CCM iliacha siku nyingi kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa vitendo

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Kusema CCM inamuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere mimi binafsi napinga kauli hiyo kuwa sio kweli.

CCM haina ubavu wa kumuenzi Mwl. Nyerere kwa vitendo, labda kwa maneno ya majukwaani. Hayati Baba wa Taifa alikufa na kinyongo sana kutokana na misingi yote aliyoijenga kubomolewa na CCM na kuwa na CCM ya Ufisadi wa kutisha kwa taifa.

Baya zaidi Mafisadi ni viongozi wenyewe. Hayati Baba wa Taifa alianzisha Azimio la Rushwa ili kuwe na miiko kwa viingozi kufanya mambo yasiyostahili kwa viongozi.

Hayati Baba wa Taifa aliiheshimu sana katiba ya nchi lakini leo hii katiba inavunjwa kwa makusudi na viongozi walioapa kuilinda kuitetea na kuisimamia. Leo bunge lina wabunge wasio na chama, wabunge waliofukuzwa uanachama na chama kilichowadhamini lakini bunge na serikali ndio vyombo vinavyowalinda.

Leo rasilimali za nchi zinapewa wawekezaji bila wananchi kushirikishwa ili mradi viongozi wameamua. Leo viwanda vyote alivyovijenga Hayati Baba wa Taifa wamegawana na kuuziana Makada wa CCM kipo wapi Kiwanda cha Tanganyika Packers? Kipo wapi Kiwanda cha Urafiki?

Ipo wapi Benki ya NBC? Ziko wapi nyumba za serikali alizozijenga Nyerere? Zote makada wa CCM wameuziana na kugawana. Hatuwezi kupanda kwenye majukwaa na kudai eti tunamuenzi Hayati Mwl. Nyerere kwa kuviharibu vile vyote alivyovijenga.

CCM aliyoianzisha Hayati Baba wa Taifa imepoteza madhumuni yake ahadi zake na imani kwa wanachama. Leo kujiunga na CCM unapewa pesa au cheo.

Leo kupata uongozi ndani ya CCM ni pesa yako, huwezi kuwa Mbunge, Diwani, Mwenyekiti wa CCM Mkoa au Wilaya bila pesa huwezi kusema tunamuenzi Hayati Baba wa Taifa kwa CCM ya aina hii.

Leo Urais ndani ya CCM kila mtu anauweza ili mradi awe na pesa, ndio maana Makada wanatafuta pesa kwa Ufisafi mkubwa kwa ajili ya kugombea Urais.
 
Back
Top Bottom