Na huwa ving'ang'anizi kweli. Katika maisha yangu siku zote nitajitahidi kuwa mkweli katika mahusiano. Ntajitahidi kumheshimu, kumpenda na kumthamini mwenza wangu. Nitamvumilia. Nitakuwa mnyenyekevu kwake.atafanya vituko vyake vyote ntakuwa humble. Lakini siku nikisema imetosha, huwa imetosha kweli. Hata siku moja sitokuwa sababu ya kuachana. Siku yeye atakayokuwa sababu, we never met before.
Nima mfano wa my recent relationship. Nilikuwa katika mahusiano na dada mmoja mrembo wa haja. Nilimpa uhuru anakuja nyumbani kwangu anavyojisikia. Wala hahitaji kutoa taarifa. Anashika simu yangu kila atakavyo. Nampa mahitaji yote. Namheshimu. Namjali. Nampenda. Ikija kwenye shoo nasimamia shoo ile mbaya. Ananiudhi mara kibao, sijawahi hata kumfokea. Siku zote nakuwa wa kwanza kutafuta suluhu.
Wenzake wakawa wanampa kiburi. Wanamfundisha kuwa mie kwake sifurukuti. Kitu kidogo tu, hata nisipokee simu yake, hana muda wa kuuliza kulikoni, akaanza kuwa anatishia tuachane.
Akaanza tabia nikimpigia simu hapokei. Anajifanya kakasirika. Kosa lenyewe, unakuta mie kuchelewa kujibu texts zake.
Siku moja nikawambia sipendezwi na tabia yake, akaja juu eti nisimfundishe tabia alishafundishwa na mama yake.
Nikawa mpole tu. Upole wangu ukamfanya azidishe vituko akijua nampenda sitofurukuta. Lkn nilikuwa namwambia siku nitakayochoka itakuwa moja tu. Wenzake wakawa wanamwambia mkwara tu yule jamaa hana jeuri. Naye anapata kiburi.
Siku ikafika mkuu.
Huki natabasamu kama Baba Rizi, nikamwambia safari yetu imefika ukingoni hatuwezi endelea.
Akaondoka kwa nyodo, anasema, utanitafuta tu.
Nikacheka zangu.
Ulipoisha mwezi sijamtafuta akajua ishakula kwake.
Aliwatumia hadi mama na dada zangu wambembelezee aligonga mwamba. Akasema basi walau tuwe marafiki baada ya kuona muda unakwenda mie kauzu. Nikamwambia sinaga urafiki na mtu niliyewahi kutoka naye kimapenzi, wala sinaga ex. Naanza maisha upya.
Nimetoa stori ndefu hapa si mahali pake. Muhimu, wewe usiwe sababu ya kuvunjika uhusiano.