Kuna haja ya kuwa maadui baada ya kuachana?

Kuna haja ya kuwa maadui baada ya kuachana?

Nafikahedi

Member
Joined
Mar 7, 2015
Posts
61
Reaction score
22
Naomba kuelewa juu ya hili kwani kuna rafiki yangu kaachana na baba watoto wake, cha kushangaza mwenzie kamnunia hata akimtumia massege ya kawaida kabisa kuhusu watoto hajibu wala simu hapokei na mwenzie ndiye aliyebaki na watoto.

IeIeweke rafiki yangu huyo hampigii kuomba warudiane na ana amani kabisa lakini mwenzie kajenga uadui kabisa. Kwani haiwezekani kuachana na mkawa na amani tu huku kila mtu akiendelea na mambo yake.

Naomba tujadili
 
Kwa nini ule matapishi yako?Move on, ni utoto kuwa na mahusiano na mtu uliyeachana nae.
 
Tatizo hapo ni watoto,watoto waende kwa baba yao.
 
Tukishaachana Lazima Kuwe Na Mipaka Ya Kuwasiliana.Sio Kila Wakati Tunapigiana Pigiana Simu.Kama Swala Ni Watoto.Lazima Tuweke Utaratibu Maalum Wa Kuja Kuwaangalia Watoto.Watoto Isiwe Sababu Ya Kusumbuana.
 
Sio yvema kuwa maadui, cusez ndo mshaachana,watoto ni wenu wote.mlishachanganya damu akiona kachuna ampelekee watoto.
 
Back
Top Bottom