Kuwa na shukrani kwa ulicho nacho

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,098
12,473
Nawasalimia kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kazi iendelee zisisimame.

Maisha ni fumbo kubwa sana ambalo kila mtu anajaribu kulitatua kwa upande wake kutokana na mazingira husika na mahitaji yake.

Kwenye maisha kila mtu huwa anatamani kitu fulani lakini hata anapokipata bado anahitaji kingine cha juu zaidi ya alichonacho, nakwambia kuwa na shukrani kwa ulicho nacho kwasababu kuna wengine wanatamani hata robo ya ulicho nacho ila hawana wakati unatamani vya juu zaidi na kutothamini ulivyo navyo kumbuka haya.

1.Kuna watu wapo kwenye ndoa miaka mitano wengine zaidi ila hawaja jaaliwa hata mtoto mmoja wewe mungu amekubariki mwaka wako wa kwanza tu wa ndoa kuwa na shukrani.

2.Ulivyo maliza chuo tu umepata kazi wakati kuna watu wana miaka mitano na zaidi hawana ajira tangu wamalize chuo na wengine hata interview wanaisikia tu kwa nini usishukuru kwa mungu wako kwa neema aliyokupatia.

3.Una nguvu una afya njema kuna wenzako wapo kitandani miaka mitano na zaidi lakini wanaamini ipo siku MUNGU atawafanyia miujiza na wataendelea na mapambano wewe una afya njema kwa nini unakosa shukran hata kidogo.

4.Kuna wenzako wanalala nje kila siku na hawaijui kesho yao wala hawana uhakika wa chakula wewe unakula chakula chochote unachotaka na unalala sehemu nzuri kwa nini unakosa shukran.

5.una kazi nzuri una familia na watoto na mke mzuri kwa nini unakosa shukran wakati kuna wenzako umesoma nao umekuwa nao lakini hawana robo ya mafanikio yako kwa nini unakosa shukran.

6.unapitia changamoto kwenye kazi unataka kuacha unapitia changamoto kwenye ndoa unataka kuachana na mwenza wako mliezaa pamoja kumbuka hakuna mtu kwenye dunia hii, ambaye hana kitu kinachomkosesha furaha hata kina bakhresa kina mo dewji kina Jack ma kina Elon musk na wao wana kitu kinawanyima raha ni vile tu hawaonyoshi kwa hyo hamna ambaye yupo kwenye mgongo wa ardhi hii anayekosa changamoto narudia hayupo tafakari kabla ya kufanya maamuzi yako.

7.Wasaidie ndugu zako na watu wakaribu wenye uhitaji hyo ndio njia pekee ya kukufanya kuwa happy kuwa na gari kuwa na kazi na cheo hakukufanyi uwe happy shukuru kwa ulicho nacho hakuna aliyemaliza kila kitu kwenye hii dunia wote tutaacha mission incomplete mshukuru mola wako kwa ulicho nacho wataalam wanasema happiness is contagious or relative.

8.umekata tamaa kwasababu huna kazi hujaanzisha familia na mda umefika wa kufanya hvyo shukuru kwa mola wako kwasababu bado una afya njema ambayo ndio msingi wa kila kitu siku moja MUNGU atakuona na atakuinua maana sio kila unachokosa ulistahili vingine havina kheri na wewe kuwa na shukrani.

9.MUNGU ndio anayepanga kila kitu wapo waliopewa walivyotamani vikawaletea shida na wapo walionyimwa walivyokuwa wanataka na baadae wakajua havikuwa na kheri wakapata vya juu zaidi hvyo shukuru kwa kila kitu wakati utafika MUNGU atakuinua tu .

10.Mwanadamu yoyote amejawa na tamaa mpaka umauti una mfika hivyo hata hao ambao unatamani maisha yao na wao pia kuna mda wanatamani maisha yako kwasababu ya changamoto mbalimbali hvyo kuwa na shukrani kwa kila kitu maana MUNGU ndio anajua hatma yetu sote hivyo kuwa na shukrani japo kidogo.

YOU OWN NOTHING AND NOTHING SHOULD OWNS YOU WE ALL POSSES CERTAIN FORTUNES IN OUR LIFE DESPITE HAVING ALL WE'RE NOT HAPPY.

WHAT BELONGS TO YOU TODAY BELONGS TO SOMEONE YESTERDAY AND WILL BELONGS TO SOMEONE TOMORROW YOU OWN NOTHING.

DON'T GIVE A https://jamii.app/JFUserGuide TO ANYTHING.

ALAMSIK.
 
Hili nalo neno.

ASANTE KWA BANDIKO LENYE VIASHIRIA VYA UKOMBOZI KWA WANAJF.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom