Kumpa mtoto Chakula na Sehemu ya kuishi hiyo haitoshi wewe kuwa Baba au Mama

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,038
45,611
Unapokuwa na Familia Usiseme Kazi yako ni kuwapa Chakula tu na Sehemu ya kulala.

Unapoitwa Baba au Mama Lengo kubwa sio kumpa mtoto Chakula au Sehemu ya kulala , Maana kila mtu anaweza kufanya hivyo.

Unapokuwa na Familia tenga Muda wa kumjenga mtoto wako kumpatia MAARIFA ya kumjenga Kama kuhakikisha anakuwa Wiser , smater, God fearing and Etc.

Hakikisha Mwanao unapata Muda wa kumjenga kiakili, kihisia na kiroho ili aje kuwa mtu Bora.

Nasema hivi maana Kuna Watu wanajiita Baba na wengine Mama lakini hawakustahili kuwa Baba Mama maana wao jinsi wanalea watoto wamekariri kulea ni kutoa chakula na sehemu ya kulala tu.

Na mwisho wamezalisha taifa bovu.
 
Kweli kabisa hii ya kutoa chakula na malazi ni sawa na kumfuga mtoto.

Tunapaswa kutoa na malezi pia, yaani mambo ni matatu:-
1. Chakula (afya njema)
2. Malazi (ulinzi sahihi)
3. Malezi (hulka/utashi sahihi)

Watu wengi sana wanafuga watoto, ndio maana unakuta mzazi anafurahia kuona mtoto amenenepa bila mpangilio akiamini ndio kulea kumbe ni kumharibu mtoto. Na hawq ni wengi sana.

Nolisoma mahali kuwa watu/wazazi wenye vipato vikubwa na vya kati wengi wanakosea kwa kuwapa watoto wao vile vitu walivyokosa wao utotoni, yaani wanaishi maisha ya utoto waliyoyakosa kwa watoto wao.

Hakuna ubaya sana kufanya ivyo kama yakiwa ni maisha chanya ila ubaya ni kuwa mingi ya mitindo hio ya maisha ni mitindo mibovu ya maisha.

Uzi muhimu sana huu
 
Mada yako ni nzuri ila umeandika kama vile mtu unayeishi ulimwengu wa kwanza
Kimsingi kumpa mtoto chakula na malazi ni jukumu la msingi la mzazi wala huna haja ya kulipuuzia;
na ukumbuke wapo wazazi wengi tu huku ulimwengu wa tatu hawana uwezo wa kutimiza jukumu hilo.
Ila ni kweli pia kuwa, Jukumu la Mzazi lisiishie kwenye kumpa chakula na malazi; liendelee mbele kwenye
kumpatia mtoto Elimu bora na malezi mazuri kwa ujumla
 
_20231116_101309.JPG
 
Back
Top Bottom