilosema kwamba: Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme, ili post yangu ipuuzwe
 
JF ni jukwaa la majadiliano na kuelimishana. Hivyo basi toa maelezo kuhusu hili ulilosema kwamba: Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme, ili post yangu ipuuzwe
Mkuu umejitahidi sana kuelezea kinagaubaga na kuambatisha vielelezo toka vyanzo mbali mbali katika thread yako hii,ili kututoa giza.

Nitakuomba sasa hao wasioamini ulichokieleza wewe, wafungue thread yao kutuelimisha kama wameshindwa jambo dogo tu la kutuletea comment za kimantiki katika thread hii.

Kwa kuwa tunatumia fake ids, waweza kuta unaongea na kubishana na pro Makambas mojawapo waliomwagwa Jf kutushinikiza tusifie uozo unaoendelea, au yaweza kuwa akawa ni Makamba mwenyewe mwamba mnayehangaishana naye, wadhani waweza kumshinda kwa ubishi!

Hivyo usijichoshe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cahora Bassa (Msumbiji/Afrika Kusini) Aswan (Misri) Akosombo (Ghana), Blue Nile (Ethiopia), Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler’s Gorge (Tanzania).
Nile ya Jinja ilijengwa

Grand Renaissance Dam ya Ethiopia imejengwa, tatizo ni misri wanahofia maji yanayotoka blue nile yatakua diverted kushibisha mradi so hapo hakuna beberu ila ni internal dispute tu.

Mbona Tanzania tumeruhusiwa kutumia maji ya ziwa victoria kusafirisha hadi kanda ya kati yatafika? Hao mabeberu mbona hawakuzuia?

Tatizo unakuta mnabuni mradi alafu mnategemea hela ya mzungu hapo lazima wawawekee uzia. Ila kama mna internal funding wala hatutolaumu mabeberu kila kitu.

Mfano TZ umeme wetu unategemea gesi zaidi ya 60% mbona mabeberu hawajazuia gesi? Ila waje kuzuia umeme wa maji ambao tunatumia below 40% pekee?

Tuache conspirancy theory na kila kitu kulaumu wazungu, tujitegemee kiuchumi kwanza tuache kupeleka mabakuli.
 
, wanadai kuna viumbe adimu Selous! Yaani chura, popo, vipepeo ni adimu na wana thamani kuliko Watanzania! (sikiliza mmoja wao)
Muandishi ni PhD kweli?? Hivi anajua maana ya bio diversity kweli? Hajui kwamba binadamu pia inategemea species tofauti ili tuweze kusurvive? Anafahamu mentallity ya binadamu ni bora kuliko ndege na wadudu ndio ilisababisha moja ya janga kubwa katika historia ya dunia?


Inaweza kuwapo sababu bora zaidi za kupromote mradi huu ila sio kwa sababu eti vipepeo sio bora kuliko binadamu, very illogical argument.
 
Kwa kuzuia ujenzi wa bwawa lile, mabeberu walifanikiwa kuzuia maendeleo ya bara zima la Afrika, kwani kusingekuwa na kijiji au nyumba Afrika ingekosa umeme. Viwanda vingechomoza mpaka vijijini
Huyu PhD uchwara anapotosha tena, mradi gharama zake ni Trillion 180 Za Kitanzania hao DRC wangetoa wapi hela?

Then mbona hasemi Inga 1 na Inga 2 dams zilijengwa tayari maana ana conclude as if umeme wa DRC sahivi hautegemei hayo mabwawa mawili??

Afrika Kusini ya makaburu ikawezeshwa kujenga vinu vya nyuklia ili bwawa likihujumiwa aumie msumbiji peke yake! Hao hao wakaja kuwanyang'anya vinu vya nyuklia ilipoonekana ANC itatwaa madaraka! Hawataki ngozi nyeusi imiliki nyuklia!
Mradi uliachwa mwaka 1989 na makaburu wenyewe maana iliwakamua pesa nyingi sana sasa sijui ni lini walinyang'anywa na mabeberu. In fact serikali ya Makaburu ilikua imewekewa vikwazo na mataifa mengi tu ya mabeberu sasa sijui hyu PhD anataka kupotosha historia kwa faida ya nani.
 
Muandishi ni PhD kweli?? Hivi anajua maana ya bio diversity kweli? Hajui kwamba binadamu pia inategemea species tofauti ili tuweze kusurvive? Anafahamu mentallity ya binadamu ni bora kuliko ndege na wadudu ndio ilisababisha moja ya janga kubwa katika historia ya dunia?


Inaweza kuwapo sababu bora zaidi za kupromote mradi huu ila sio kwa sababu eti vipepeo sio bora kuliko binadamu, very illogical argument.

Hoja yako ina uzito kuwa uhai na ustawi wa binadamu unategemeana na hali ya "bio-diversity". Lakini, kwa jinsi Mungu (kama unaamini yupo) alivyomuumba binadamu kutawala dunia (nukuu imeambatanishwa), binadamu huyo ana uwezo wa kuweka mazingira rafiki kwa hao viumbe. Hivyo basi, "argument" yake inabaki kuwa "logicaL".

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
 
Sina imani na makamba hata kidogo, Kalemani angeweza kumaliza Ujenzi salama, Makuwadi wa mabeberu wanafanya kila jitihada kuturudisha nyuma, tutavuka MUNGU Mkubwa.
Mama amenisikitisha sana mtu akiyeponda huo mradi ndo leo kakabiziwa asimamie mradi mbona kituko
 
Back
Top Bottom