[emoji3544]Wakiwa Wamekaa Ndani Mara Ghafla Msaidizi Wake Akajaa na Taarifa Hizi MBAYA...

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Umeme Umekatwa (Bill Imekuwa Kubwa Sana)

Printer Imekufa Ghafla

Maji Yamekatwa

Mwenye Jego yuko Getini Anasubiri KODI Yake huku ana hasira balaa

...Hii ilikuwa Miaka ya 90's...

Ndani ya Jiji la California Nchini Marekani, Nyumbani na Ofisini kwa Nguli mmoja wa Direct Response Marketing...

Anayeitwa... "Gary Halbert"

Kabla Sijakwambia nini Kilitokea pale Nyumbani, Ngoja kwanza nikwambie...

Direct Response Marketing ni Nini...

Na...

Huyu Gary Halbert ni Nani hasa...

Kama Hufahamu tu, Direct Response Marketing ni...

Aina ya Marketing inayoandaliwa kwa Lengo la kumfanya Mteja achukue hatua flani Iliyokusudiwa kwa haraka zaidi

Na Direct Response huwa na Malengo Makubwa mawili..

1). Ni Kuwafanya walengwa wachukue hatua kwa haraka zaidi kama Mlenga (Marketer) anavyotaka

2). Kuikuza na Kuitambulisha Brand ya Mtu au Kampuni flani

Na Mfano Mzuri wa Direct Response ni...

Matangazo yote Unayokutana nayo kwenye...TV, Redio, Magazeti, Barua (Direct Mail) na Social Media zote

Yaani hayakwambii Ununue Kitu flani bali Yanakwambia Uchukue hatua flani, Mfano Uweke...

Email yako

Namba yako ya Simu

Ufanye Sign Up

Ufanye Registration flani

Au...

U–share Link kwa Kuwatumia watu kwenye Namba zako

Kwa Ahadi ya kwamba Utapata Kitu flani baada ya kufanya hivo

Kama Umeshawahi Kukutana na Zile Link uki Share kwa watu 10 Mfano Unapata..."FREE Mb's Bundle"

Huo ni mfano ulio UCHI Kabisa ambao naweza kukupa na Ukanielewa Vizuri kuhusu Direct Response

Kwahiyo kwa Ufupi tu hiyo Ndio Direct Response Marketing aliyokuwa akifanya...Gary Halbert!

Unaweza Kujiuliza na Gary Halbert ni Nani Sasa?..

Kwa Ufupi tu...

Gary Halbert... Ni marketer na nguli wa Copywriting duniani aliweza kutengeneza zaidi ya dollar billioni moja za ki Marekani...

Kwa kuuza bidhaa na huduma mbalimbali kupitia..."Direct MAILS"

Bila shaka hadi hapo Utakuwa Umenipata Kidogo Ninaposema...

Direct Response Marketing ni nini na Gary Halbert ni nani au Sio?..

Yeah Vizuri

Turudi kwenye Story yetu Sasa...

...Wakati Msaidizi wake analeta Taarifa hizo MBAYA, Gary alikwepo na Mke wake sebleni

Gary Akamjibu Msaidizi...

"Nashukuru, Unaweza Kwenda Kuendelea na kazi Ofisini kwako"

Kisha Mke wake akamshika Mkono wa kushoto Gary huku akimvuta taratibu hadi Chumbani kwao

Kisha Akamwambia kwa upole...

"Gary... Kama umeshindwa Kufanya hiki kitu ili Kitupe Kipato ndani ya wiki moja, Basi fanya uende ukatafute kazi ya Kujishikiza"

Unajua Gary alifanyaje baada ya maneno hayo kutoka kwa Mke wake?..

Angalia Hapa

Gary alimwambia Mke wake Maneno haya kwa uchungu...

"Nakupenda Mke Wangu"

Halafu taratibu akamshika nywele kichwani kisha Akambusu juu ya Komwe...

Kisha akatoka kuelekea kwenye chumba kilichokuwa ni Ofisi yake.

Kumbuka...

Hapa Gary Halbert alikuwa hana Chaguo lolote zaidi ya kuendelea kufanya kilichopo Mkononi kwake.

Kwasababu...

Hakuna Kibarua angepata kwa haraka kiasi kile na Kiweze kumpa Kipato cha Kulipa Bills zote zile

Ndio maana kuna Msemo napenda kuwaambia watu kwamba...

