SoC03 Kumbuka kuwa na shukrani mara kwa mara, utaona faida kama hizi

Stories of Change - 2023 Competition

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Shukuru umeiona tena hii weekend.
Shukuru safari zako za wiki zilikua salama.
Shukuru kwa ulichojaaliwa kupata kwa wiki, hata kama ni kidogo.

Shukuru kwa kuwa upo salama sasa, japo sjui unasoma tokea wapi (unasoma tokea wapi?), lakini unasoma ukiwa salama.

Shukuru kwa mambo mengi mola aliyokuwezesha. Na utaendelea kupata baraka zaidi ili upate vitu vingi vya kushukuru zaidi.

Japo mwanzoni unaweza kuona huna cha kushukuru, lakini ukiangalia vizuri utagundua una mengi ya kushukuru kuliko unavyodhani.

Mfano, unapumua vizuri, umepata msosi jana na juzi, unaona vizuri, una mahali pa kumpumzika na una marafiki wanaokusaidia.

Hivyo vitu tunavichukulia poa, lakini wapo ambao wanavitamani hata kwa sekunde moja.

Chukulia mifano hii,
Kwa mfano una una mtu wako wa karibu, kila unachompa/ kumfanyia anakushukuru kwa moyo. Anakushukuru vizuri kwanza alafu baaaadae ndo anakuambia bhana kile ulichonipa kina upungufu huu na huu/ au ningependa kiwe hivi au vile. Au asikuambie kitu kabisa. Kiasi kwamba kila unapompa/ kumfanyia kitu unajisikia amani moyoni.

Unaona unachokifanya kina thamani. Yani anathamini kujitoa kwako.

Na upande mwingine, una mtu wako wa karibu, kila unachompa/ kumfanyia anaanza na lawama/ malalamiko na kukusema juu. Atakuambia mapungufu ya kile ulichomfanyia au kwanini usingempa hiki au kwanini asingemfanyia hiki kingine. Muda mwingine utasikia “ah! We kila siku unanipa icho icho tu, nshachoka mimi”
Moyoni utajisikia ukakasi. Utaona hathamini hicho unachojitolea kwake.

Kati ya hao wawili yupi utakua tayari kumpa kitu/ kumfanyia kitu tena? Yupi utapenda uwe naye karibu? Yupi utakua unamfanyia vitu kwa furaha na sio kumpa ilimradi?

Na Mungu ndo hivyo hivyo. Kuwa mtu wa shukrani na utapewa vingine vya kushukuru zaidi na zaidi. Sababu anajua utamshukuru tena na tena badala ya kumlalamikia.

Kinyume cha shukrani ni malalamiko na lawama.
Ukiona unalalama sana ujue huna shukrani vile inavyotakiwa.
Na unajikuta unaendelea kupata vitu vya kulalamikia zaidi, sababu hivyo ndo unavyojiombea.

Hili likae sawa, kutoridhika sio kinyume cha kuwa na shukrani.
Wala kuridhika sio kielelezo cha shukrani.
Shukuru kwa ulichopata ila usiridhike kwa ulipoishia ili usonge mbele zaidi.

Kutoridhika maana yake matamanio ya kusonga mbele zaidi. Ile hamu uliyonayo kupata mafanikio zaidi ndo inakusukuma usonge mbele zaidi. Maana yake hujaridhika na sehemu uliyopo.
Ukiridhika maana yake umekubali kubaki hiyo sehemu uliyopo.

Ni vile tu sisi tunayatumia vibaya maneno yetu. Lakini kutoridhika sio jambo baya, ila kutokua na shukrani ndo balaa.

Angalia hii pia, chukulia maombi yako ni kama maboksi alafu maombi yako yanapofikia ni kama kichumba. Kadri unavyozidi kuomba unazidi kuyajaza maboksi kwenye hicho chumba. Mengine unayabananisha na mengine mpaka yanachanika. Mengine yanakosa nafasi, kwaiyo hayafiki hata kwenye icho chumba cha kutendewa.

Alafu shukrani maana yake kusafisha chumba ili upate nafasi ya maboksi mengine. Kadri unavyozidi kushukuru unazidi kupunguza maboksi yasiyo na msingi tena kwenye hicho chumba ili upate nafasi ya maboksi mapya.
Kadri unavozidi kushukuru chumba kinakua chepesi pia na maombi yako yanaonekana kirahisi.

Natumaini umenielewa hapo, ndo mana shukrani ina faida sana kama hivi.

Ni rahisi kupokea tena.
Utazidi kupata. Utazidi kujaziwa.
Mtu anayeshukuru ni rahisi kupewa tena. Ndo mana hata tulipokua wadogo tulikua tunalazimishwa kushukuru. Tulifundishwa kushukuru.
Unamfanya anayekupa awe na moyo wa kuendelea kutoa kwako.
Lakini malalamiko/ lawama zinamfanya ajione mjinga kukupa. Na ataacha.
.
Ni rahisi kuwa na amani hata kama mambo yanaenda mrama.
Kama nlivoeleza hapo juu, shukrani inasafisha. Shukrani inaosha majonzi uliyonayo. Inakufanya ujisikie mwepesi rohoni.

Utakuwa haungalii mambo yanayoenda vibaya, bali unaangalia ambacho tayari kinakupa furaha, ambayo tayari umeyapata na ambayo tayari yanakupa amani moyoni.

Ukiona mpenzi wako hakupi amani, anza kuangalia vitu vinavyokupa furaha kwanza, pengine una watoto wanakupa furaha au familia yako. Ayo tayari Mungu ameshakujalia. Badala ya kwenda kumlalamikia kila saa kwanini mpenzi wako hakupi amani.

Kila mtu anataka amani ya moyo. Shukrani ni sehemu ya kuanzia.
.
Unajitenga na lawama, chuki na malalamiko.
Lawama na malalamiko lazima yakutengenezee chuki moyoni mwako.
Moyo wako unasuuzika kwa yote uliyonayo badala ya kuangalia ambavyo huna.
Kuwa mtu wa lawama maanake umechagua kutokuona uliyojaliwa na Mungu na kwa makusudi unaangalia yale yote yanayokufanya ulalamike tu.
Kulalamika sio vibaya, ubaya unaanzia pale unapolalamika kila siku, kila saa, kwenye kila kitu.
Ukipata kitu unaanza na kusonya kwanza, apo unakua umelaumu hata kabla hujafungua mdomo.
Ukiona maombi yako yanatimia kwa manati sana, anza kuangalia kama unalalamika mno kwanza kabla ya kubadili staili/ sehemu ya kuomba.

Pia Nakushukuru Kwa Kuwa Nami Hadi Leo Hii.
 
Back
Top Bottom