CHADEMA ni wazalendo. Wanaishi kwa vitendo maono ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Huu uzi ni maalum kuwapa maua yao wenzetu kwenye siasa, CHADEMA, kwa uzalendo mkubwa wanaouonyesha kwa nchi yetu ya Tanzania. Na pia kwa muda mrefu wameonyesha kuishi kwa vitendo kwenye maono ya baba wa taifa, Mwalimu Nyerere.

Wiki hii mara baada ya uteuzi na kukabidhiwa ofisi kwa katibu mwenezi wa chama pendwa CCM, komredi Makonda, hawa wenzetu waliibuka na kutoa maoni ya kuonyesha kutopendezwa na uteuzi huo. Askofu wa CHADEMA, Ndugu Mwamakula kupitia ukurasa wake wa Facebook alidai CCM inajiundia mgogoro bila kujua. Tukijikumbusha kauli maarufu ya hayati baba wa taifa inayosema "Nang'atuka, lakini bado nasisitiza kuwa, bila CCM imara nchi yetu itayumba" basi moja kwa moja utaona wanaCHADEMA hasa viongozi wao wanatambua kuwa bila CCM imara nchi itayumba.

CHADEMA ni wazalendo na hawatali nchi iyumbe ndo maana kwenye karibu kila jambo la CCM lazima wajitokeze makada na viongozi wao kutoa maoni ya kupongeza na kukosoa. Jiulize kama CCM inajiundia mgogoro si ndo faida kwa wapinzani? CCM ikiingia kwenye mgogoro si ndo itasababisha wapinzani wajibebee kura kiulaini? Si ilibidi wakiona makosa kwenye teuzi za CCM wayasifie ili iwe faida kwao? Kwa kifupi hata wapinzani wanajijua kwa sasa bado CCM imara inahitajika ndo maana utaona kina Lema, Mwamakula, Malisa na wengineo wanatoa maoni kwenye kila jambo la CCM.

Mimi niwaambie CHADEMA kuwa wasiwasi walioonyesha na kudhani CCM itayumba kwa sababu ya uteuzi wa Makonda wanapaswa kuuacha na kuendelea kuiamini CCM iliyobeba matumaini yao.

NINAWAPONGEZA KWA UZALENO
 
Uko sahihi chadema ni watoa taarifa
 
Back
Top Bottom