Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,627
Wanabodi,
Huu ni wito kwa Watanzania tujifunze kuwa ni watu wa shukrani, tuwe na shukrani kwa kwa madogo ili tupatiwe makubwa!. Je tujifunze kuwa na shukrani kwa madogo ili tupatiwe makubwa!. Japo tulitaka kikubwa, Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, tumepewa kiduchu tuu!, je tukipokee tushukuru, au tususe na kuendelea kudai kikubwa?.
Mtu ukiwa na shida fulani kubwa, mfano una dharura unahitaji shilingi milioni, ukabisha hodi kwa majirani, ndugu, jamaa na marafiki kuwaomba milioni, kila unae muomba hana hiyo milioni, anakuambia nina laki, kwa vile shida yako ni milioni, hiyo laki haiwezi kusaidia kitu, je utaacha kuipokea hiyo laki na kuendelea kutafuta milioni?, au utaipokea hiyo laki na kushukuru, kisha utaendelea kutafuta ile milioni ambayo sasa ni laki tisa!.
Huu ni wito kwa Watanzania haswa vyama vya siasa, wadau wa demokrasia na wanaharakati, najua mnataka katiba mpya, tume huru na shirikishi ya uchaguzi na sheria nzuri ya uchaguzi yenye kutoa haki kwa kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa, nawasihii pokeeni hiki kidogo mlichopewa, shukuruni kwa kidogo, kisha endeleeni kutafuta hicho kikubwa!. Haba nah aba hujaza kibaba!. Safari ni hatua, huu ni mwanzo.
Pongezi Rais Samia kwa Mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi, Tanzania kitu inachohitaji kwanza ni mabadiliko ya katiba ndipo tuje kwenye mabadiliko ya sheria, maadam sasa tumeletewa mabadiliko ya sheria, tuyapokee, tushukuru kisha tuendelee kuomba mabadiliko ya katiba ili yaendane na mabadiliko ya sheria hizi.
Nimeianza makala ya leo kwa kusisitiza umuhimu wa kuwa na shukrani kwa madogo ili upatiwe makubwa, kwasababu kilio kikubwa cha demokrasia yetu nchini Tanzania, ni kilio cha katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025.
Lakini muda ulibaki kufikia 2025 ni muda mfupi kwa mchakato wa katiba mpya, hivyo serikali yetu sikivu ikaona tuanze na mabadiliko ya sheria za uchaguzi na Tume ya Uchaguzi.
Kwavile tulichokitaka ni kikubwa, tumekikosa tulichokitaka hivyo tupokee kwanza hiki kidogo kilichopatikana na kushukuru kwa kusema asante, kisha tuendelee kuomba kile kikubwa tunacho kiomba na kukihitaji.
Kwenye safu hii, nimeandika zaidi ya mara 10 kuhusu hitaji la katiba mpya, mabadiliko ya katiba, sheria ya uchaguzi na mambo ya demokrasia.
Baadhi ya mada zangu ni hizi
"Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria"
" Fupa hili la katiba, lililowashinda wanaume wanne, jee mwanamke mmoja ataliweza?"
"Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa?"
"Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Je Rais Samia Ataliweza ?.
Sasa jana Ijumaa ya tarehe 10 November, 2023 ni kama siku ya ukombozi mpya fulani kwenye demokrasia ya taifa letu la Tanzania, kuanza kulishungulikia Lile Fupa la katiba Lililowashinda Marais Wanaume 4 kwa kipindi cha miaka 40!, Rais Samia, ambaye ni rais Mwanamke mmoja, ameonyesha ushujaa mkubwa ndani ya awamu yake ya sita, akiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili tuu na miezi kadhaa, kuileta hii miswada mitatu ya ukombozi mpya wa demokrasia ya taifa Letu, imetua Bungeni Dodoma.
Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo japo ni tume huru, haikuwa shirikishi, sasa tunakwenda kuunda Tume Huru zaidi ya Uchaguzi ambayo itakuwa shirikishi zaidi kuliko tume iliyopo.
Pia Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kurekebisha kasoro mbalimbali kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Miswada hiyo tayari imeisha somwa Bungeni kwa mara ya kwanza, na tayari iko wazi kwenye tovuti ya Bunge.
Hatua ya pili ni kwa wadau kutoa maoni yao kuhusu miswada hii kwa kipindi cha miezi 3, halafu kikao cha Bunge cha February 2024 itasomwa kwa mara ya pili ikiwa imejumuisha maoni ya wadau, kisha kujadiliwa na Wabunge, ndipo ipitishwe.
Hivyo hiki kitendo tuu cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ya Rais Samia kuboresha demokrasia nchini, anastahili pongezi za dhati na pia kuendelea kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko hata wanaume kwenye baadhi ya maeneo.
Kwa vile tulichotaka sicho tulichopewa, tulitaka kikubwa tumepewa kidogo, tukipokee na tuna miezi mitatu ya kukijadili, tuendelee kuomba kile kikubwa na huwezi jua labda hata ile hoja yangu ya " Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!" inaweza kupatiwa ufumbuzi kwa Rais msikikivu Mama Samia, mara ghafla akatuletea maji ya kunawa kwa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ndipo tubadilishe hizi sheria.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali