Hii tabia wanayo sana wanaume, mtu anataka kama mmezaa nae basi aendelee tu kukutumia bila hata kujua kuwa mapenzi kuna wakati yanaisha kabisa, na akiona unampotezea ndio atasimulia ndugu na marafiki kuwa hutaki yeye awaone watoto, ukimpa yeye watoto bado atataka wewe uwe unaenda kumwona mtoto kwake huo si ukorofi jamani???? Ukimwambia unahitaji kufanya mambo yako ila mtoto utatafuta njia ya kumjulia hali basi ndio hapokei sim kabisa ili kukukomesha, ndio maana naona mtu mkiachana bora mtoto nikamsalimie kupia ofisi za ustawi wa jamii kama ni wakati wa likizo au shuleni (bording) wakati mwingine, nikijisikia kwenda kumuona mwanangu nampigia simu mwalimu siku hiyo naenda asubuhi nakaa na mwanagu hadi jioni, yeye akili yake inajua imenikomesha kumbe mimi namwona mwanangu pasipo karaha.