Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,601
Karibuni tena kwenye makala zangu za “Kwa Maslahi kwa Taifa”, zinazozungumzia mada mbalimbali kuhusu taifa letu ziwe ni za kisiasa, za kiuchumi au za Kijamii, baada ya leo ni kuhusu kumuenzi Mwalimu Nyerere, kwa vile Tarehe 14 October ni Nyerere Day, leo naomba tutafakari jinsi sisi Watanzania, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, jee tunamuenzi kweli, kwa mawazo maneno na matendo?,
Mwalimu Nyerere sio tuu alikuwa ni muasisi wa CCM, mpaka kifo chake aliiamini CCM, hivyo hata baada ya nchi Tanzania, kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992, bado Mwalimu aliamini kuwa Wapinzani wanaweza kuleta wabunge bora, na hili tumelishuhudia kwa baadhi ya wabunge wa upinzani,walikuwa ni wabunge bora kabisa, lakini kwenye uraisi wa JMT, Mwalimu Nyerere aliamini “Rais bora atatoka CCM pekee”. Jee kuna Wana CCM wanao maishi Baba wa Taifa kwa mawazo, maneno na matendo?, ama watu tunamuenzi Mwalimu kwa mawazo na maneno tuu, lakini matendo na kumuishi....!.
Mimi ni mtu wa mastory mastory, yaani ni story teller, hivyo kama wewe sio mtu wa mastory story, katishia hapa, nenda mwisho, wale wa mastory mastory, tuendelee...
Jinsi Nilivyo Mfahamu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Baada ya sekondari nikajiunga na chuo cha Uandishi habari TSJ, ndipo Jumapili moja asubuhi, nikaja kuamshwa na mlinzi wa hostel, kuna nina mgeni!, si unajua tena mambo ya ujana, na hostel, ukisikia tuu una ugeni basi unajua ni ugeni wa type gani, ila asubuhi, tena Jumapili, asubuhi ni hatari!, kunaweza kutokea ajali!.Mimi nimezaliwa miaka ya mwishoni kwa 60s, hivyo nimepata akili za kujitambua nilipoanza Darasa la kwanza, mwaka 1975 Shule ya Msingi ya Nyakahoja jijini Mwanza, kwa kumsikia tuu Rais Nyerere, na kumuona kwenye magazeti baba Mzee Mayalla (RIP) akisoma. Mwaka 1976, baba alipatwa na matatizo kazini, tukahamishwa usiku usiku na landrover 109 za polisi na kupelekwa kijijini Itonjanda huko Tabora, huku ni kwa bibi mzaa baba, babu mzee wa Kusukuma baada ya kuoa mwanamke wa Kinyamwezi, Mwanza tuliishia kuisikia tuu!, akahamia jumla Tabora.
Nimeishuhudia kwa Macho, CCM Ikizaliwa!, Ile Kauli ya Kila Lenye Mwanzo...
Ile mwaka 1977 wakati CCM inazaliwa nilikuwa darasa la 3 Shule ya Msingi ya Itonjanda, siku hiyo shule tulichinja ng’ombe na ndio mara yangu ya kwanza kushuhudia jinsi wanafunzi wanavyogombea nyama!, nikawa nawashangaa maana mimi nilikuwa sipendi nyama ya ng’ombe nilipenda kuku, lakini baada ya kufika kijijini, zile kuku ziliishia Mwanza!, ila niliishuhudia CCM ikizaliwa!. Ule msemo wa kila lenye mwanzo lina mwisho, ni uongo, sio kila lenye mwanzo lina mwisho!, CCM ina mwanzo tuu lakini ....
Kumuona Nyerere kwa Macho kwa Mara ya Kwanza,
Mwaka 1978, nikafuatwa kijijini na baba yangu mdogo, Mzee Mathew Kasanga, na kuja kuishi na familia yake jijini Dar es Salaam, eneo la Drive In, kanisa letu ni St. Peter, hivyo siku ya kwanza napelekwa kanisani, mimi si mgeni kanisa hilo, hivyo tulipoingia, nikashangaa wenzangu wanajazana viti vya nyuma, wakati pale mbele kuna rows za viti vitatu ziko tupu, hivyo mimi na ushamba wangu, nikajiona mjanja ngoja niwahi kukaa siti za mbele, hivyo nikaenda kukaa siti ya kwanza kabisa niko peke yangu!.
