Kuna haja ya kuwa maadui baada ya kuachana?

Kuna haja ya kuwa maadui baada ya kuachana?

Kama mliwahi kuwa wapenzi kisha mkaachana na kuendelea kuwa marafiki jibu jepesi ni kuwa hapakuwahi kuwa na mapenzi ya dhati baina yenu au bado mna mapenzi mazito na huenda muda wowote mkarudiana.

Binafsi sitaki na wala siruhusu urafiki wa aina yoyote baina ya mpenzi wangu na mtu wake wa zamani.

kuna ukweli kuna mtu untill today tukiwekwa chumba kimoja ...!!!
 
Inategemea sababu iliyowafanya waachane na jinsi ya walivyoachana pia. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa kila mtu ana jinsi ya anavyopokea na kukubali halihalisi kama hizo za kuachana. Ila baada ya muda naamini watakuwa sawa tu
 
Hii tabia wanayo sana wanaume, mtu anataka kama mmezaa nae basi aendelee tu kukutumia bila hata kujua kuwa mapenzi kuna wakati yanaisha kabisa, na akiona unampotezea ndio atasimulia ndugu na marafiki kuwa hutaki yeye awaone watoto, ukimpa yeye watoto bado atataka wewe uwe unaenda kumwona mtoto kwake huo si ukorofi jamani???? Ukimwambia unahitaji kufanya mambo yako ila mtoto utatafuta njia ya kumjulia hali basi ndio hapokei sim kabisa ili kukukomesha, ndio maana naona mtu mkiachana bora mtoto nikamsalimie kupia ofisi za ustawi wa jamii kama ni wakati wa likizo au shuleni (bording) wakati mwingine, nikijisikia kwenda kumuona mwanangu nampigia simu mwalimu siku hiyo naenda asubuhi nakaa na mwanagu hadi jioni, yeye akili yake inajua imenikomesha kumbe mimi namwona mwanangu pasipo karaha.

Kinda umeongea kwa uzoefu fulani amazing hivi. Ha ha ha. Anyways, kweli kuna mazingira yakijitokeza unajikuta njia pekee na bora ni hiyo ili upate peace of mind. Cheers
 
Mi huwa nasema siku zote, kama hamkuweza kuheshimiana na kupendana ndani ya uhusiano hata ikapelekea mkaachana, hamwezi kujidanganya mnaheshimiana na kupendana baada ya kuachana kwenu. I'm not having an ex in my life. If u walk away, we'd never met before.
 
Mi huwa nasema siku zote, kama hamkuweza kuheshimiana na kupendana ndani ya uhusiano hata ikapelekea mkaachana, hamwezi kujidanganya mnaheshimiana na kupendana baada ya kuachana kwenu. I'm not having an ex in my life. If u walk away, we'd never met before.


Nimeipenda hii mkuu. Msimamo wa aina hii ni salama zaidi. Japo inahitaji ujasiri sana, hasa pale unapojikuta mwenzio ni king'ang'anizi.
 
Nimeipenda hii mkuu. Msimamo wa aina hii ni salama zaidi. Japo inahitaji ujasiri sana, hasa pale unapojikuta mwenzio ni king'ang'anizi.
Na huwa ving'ang'anizi kweli. Katika maisha yangu siku zote nitajitahidi kuwa mkweli katika mahusiano. Ntajitahidi kumheshimu, kumpenda na kumthamini mwenza wangu. Nitamvumilia. Nitakuwa mnyenyekevu kwake.atafanya vituko vyake vyote ntakuwa humble. Lakini siku nikisema imetosha, huwa imetosha kweli. Hata siku moja sitokuwa sababu ya kuachana. Siku yeye atakayokuwa sababu, we never met before.

Nima mfano wa my recent relationship. Nilikuwa katika mahusiano na dada mmoja mrembo wa haja. Nilimpa uhuru anakuja nyumbani kwangu anavyojisikia. Wala hahitaji kutoa taarifa. Anashika simu yangu kila atakavyo. Nampa mahitaji yote. Namheshimu. Namjali. Nampenda. Ikija kwenye shoo nasimamia shoo ile mbaya. Ananiudhi mara kibao, sijawahi hata kumfokea. Siku zote nakuwa wa kwanza kutafuta suluhu.

Wenzake wakawa wanampa kiburi. Wanamfundisha kuwa mie kwake sifurukuti. Kitu kidogo tu, hata nisipokee simu yake, hana muda wa kuuliza kulikoni, akaanza kuwa anatishia tuachane.

Akaanza tabia nikimpigia simu hapokei. Anajifanya kakasirika. Kosa lenyewe, unakuta mie kuchelewa kujibu texts zake.

Siku moja nikawambia sipendezwi na tabia yake, akaja juu eti nisimfundishe tabia alishafundishwa na mama yake.

Nikawa mpole tu. Upole wangu ukamfanya azidishe vituko akijua nampenda sitofurukuta. Lkn nilikuwa namwambia siku nitakayochoka itakuwa moja tu. Wenzake wakawa wanamwambia mkwara tu yule jamaa hana jeuri. Naye anapata kiburi.

Siku ikafika mkuu.

Huki natabasamu kama Baba Rizi, nikamwambia safari yetu imefika ukingoni hatuwezi endelea.

Akaondoka kwa nyodo, anasema, utanitafuta tu.

Nikacheka zangu.

Ulipoisha mwezi sijamtafuta akajua ishakula kwake.

Aliwatumia hadi mama na dada zangu wambembelezee aligonga mwamba. Akasema basi walau tuwe marafiki baada ya kuona muda unakwenda mie kauzu. Nikamwambia sinaga urafiki na mtu niliyewahi kutoka naye kimapenzi, wala sinaga ex. Naanza maisha upya.

Nimetoa stori ndefu hapa si mahali pake. Muhimu, wewe usiwe sababu ya kuvunjika uhusiano.
 
Back
Top Bottom