omtiti
JF-Expert Member
- Jun 19, 2019
- 1,022
- 1,590
Nawauliza Watanzania, nchi hii ni maskini kweli au inakosa viongozi wenye maono?
Kabla ya Magufuli kuingia madarakani Kikwete alitembeza sana bakuri ughaibuni,tulivyoambulia ni pamoja na vyandarua toka USA
Magufuli akaingia madarakani slogan yake akasema nchi hii si maskini, ina kila aina ya utajiri, akasisitiza Watanzania tuchape kazi na ndani ya muda mfupi alifanya maajabu, shahidi ni Rais wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, mara kwa mara alikiri hadharani juu kazi nzuri ya hayati Magufuli.
Ifahamike mzee huyu ni mchamungu haswa.
Zama za MAGUFULI zimepita.
Awamu ya sita imeingia naona kama tunaanza kulemazwa na misaada uchwara tena, walewale ambao wanafahamu sisi ni matajiri kwa raslimali zetu ndio wako mstari wa mbele na vijimisaada. nasi tunashangilia kweli kweli.
Je, tunahitaji misaada ama tunahitaji viongozi wenye maono ya kuhakikisha neno maskini linafutika midomoni mwetu.
Na kwanini kiongozi anayejaribu kutufumbua macho anakuwa adui kwa hawa wanaotubatiza umaskini?
Huu unaoitwa umaskini ni wa kweli au ni ukosefu wa akili ,uzalendo na maarifa?
Jamaa badala watupe ndoano tuvue samaki kazi yao ni kutupatia samaki wa kula ,nini kilicho nyuma ya hii ajenda?
"Mtanikukumbuka "alisema kiumbe mmoja