Nikaona kama watu wananishangaa shangaa, mara nikafuatwa na mzee mmoja amevaa Kaunda suti nyeusi na kuniuliza, wewe ni nani?, nikamtajia jina, akaniuliza unakaa wapi, nikamjibu, akaniuliza, wewe ni mgeni kanisa hili, hujui hizi siti za nani?, nikajibu mimi ni mgeni na leo ndio mara yangu ya kwanza kuja kanisani!, nikaambiwa nifuate, nikatolewa nje huku kanisa zima wanashangaa!. Kule nje nikaitiwa polisi nikabidhiwe nikahojiwe!, ndipo ndugu zangu wakawafuate wale wazee na kuwasihi nisamehewe, nikasamehewa na kurudi ndani.
Baada ya kurudi kanisani ndipo nikamuona babu mmoja ana nywele nyeusi na nyeupe, ndipo nikamkumbuka ni Nyerere, akaenda kukaa kwenye benchi zima la pili peke yake!. Benchi la kwanza liko tupu, na benchi la mwisho wamekaa watu wawili mwanzo wa benchi na mwisho wa benchi!. Sasa ndio nikaelewa kwanini watu walinishangaa!. Hivyo mimi mwenzenu Nyerere nimemuona live toka mwaka 1978!.
Wakati wa kutoka nikaona watu wanatoka kanisani haraka na kupanga foleni pale nje kwenye ngazi kumsubiri Nyerere atoke, alipotoka akawa anawasalimia watu kwa kuwashika mkono. Jumapili iliofuata na mimi nikafoleni ila mkono sikushikwa, na iliofuta, na iliyofuata, hatimaye nikaacha kufoleni kwa kujua Nyerere hashiki mikono ya watoto.
Baadaye, nikawa mtumishi wa kanisa, nikawa naomba kupangiwa misa ya kwanza, hivyo nikawa namhudumia Mwalimu Nyerere kwa kumshikia kisahani cha hostia, na ndipo pia nikayaona meno yake kwa karibu na kuijua maana ya jina la Mchonga!.
Tangu hapo nikawa namfuatilia sana, ile hotuba yake ya kutangaza vita, nikaikariri baadhi ya vifungu na kumuiga, “Uwezo wa kumpiga tunao, Sababu ya kumpiga tunayo, Nia ya kumpiga tunayo, Tutampiga Amini!.”
Mwaka 1979 kwenye mapokezi ya mashujaa wetu pale uwanja wa Taifa nilikuwepo na kumshuhudia Mwalimu machozi yakimtoka kutokana na lile tukio! .
Baada ya kumaliza shule ya Msingi, familia ya Mzee Kasanga ikahamia Mikocheni opposite na Msasani kwa Nyerere, mimi nikajiunga sekondari ya Tambaza, tulikuwa darasa moja na mmoja wa watoto wa Nyerere akiishi hapo Msasani sasa kwa Nyerere tukawa tunakwenda kucheza!.
Baada ya Tambaza nikaenda Ilboru, nikapelekwa nyumbani kwa Makongoro Nyerere, enzi hizi Mako ni mjeshi. Nilipelekwa pale na Rastafarian mmoja, mdada wa Kijamaica aliyelowea Tanzania akiitwa Gipsy, tukatokee kupatana sana na Mako, maana ndege wafafanao huruka pamoja!, siku za weekend ni usawa wa Cave, kiukweli sijui alikuwa anarudi home saa ngapi!.
Kufika nikakuta jamaa fulani mweupe ana bonge la afro na gari sports car nyekundu na kujitambulisha Mimi ni Madaraka Nyerere, mtoto wa Nyerere, anahitajika Msasani kwa Nyerere!.
Naomba niishie hapa, tukutane wiki ijayo mjue niliitiwa nini Msasani kwa Nyerere?, Jee nilikwenda?, Nilimuona Mwalimu Nyerere?.
Nawatakia Nyerere Day Njema.
Paskali.