(Wakina baba tu) - Upo busy na kazi? Haya ndiyo malezi anayopewa mwanao wa kiume

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Kabla hatujaendela hapa; nikupe pole na hongera kwa kazi kama baba, kwa sababu uzi huu ni mahsusi kwa ajili yako. Karibu.

Tumuangalie mtoto wako wa kiume, nimelenga huyo kwa sababu yupo kwenye hatari ya kupotea, sio yeye kama kiumbe, hapana; ila ni yeye kama Mwanamume. Uanamume unaanzia kwenye maumbile yake, lakini kijamii uanamume haushii hapo. Kuna majukumu yanamuita kutokana na uwezo asilia wa jinsia yake. Majukumu haya hayafundishwi kwa kuambiwa, bali kuona. Ila tazama hapa chini ratiba ya mtoto wa kiume wa leo kwenye familia nyingi.

Asubuhi Wewe na Mkeo mnatoka, naam, mnaenda kutafuta. Lakini kwenye mchakato wa kujiandaa nina hakika mkeo au dada wa kazi ndiye anayemuamsha mwanao kujiandaa na shule, wanamuogesha na kumpa breakfast, kisha mkeo anarudi kwako kukuandalia maji (kama bado mahaba yapo) ukaoge; safari ya mwanao inaanza.

Hapa nazungumza sana na wewe ambaye mwanao yupo shule ya Msingi, ambapo walimu wa kike ni wengi zaidi kuliko wa kiume; kule atafundishwa na hao, na kama yupo day care atafunzwa kila kitu, ila katika haiba ya kike. Kwa sababu, mwanamke hamfundishi mtoto wa kiume kuwa mwanamume.

Baadae anarudi kutoka shule, msichana wa kazi anamuogesha kuondoa uchovu, naam anamuogesha sio mama yake, mama katoka. Akimaliza dada anamuandalia chakula, anakula na kwenda kupumzika, akiamka anacheza (kama anaruhusiwa), ingawa kuna wale waliofungiwa ndani. Baada ya hapo dada anamuita arudi nyumbani, wakati huo mama akikaribia kurudi.

Baadae mama yake, yaani mkeo anarudi kazini, anakagua kama mtoto kafanya homework, akimaliza atashinda nao kwa muda, kwa kuwa nae atakuwa amechoka atamwambia dada amuandalie chakula na watoto. Baada ya kuoga watakula, wakimaliza ni kwenda kulala; kisha wewe ndiyo unarudi.

Siku nzima mtoto wako wa kiume amelelewa ndani ya ulimwengu wa kike, na kama alienda kucheza huko nje ni na watoto wenzie ambao kimsingi hawawezi kumjenga kwa namna yoyote kifikra au kimaadili. Upo?
 
KItabu chako kitasababisha wababa waanze kuwaogesha watoto?
Jibu ni hapana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom