Unaingiaje ofisini kwa mwenza
wako kama chooni? Kwa walinzi na
reception unasema una shida
gani?[/qoute]
Duh.... mbona dillema??? Ngoja niwaite hawa waongezee michango yao, wapi Mzee
Mtambuzi, vipi mama Ngina akija hapo kazini kwako ghafla akakuta unamhug kimwana????
Dada mkubwa
gfsonwin na
snowhite hebu tupe uzoefu wako katika hili.....
Kaka
HorsePower sema neno na roho yangu itatulia.......
charminglady asante kwa mwaliko.
Kwanza nikubali kuwa utani upo sana makazini na kwa namna fulani husaidia kuondoa stress za kazi na kuigeuza sehemu ya kazi kuwa ni sehemu ya furaha pia! Lakini inapokuja suala la utani hasa utani uliopitiliza kwa wale wenye ndoa ni vyema kuwa makini na kuweka mipaka kama alivyoongea Mwl
gfsonwin. Mume/mke wa mtu ni vyema kuepuka utani wa kufikia hatua ya kuegamiwa au kushikwashikwa au kutembea mmeshikana viuno nk nk na mfanyakazi au rafiki wa jinsi tofauti. Kwa vitendo hivi, endapo mmoja wa wanandoa atavamia ofisi kwa sababu yoyote ile, inaweza kuleta mtafaruku ndani ya ndoa.
Kuhusu suala la mwenza kumtembelea mke/mume ofisini sioni tatizo, maana naamini atapelekwa hapo ofisini kwa shida maalumu. Inaweza kuwa wanashare gari na hivyo wanahitaji kupitiana au kuna dharura yeyote ambayo inahitaji kujadiliwa ana kwa ana, au mmoja wapo wa wanandoa hao alisahau kitu hivyo mwenzi wake kaamua kumpitishia ofcn nk nk. Sioni tatizo ktk hilo, maana pia kitendo cha kukubali kuingia kwenye ndoa maana anasa na tamaa zingine umeamua kuzikata na hivyo unapaswa kubehave kama mwanandoa ili mwenza wako akikukuta sehemu yoyote au ndg zake au marafiki zake, asije akafikisha ujumbe mbaya kwa mwenza wako na kuhatarisha ndoa.
Kwa kifupi, ukiwa kwenye ndoa ni sawa na mnyama anayewindwa porini, ni vyema kuwa mwangalifu kila wakati na kuepuka matendo yote ambayo jamii, marafiki au ndg wanaweza kukutafsiri tofauti, Utani wa kawaida na hata kumu-hug mtu si mbaya ila usizidi hapo!