Kuna maisha baada ya kupigwa kibuti

Kuna maisha baada ya kupigwa kibuti

Asante, tutambue tu kuna watu wanakuja kwneye maisha yetu kama baraka wengine huja kama mafundisho. Ukianguka unanyanyuka unajifuta vumbi unaendelea mbele, yeye si wa kwanza na wala hawezi kua wa mwisho,

Kubwa na cha msingi ni kujua hakua riziki yako pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali, utapata atakayejua thamani ya machozi yako na kukupa upendo mara mbili ya ulioutoa

Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee kubali hali, lia unavyoweza hakikisha ukitoka hapo hulii tena then move on with your life.
Madame hii ni changamoto sana inaitaji maneno ya kuamua na kuendelea mbele..japo ni kazi nilipambana nayo sana.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Bado hujapenda kisawasawa wewe
Nilipenda mpaka nikafeli mitihani na kukonda nikakonda maradufu, sema ndo hivyo niliamua kuchukua maamuzi mapema ya kumwambia tuachane na yeye akajibu poa,

Maana nilikuwa na ushahidi wa kutosha kama ananisaliti na ni kweli bwana ake mpya alikuwa amenizidi kipato hivyo nikakubaliana na hali halisi
 
Unakua umependa kweli mkuu?
Huwa napenda Sana sio kidogo, ila ninapoona maumivu yanazidi huwa najiuliza, "kabla ya kukutana nae nilikuwa naishi vipi?" Nikishapata jibu la hapo tu basi nachukua maamuzi haraka sana na huwa sijutii

Kumbuka ukisubiri akutamkie yeye maumivu yatakuwa makali zaidi, hivyo njia nzuri ni kuamua wewe.

Mwanzoni itakuwa ngumu ila ukishakubaliana na hali iliyopo hautaumia sana
 
Kupigwa kibuti sioo sababu ya wewe kuzeeka kwa vilio vya masononeko na lawama za Why me Lord Why me kama Shaggy..Tabasamu lako lazima liendelee kipindi cha Jua au kipindi cha mvua..Hakuna Binadamu mwenye kauli ya mwisho kwa furaha na smile yako,There is life still after a break up,kama alivyokuja kwenye maisha yako na kukukuta unasmile muache aondoke peke yake na aliache smile pale alipolikuta..Usimfanye ajihisi yeye ndo malkia saaaanaaa,au yeye ndo mfalme kiivyo,kwamba alipoondoka maisha yako yame-shake,kwani yeye ni nani??Alichangia hata koleo moja kwenye karai la udongo aliotumia Mungu kukuumba???Tupa kule...
Ladies and Gentlemen,Keep smiling always no matter what,wewe ni kama ATM ya NMB,People will always come in,withdraw money and go,Huna haja ya kumlilia mpuuzi yeyote asiyejua thamani ya Penzi lako!


Kamata glass tugonge cheers[emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482]
agiza nakuja kulipa bill zote mdogo wangu
 
Back
Top Bottom