"Hakuna muda Mgumu wa kuitafuta PESA Kama kipindi Ukiwa na Shida nayo"

(Rudia Kusoma Tena Hiyo)

Kwahiyo chaguo lilikuwa ni moja tu...

Akae chini aendelee kuandika zile Mails (Barua) kwa walengwa wake.

...Akiwa Ofisini kabla hajaanza kuandika chochote kile...Gary Alijiuliza swali moja kichwani kwake kwamba...

"Vipi kama kuna Mtu kaja kaniwekea Bastola Kichwani na Ili asikatishe UHAI wangu Inabidi niandike hii Mail ambayo Italeta Matokeo...

Je Ningefanya kazi kwa UBORA wa Kiasi gani?"

Kisha mwanaume akaa chini kwa Masaa sita akiandika Barua (Mail) ili aitume kwenda kwa walengwa wake

...Na mpaka jioni tayari Gary alikuwa kishapata Pesa za Kulipa Bills zote alizokuwa akidaiwa

Na...

Mwisho hiyo Barua ilikuja kuwa ndio moja ya barua bora zaidi kuwahi kuiandika na kumtengenezea Mapato ya...

Zaidi ya dolla za ki Marekani Billioni moja... Yeah It's One Billion Dollar

Na...

Baada ya Mafanikio hayo Gary akaipa hii Strategy jina la...

"Gun To Your Head Marketing"

Yaani akiwa na Maana ya kwamba...

Katika kila kazi yako Unayofanya kila siku hakikisha na ashumu kwamba kuna

Mtu yuko pembeni yako kakushikia Bastola kiasi kwamba ukifanya kazi Mbovu basi anapita na Ubongo wako

Hiyo Itakufanya kila unapofanya kazi Uwe makini na utoe kazi Nzuri kuliko Iliyopita

Kwa sababu...

Ukweli ni kwamba Binadamu huwa anaonesha Uwezo wa mwisho alionao kwenye hali ya...

Presha na ambayo hakuna Chaguo lingine lolote zaidi ya kufanya kazi Iliyopo Mezani

Ndio maana Mtu ukimpa Deadline ya Kazi yoyote Ile atafanya kila kila namna aimalize kwa wakati.

Na...

Hiki Kitu KIMOJA Ndicho Kilichomfanya Gary Halbert kuwa Miongoni mwa Nguli wa Direct Response Marketing na Copywriting

Kama utapata Nafasi Katafute hizo Direct Mails zake halafu uone kazi alizokuwa akifanya

Kila Kazi Ilikuwa ni...Msiba (Nzuri)!

...Nadhani pia Kitu pekee ambacho unachoweza kujifunza kutoka kwenye hii Strategy ya Gun to Your Head Marketing

Kama Wewe Ni...

Graphics Designer

Producer

Photographer

Artist

Musician

N.k..

1). Siku zote unapopewa kazi na Mteja wako hakikisha Unafanya kwa uwezo wako wa Mwisho hata kama Itakuchukua muda mrefu lakini hakikisha kazi haitoki mbaya

Kazi NZURI Itajitangaza Yenyewe Lakini Kazi Mbaya hata ukiitoa Bure hakuna Mtu ataishobokea

Pia Kazi Nzuri hakuna Mshindani wako anaweza Kuiiga hata mara moja

2). Kwenye Biashara yako...Wewe ndio mtu pekee ambaye unajua Pesa Inatengenezwa Vipi

Kwahiyo hakikisha FOCUS yako yote Iko kwenye Kutengeneza Pesa

(Jilinde Wewe na Vitu Vibaya vyote Kwa sababu wewe Ndio Rasilimali Muhimu kwenye hiyo Biashara)

Kwahiyo Ili Kuwa na Biashara Makini hakikisha unatumia hiyo Strategy ya...

"Gun To Your Head Marketing"

By the way...

Kama Unahisi Umejifunza Kitu na Ungependa nishushe Madini mengine Mengi kama haya basi...

Reply Neno..."MADINI"

Hapo kwenye Sehemu ya Comments Chini

I Hope Umejifunza Kitu Kipya.

Uwe na Siku Njema!

Gracias

Seif Mselem
 
Kama thread zako huwa ziko fresh sana ila mimi huwa sielewi namna ya uandishi wako. Mpangilio wako aseeh kuna muda unachosha. Basi atleast kila paragraph iwe na mistari minne mpaka mitano.

So far huwa najitahidi sana kusoma haya madini na ni madini kweli
 
Back
Top Bottom