Namuona Dkt. Nchimbi akifanikiwa pakubwa kujenga utaasisi ndani ya CCM

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,602
Kama Leo ingekuwa ni 2015 na Dkt.Ncimbi angekuwa ni Katibu Mkuu wa CCM naamini angepambana vya kutosha kumpambania Lowassa ndani ya CCM lakini Kwa Sasa ana mtazamo tofauti kabisa, mtazamo alionao Sasa ni maslahi ya CCM kwanza na maslahi binafsi baadaye.

SG Nchimbi ana historia kubwa ndani ya CCM ,CCM ambayo inaweza kukisaidia Chama na kukibadilisha na kukijengea utaasisi na hapa ndio nasimama na Kila kauli na vitendo vya SG huyu mpya maana ni mtu sahihi wa kuisuka CCM Upya.

Mtazamo wa Dkt. Nchimbi umebadilika kabisa kutoka kuamini katika makundi ya kumfia mtu mpaka kuamini katika makundi ya kukifia Chama. Laiti kama Leo ingekuwa ni 2015 angekuwa katika kundi lile mpaka mwisho ila Sasa kundi analoamini ni umoja na mshikamani ndani ya CCM.

Kwa kauli yake aliyotoa hivi karibuni kule Zanzibar siku chache baada ya uteuzi wake kama SG wa CCM kwamba utamaduni wa CCM ni vipindi 2 na 2025 ataendelea Rais Samia inaonesha Wazi anatambua ni namna gani makundi ya wasaka urais yatavyovuruga mipango ya Chama hivyo ametoa tahadhari ya mapema kabisa kwamba kundi lililopo Sasa ni la kumuunga mkono Rais Samia.

Kwangu Mimi naona hii kama ni hatua ya awali kabisa ya SG Nchimbi kuunganisha chama na wanachama wake na kujenga mshikamano wa kutosha ndani ya CCM na Kwa hatua hii tutegemea makubwa na ushindi wa kishindo Kwa CCM uchaguzi mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom