Kumbe Watanzania Wana Uwezo Kuwa Mabilionea, Walikosa Mitaji na Mbinu!. TotalEnergy Mkombozi, Yamwaga Fursa za DODO Nchi Nzima!. Tuchangamkie Fursa?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za "Kwa Maslahi ya Taifa". Tanzania sio masikini, Tanzania ni nchi tajiri sana yenye Rasilimali lukuki, ila watu wake ni masikini Kwa Umasikini wa files. "Umasikini m-mbaya kabisa ni umasikini wa fikra"-JK Nyerere.

Nimegundua kumbe Watanzania wengi tuu, Umasikini wao ni Umasikini wa fikra, wakielimishwa kubadili mind set, na kujengewa uwezo wa kimitaji na mbinu za biashara, Watanzania wana uwezo mkubwa wa kumiliki uchumi wetu na kuwa mamilionea, na mabilionea!, kitu pekee walichokosa ni mitaji na mbinu za kisasa za biashara.

Kampuni ya TotalEnergy, kwa kukiambia hili, ghafla imekuwa ni mkombozi wa Watanzania kwa kuwajengea uwezo wa elimu biashara na kutengeneza mamilionea, watakaokuwa mabilionea!, wamemwaga fursa za kitu kinachoitwa DODO kwa nchi nzima!. Jee Watanzania tuchangamkie hizi fursa za DODO tuwe mamilionea, au tuendelee na umasikini wetu wa fikra kuwa utajiri ni kwa matajiri tuu, sisi ni masikini tuendelee na umasikini wetu? au tubadilike, tuchange mind set zote tuachane na mawazo ya kimasikini tuchangamkie Fursa?.

Kujua zaidi kuhusu fursa za biashara ya mafuta, karibu mitaa hii

Kila binadamu anazaliwa mtupu, bila kuja na kitu chochote hapa duniani, na siku anaondoka, anaondoka mtupu kama alivyozaliwa, hata akizikwa na jeneza la thamani gani, na kushehenezwa na vito vya thamani, dhahabu, almasi na vito, vyote vitaishia tuu pale kaburini, na kasha tuu la mwili, lakini mwenyewe anakuwa ameisha ondoka na haondoki na kitu chochote!.

Hivyo wote kama tumezaliwa watupu, utajiri na umasikini ni vitu tunavyovikuta hapa duniani na tutaviacha.

Kuna aina 5 za matajiri na utajiri, na aina 5 za masikini na umasikini, na umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra.
Aina 5 za Utajiri na Umasikini
  1. Utajiri wa Kurithi- The Best Inheritors, umezaliwa kwenye familia tajiri, hivyo tangu unazaliwa wewe ni tajiri tayari, hata usipojishughulisha na jambo lolote, wewe utaishi vizuri kitajiri mpaka siku unakufa, wanaita umezaliwa na "silver spoon". Na ukizaliwa kwenye familia masikini wa kutupwa, mtaji wa masikini ni nguvu zake, usipofanya juhudi zozote kuibadili hali hiyo, au usipokuwa sehemu ya makundi manne haya yanayofuatia, then for sure, unazaliwa masikini na utakufa masikini!.
  2. The Best Talents- Hawa ni wale wanaozaliwa na kipaji. Hata kama umezaliwa kwenye umasikini lakini una kipaji, ukikitumia vizuri kipaji chako, kinakuletea utajiri, hawa ndio kina Michael Jackson, hakusoma hata darasa moja, Diamond Platnum aliishia darasa la 4!. Kwenye kundi la the best talents kuna wasanii, wanamichezo, wanamuziki wachoraji, waibaji, actors, etc. Na sisi Waandishi wa habari na Watangazaji tuko kundi hili. Kila mtu anazaliwa na kipaji fulani, ila wengi hawajitambui, hivyo wanakuwa masikini kwa kutokujitambua na kutumia vipaji vyao.
  3. The Best Brains- Hili ni kundi la wale bright, brilliants, genius, wenye akili nzuri, wanafanya vizuri darasani, wana score high, hivyo ku attract top jobs, kulipwa vizuri top salaries na hivyo kuishi vizuri, ma scientist, ma profesa, wasomi ndio kundi hili. Ila pia kuna wenye best brain ya akili tuu za darasani na kuajiriwa kulipwa mshahara, lakini hawana akili za maisha, hivyo baada ya kustaafu, maisha yanawapiga sana!.
  4. The Hard Workers- Hili ni kundi la wafanyakazi kwa bidii, watu wanaojituma, wanatumia efforts zao na muscle powers zao kutoka jasho na kula kwa jasho lao, hivyo wanafanikiwa. Ukifanya kazi kwa bidii kwa kujituma, na kuwajibika, utafanikiwa, lakini ukipiga uvivu, lazima tuu utakuwa ni masikini wa kujitakia.
  5. The Fixers, hili ni kundi la watu wanaoendesha maisha yao kwa mishe mishe, they are well connected, they are not the inheritors, hawana talent yoyote!, they are not the best brains, wengine ni vilaza, they are not hard workers, but they have the best life. Kundi hili ndilo lenye wanasiasa na matapeli pia. Kwenye kundi hili kuna the lucky ones wenye bahati, wanapata connections, na channels, wanapiga pesa ndefu na wanakuwa mamilionea na na mabilionea. Hawa the lucky ones, baadhi yao wana kitu kinachoitwa "The Midas Touch" everything they touch turns to gold wengine wanasemekana wanatumia 'kizizi'!. The unlucky ones ni wasio na bahati, kila wanachofanya kinakwama, kinaishia njiani au kikifika mwisho hakizai matunda, hawa wanasemwa kuwa na damu ya kunguni, hata ukiwapa ng'ombe, akizaa, anazaa dume!.
NB. Kwenye makundi haya kuna baadhi wanaingia kote, they are the best inheritors, anatoka familia bora hivyo anasomeshwa best schools money can pay kama Mo Dewji, hivyo anakuwa ni best brain, wengine pia wana vipaji, halafu wanafanya kazi kwa bidii na kujituma, kisha anajiunga na kundi la ma fixers kwa kuingia Bungeni just to get connections ili kuwa connected, kama kina Mo, Rostam, Sumri, Abood, Mkono etc.

Idadi ya Watanzania tunakwenda kufikia milioni 60!. Kati ya hawa kundi kubwa zaidi ni la masikini wa kutupwa wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea.

Ili tuendelee tunahitaji vitu 4, Land, labor, capital na entrepreneurship. Tanzania tuna land ya kutosha, tuna watu wenye nguvu, tumekosa capital na entrepreneurship. Umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra, umasikini wa mawazo ya kimasikini kuwa sisi ni masikini. Utafiti wangu binafsi umebaini Watanzania wengi ni watu wenye uwezo mkubwa, na wanamiliki ardhi ambayo ni mali, lakini hawana mbinu na mitaji.

Kampuni ya mafuta ya Totalenergy Tanzania, kwa kulitambua hili, kupitia mpango mkakati wake uitwao DODO, wameamua kuwajengea uwezo Watanzania kumiliki vituo vya mafuta
Screen Shot 2022-05-29 at 2.52.17 PM.png
Screen Shot 2022-05-29 at 2.52.50 PM.png

Watanzania Tuna Uwezo wa Kuwa Mamilioneo na Mabilionea, Tatizo ni Mitaji na Elimu ya Biashara yaani entrepreneurship.

Naendelea na zile makala zangu elimishi kwa Maslahi ya Taifa, kwa kuuliza maswali ambayo yakipatiwa majibu mujarabu, yatalibadili taifa kutoka hapa tulipo, na kupiga hatua mbele zaidi kimaendeleo.

Kunapotokea tatizo mahali, ili kulitatua hilo tatizo, hatua ya kwanza ni kulitambua tatizo, kukijua chanzo cha tatizo, kujua ufumbuzi wa tatizo hilo, na mwisho kuchukua hatua za kulitatua au kulifumbua.

Tukubali, tukatae, mfumo wetu wa elimu una matatizo, tunafundishwa elimu ya nadharia kwa kutumia modali za wenzetu ambayo imewajenga wasomi wetu kuajiriwa na sio kujiajiri au kujitegemea.

Mfumo wetu wa elimu, hatufundishiwi kutatua changamoto zetu bali ni elimu ya nadharia kubwa, lakini vitendo vichache.

Mfano Tanzania tuna elimu ya Fasihi, (literature), hadi Chuo Kikuu, tuna maprofesa wa Ph.D za fasihi makumi kwa mamia kutoka vyuo vikuu vyetu, toka miaka ya 60. Mimi nimesoma fasihi sekondari hadi Chuo Kikuu, hakuna hata kitabu kimoja cha fasihi kilichoandikwa na maprofesa wetu ambacho kilitumika kufundishia, vitabu vyote ni vya waandishi kutoka nchi za wenzetu!. Vitabu vya karibu ni ni vya majirani zetu wa Kenya, Ngungi wa Thiong'o, “The River Between” na Okot T’Bitek “Song of Lawino”, lakini tumefundishwa literature za Chinua Achebe “Things Fall Apart” na kina Henrik Ibsen “An Enemy of The People”, wote hawa ni waandishi wa nje, hivi hao wasomi wa Literature wa vyuo vyetu vikuu, wako wapi?!. Jibu ni wasomi wa nadhariia tuu!.

Nikiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), nilikuwa natembelea maktabu kuu ya UDSM, (ukiwa ni mwandishi wa habari, mwenye damu ya habari za uchunguzi, ukifika mahali popote, lazima tuu utachunguza hata kwa kupepesa macho). Sasa ukifika Maktaba ya Chuo Kikuu, sehemu za tasnifu za Ph.D, utakuta thesis za Ph.D mamia, zenye tafiti na majawabu ya matatizo yetu kwenye ma kabrasha yakila vumbi tuu maktaba, tafiti ambazo hazifanyiwi kazi!, kwa vile lengo la tafiti hizo ni tasnifu tuu za kupatia Ph.D, watafiti hao wakiisha tunukiwa Ph.D zao, kazi yao ndio imeishia hapo!, kilichotafitiwa kinaishia kwenye ma kabrasha!.

Ukifanyika utafiti wa mamilionea na mabilione 100 Tanzania, utashangaa kukuta nusu waliishia darasa la saba, na unaweza kukuta hakuna milioneo au bilionea yoyote ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu chetu!. Hii ni kwasababu tunafundisha elimu ya nadharia na sio elimu ya kujitegemea.

Bilionea mdogo kabisa kwa sasa ni Diamond Planinum, yeye aliishia darasa la 4!. Bilionea wa ukweli number moja wa Tanzania mwenye impact kubwa kwa maisha ya wengi, naomba nisimtaje jina, ila hakusoma hata darasa moja zaidi ya elimu ya madrasa!.

Hii maana yake, Tanzania hatuwezi kupata maendeleo ya kweli, kwa kuwategemea wasomi wa elimu ya kizungu ya darasani, tutapata maendeleo ya kweli kwa kuwajengea uwezo, Watanzania wenye vipaji vya biashara kwa kuwapatia mitaji.

Mwalimu Nyerere kwa kilijua, hilo, ali introduce elimu ya kujitegemea, ili mwanafunzi akimaliza darasa la saba aweze kujitemea. Mwalimu Nyerere alipomaliza kipindi chake, aliondoka, na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea, Azimio la Arusha lenye Siasa ni Kilimo, Uhuru ni Kazi na Elimu ya Kujitegemea, vyote viliondoka nae.

Enzi za ukoloni, watu walioishi maeneo ya Oyster bay walikuwa ni wazungu. Baada ya kupata uhuru, maeneo hayo waliishi maofisa wa juu wa serikali. Enzi hizo za Mwalimu Nyerere na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, maofisa wa serikali walioishi Oster bay, baada ya kustaafu, walirejea vijijini mwao na kuendelea kuishi kwenye majumba ya madongo poromoka!.

Enzi ya Mkapa, ikaamuliwa maeneo hayo wagawane viongozi Kwa kuuziwa kwa bei za zuga, viongozi na baada ya kupeana kwa zuga ya kuuziwa , ukipita Oyster Bay ya leo na Masaki, utaona mijengo ya maana, zile nyumba zilizokuwa Oyster Bay ya zamani, nyingi zimebomolewa na kujengwa mijengo ya kisasa ya maana. Lakini ukifanywa utafiti kuangalia ni Watanzania wangapi wanaishi Oyster bay na Masaki, unaweza usiamini, idadi ya wageni ni kubwa zaidi kuliko wazawa, kwasababu wengi wa wazawa, hawana uwezo wa kuishi maeneo hayo.

Kinachofanywa na wawekezaji ni kuwanunua wazawa, kupisha na kuwekwa uwekezaji wa maana, lakini laity wazawa wamiliki wa maeneo hayo wangejengewa uwezo wa kimitaji, wawekezaji wakaingia ubia na wazawa hao, saa hizi tungejikuta Osterbay na Masaki yote inamilikiwa na mazawa na wote ni mabilionea.

Kazi ya kutengeneza mabilioneo wa Kitanzania, ndicho kitu kinachofanywa na kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, kupitia mpanga wake uitwao DODO ambao unawezesha Watanzania wenye maeneo ya pembezoni mwa barabara kuu, kujengewa uwezo wa kumiliki kituo cha mafuta na kufundishwa uendeshaji wa biashara ya vituo vya mafuta, hivyo TotalEnergy kusaidia kuzalisha mabilionea wa Kitanzania.

Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, imeendelea kumwaga Fursa kwa Watanzania, kumiliki vituo vya mafuta, kwa kuzindua kituo cha mafuta cha 14 kinachomilikiwa na Mtanzania katika eneo Mapinga, wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, na kuwaomba Watanzania wengine wenye maeneo kando kando ya Barabara kuu, kuchangamkia fursa hizo za kujengewa Vituo vya Mafuta vya TotalEnergies na kuviendesha kwa ubia.

Wito huo umetolewa leo, na Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp , (Inatamkwa Jan Franswa Shapp), wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha TotalEnergies, eneo la Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkurugenzi huyo amesema DODO ni fursa nzuri kwa Watanzania wenye maeneo ya kando ya barabara, kuingia kwenye biashara ya mafuta, TotalEnergies itawapatia kila aina ya usaidizi, ili Watanzania wengi zaidi wamiliki vituo vya mafuta.

Nae Mmiliki wa Kituo hicho, Jackson Swai, na Mkewe, Joyce Swai, waliishukuru TotalEnegy Tanzania kwa kuwafungulia fursa hiyo, na kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwapa mkopo wa ujenzi wa kituo hicho.

Pasco
Rejea za TotalEnergies.
Kwanza walianza Kampuni ya Total Yainunua Gapco na Kuwa The Biggest Oil Company in Tanzania, Kenya & Uganda.
kisha Total Tanzania yafanya makubwa, kuigeuza Tanzania kama Ulaya, yaanzia Temeke
Kisha Una Eneo Pembeni ya Barabara?, Ungependa Kuwa Millionaire au Bilionea?. Usiuze Eneo Lako!. Total Kutengeneza Ma Milionea na Ma Bilionea 100 wa DODO!.
Kisha Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station
Kisha Total yatoa fursa vituo vya COCO na CODO kuzigeuza DODO! Kuwa umiliki kituo cha mafuta cha total
Kisha Total yazidi kufanya mambo kwa ajili ya Watanzania! Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja; mteja ni mshirika
Mafuta yao Jee Kuna Ukweli Kuwa in Tanzania, Mafuta ya Vituo vya Total, " They are The Best?. If Yes, How Wakati Tunanunua Bulk?.
Jambo Total yabadili jina sasa kuitwa TotalEnergies
Uwekezaji Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!
Nishati Jadidifu Nishati Jadidifu: TotalEnergies yafanya tena kweli, yaongoza njia. Waziri Makamba aipongeza, awataka wengine wafuate
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za "Kwa Maslahi ya Taifa". "Umasikini m-mbaya kabisa ni umasikini wa fikra"-JK Nyerere.
Nimegundua kumbe Watanzania wengi tuu wana uwezo mkubwa wa kuwa mamilionea, na mabilionea!, kitu pekee walichokosa ni mitaji na mbinu za kisasa za biashara. Kampuni ya TotalEnergy ghafla imekuwa mkombozi wa Watanzania kwa kutengeneza mamilionea, watakaokuwa mabilionea!, wamemwaga fursa za kitu kinachoitwa DODO kwa nchi nzima!. Jee Watanzania tuchangamkie hizi fursa za DODO tuwe mamilioneo, au utajiri ni kwa matajiri tuu, sisi ni masikini tuendelee na umasikini wetu? au tuchangamkie Fursa?.

Kila binadamu anazaliwa mtupu, bila kuja na kitu chochote, na siku anaondoka, anaondoka mtupu kama alivyozaliwa, hata akizikwa na jeneza la thamani gani, na kushehenezwa na vito vya thamani, dhahabu, almasi na vito, vyote vitaishia tuu pale kaburini, mtu haondoki na kitu.

Hivyo wote kama tumezaliwa watupu, utajiri na umasikini ni vitu tunavyovikuta hapa duniani na tutaviacha.

Kuna aina 5 za matajiri na utajiri, na aina 5 za umasikini na masikini, umasikini mbaya kabisa ni umasikini wa fikra.
Utajiri
  1. Utajiri wa Kurithi- The Best Inheritors, umezaliwa kwenye familia tajiri, hivyo tangu unazaliwa wewe ni tajiri tayari, hata usipojishughulisha na jambo lolote, wewe utaishi vizuri kitajiri mpaka siku unakufa, wanaita umezaliwa na "silver spoon". Na ukizaliwa kwenye familia masikini wa kutupwa, usipokuwa sehemu ya makundi manne haya yanayofuatia, then for sure, unazaliwa masikini na utakufa masikini!.
  2. The Best Talents- Hawa ni wale wanaozaliwa na kipaji, akikitumia vizuri kipaji chake, kinamletea utajiri, hawa ndio kina Michael Jackson, hakusoma hata darasa moja, Diamond Platnum aliishia darasa la 4!. Kwenye kundi la the best talents kuna wasanii, wachoraji, waibaji , actors, etc. Kila mtu anazaliwa na kipaji fulani, ila wengi hawajitambui, hivyo wanakuwa masikini kwa kutotumia vipaji vyao.
  3. The Best Brains- Hili ni kundi la wale brights, briliants, genius, wenye akili nzuri, wanafanya vizuri darasani, wana score hight, hivyo ku attract top jobs, kulipwa vizuri na hivyo kuishi vizuri, ma scientist, ma profesa, wasomi ndio kundi hili. Ila pia kuna wenye best brain ya akili tuu za darasani na kuajiriwa kulipwa mshahara, lakini hawana akili za maisha, hivyo baada ya kustaafu, maisha yanawapiga sana!.
  4. The Hard Workers- Hili ni kundi la wafanyakazi kwa bidii, watu wanaojituma, wanatumia efforts zao na muscle powers zao kutoka jasho na kula kwa jasho lao, hivyo wanafanikiwa. Ukifanya kazi kwa bidii kwa kujituma, na kuwajibika, utafanikiwa, lakini ukipiga uvivu, lazi tuu utakuwa ni masikini wa kujitakia.
  5. The Fixers, hili ni kundi la watu wanaoendesha maisha yao kwa mishe mishe, they are well connected, they are not the inheritors, hawana talent yoyote!, they are not the best brains, wengine ni vilaza, they are not hard workers, but they have the best life. Kundi hili ndilo lenye wanasiasa na matapeli pia. Kwenye kundi hili kuna the lucky ones wenye bahati, wanapata connections, na channels, wanapiga pesa ndefu na wanakuwa mamilionea na na mabilionea. Hawa the lucky ones, baadhi yao wana kitu kinachoitwa "The Midas Touch" everything they touch turns to gold wengine wanasemekana wanatumia 'kizizi'!. The unlucky ones ni wasio na bahati, kila wanachofanya kinakwama, kinaishia njiani au kikifika mwisho hakizai matunda, hawa wanasemwa kuwa na damu ya kunguni, hata ukiwapa ng'ombe, akizaa, anazaa dume!.
Watanzania tuko milioni 60!. Kati ya hawa kundi kubwa zaidi ni la masikini wa kutupwa wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea. Ili tuendelee tunahitaji vitu 4, Land, labor, capital na interprenaship. Tanzania tuna land ya kutosha, tuna watu wenye nguvu, tumekosa capital na interprenaship. Umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra, umasikini wa mawazo ya kimasikini kuwa sisi ni masikini. Utafiti wangu binafsi umebaini Watanzania wengi ni watu wenye uwezo mkubwa, na wanamiliki ardhi ambayo ni mali, lakini hawana mbinu na mitaji.

Kampuni ya mafuta ya Totalenergy Tanzania, kwa kulitambua hili, kupitia mpango mkakati wake uitwao DODO, wameamua kuwajengea uwezo Watanzania kumiliki vituo vya mafuta
View attachment 2243500View attachment 2243502
Watanzania Tuna Uwezo wa Kuwa Mamilioneo na Mabilionea, Tatizo ni Mitaji na Elimu ya Biashara!.

Naendelea na zile makala zangu elimishi kwa Maslahi ya Taifa, kwa kuuliza maswali ambayo yakipatiwa majibu mujarabu, yatalibadili taifa kutoka hapa tulipo, na kupiga hatua mbele zaidi kimaendeleo.

Kunapotokea tatizo mahali, ili kulitatuta hilo tatizo, hatua ya kwanza ni kulitambua tatizo, kukijua chanzo cha tatizo, kujua ufumbuzi wa tatizo hilo, na mwisho kuchukua hatua za kulifumbua.

Tukubali, tukatae, mfumo wetu wa elimu una matatizo, tunafundishwa elimu ya nadharia kwa kutumia modali za wenzetu ambao hatufundishiwi kutatua changamoto zetu bali ni elimu ya nadharia kubwa, lakini vitendo vichache.

Mfano Tanzania tuna elimu ya Fasihi, (literature), hadi Chuo Kikuu, tuna maprofesa wa Ph.D za fasihi makumi kwa mamia kutoka vyuo vikuu vyetu, toka miaka ya 60. Mimi nimesoma fasihi sekondari hadi Chuo Kikuu, hakuna hata kitabu kimoja cha fasihi kilichoandikwa na maprofesa wetu ambacho kilitumika kufundishia, vitabu vyote ni vya waandishi kutoka nchi za wenzetu!. Vitabu vya karibu ni ni vya majirani zetu, Ngungi wa Thiongo, “The River Between” na Okot T’Bitek “Song of Lawino”, lakini tumefundishwa literature za Chinua Achebe “Things Fall Apart” na kina Henrik Ibsen “An Enemy of The People”, wote hawa ni waandishi wan je, hivi hao wasomi wa Literature wa vyuo vyetu vikuu, wako wapi?!. Jibu ni wasomi wa nadhariia tuu!.

Nikiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), nilikuwa natembelea maktabu kuu ya UDSM, ukiwa ni mwandishi wa habari, mwenye damu ya habari za uchunguzi, ukifika mahali popote, lazima tuu utachunguza hata kwa kupepesa macho. Sasa ukifika Maktaba ya Chuo Kikuu, sehemu za tasnifu za Ph.D, utakuta thesis za Ph.D mamia, zenye tafiti na majawabu ya matatizo yetu kwenye ma kabrasha yakila vumbi tuu maktaba, tafiti ambazo hazifanyiwi kazi!, kwa vile lengo la tafiti hizo ni tasnifu tuu za kupatia Ph.D, watafiti hao wakiisha tunukiwa Ph.D zao, kazi yao ndio imeishia hapo, kilichotafitiwa kinaishia kwenye ma kabrasha.

Ukifanyika utafiti wa mamilioneo na mabilione 100 Tanzania, utashangaa kukuta nusu waliishia darasa la saba, na unaweza kukuta hakuna milioneo au bilioneo yoyote ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu chetu!. Hii ni kwasababu tunafundisha elimu ya nadharia na sio elimu ya kujitegemea.

Bilionea mdogo kabisa kwa sasa ni Diamond Planinum, yeye aliishia darasa la 4!. Bilioneo wa ukweli number moja wa Tanzania mwenye impact kubwa kwa maisha ya wengi, naomba nisimtaje jina, ila hakusoma hata darasa moja zaidi ya elimu ya madrasa!.

Hii maana yake, Tanzania hatuwezi kupata maendeleo ya kweli, kwa kuwategemea wasomi wa elimu ya kizungu ya darasani, tutapata maendeleo ya kweli kwa kuwajengea uwezo, Watanzania wenye vipaji vya biashara kwa kuwapatia mitaji.

Mwalimu Nyerere kwa kilijua, hilo, ali introduce elimu ya kujitegemea, ili mwanafunzi akimaliza darasa la saba aweze kujitemea. Mwalimu Nyerere alipomaliza kipindi chake, aliondoka, na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea, Siasa ni Kilimo, Uhuru ni Kazi na Elimu ya Kujitegemea, vyote viliondoka nae.

Enzi za ukoloni, watu walioishi maeneo ya Oysterbay walikuwa ni wazungu. Baada ya kupata uhuru, maeneo hayo waliishi maofisa wa juu wa serikali. Enzi hizo za Mwalimu Nyerere na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, maofisa wa serikali walioishi Oster bay, walirejea vijijini mwao na kuendelea kuishi kwenye majumba poromoka!.

Enzi ya Mkapa, ikaamuliwa maeneo hayo wauziwe viongozi wa Serikali, na baada ya kuuziwa, ukipita Oyster Bay ya leo na Masaki, utaona mijengo ya maana, zile nyumba zilizokuwa Oyster Bay ya zamani, nyingi zimebomolewa na kujengwa mijengo ya kisasa. Lakini ukifanywa utafiti kuangalia ni Watanzania wangapi wanaishi Osterbay na Masaki, unaweza usiamini, idadi ya wageni ni kubwa zaidi kuliko wazawa, kwasababu wengi wa wazawa, hawana uwezo wa kuishi maeneo hayo.

Kinachofanywa na wawekezaji ni kuwanunua wazawa, kupisha na kuwekwa uwekezaji wa maana, lakini laity wazawa wamiliki wa maeneo hayo wangejengewa uwezo wa kimitaji, wawekezaji wakaingia ubia na wazawa hao, saa hizi tungejikuta Osterbay na Masaki yote inamilikiwa na mazawa na wote ni mabilionea.

Kazi ya kutengeneza mabilioneo wa Kitanzania, ndicho kitu kinachofanywa na kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, kupitia mpanga wake uitwao DODO ambao unawezesha Watanzania wenye maeneo ya pembezoni mwa barabara kuu, kujengewa uwezo wa kumiliki kituo cha mafuta na kufundishwa uendeshaji wa biashara ya vituo vya mafuta, hivyo TotalEnergy kusaidia kuzalisha mabilionea wa Kitanzania.

Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, imeendelea kumwaga Fursa kwa Watanzania, kumiliki vituo vya mafuta, kwa kuzindua kituo cha mafuta cha 14 kinachomilikiwa na Mtanzania katika eneo Mapinga, wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, na kuwaomba Watanzania wengine wenye maeneo kando kando ya Barabara kuu, kuchangamkia fursa hizo za kujengewa Vituo vya Mafuta vya TotalEnergies na kuviendesha kwa ubia.

Wito huo umetolewa leo, na Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp , (Inatamkwa Jan Franswa Shapp), wakati wa ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha TotalEnergies, eneo la Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkurugenzi huyo amesema DODO ni fursa nzuri kwa Watanzania wenye maeneo ya kando ya barabara, kuingia kwenye biashara ya mafuta, TotalEnergies itawapatia kila aina ya usaidizi, ili Watanzania wengi zaidi wamiliki vituo vya mafuta.

Nae Mmiliki wa Kituo hicho, Jackson Swai, na Mkewe, Joyce Swai, waliishukuru TotalEnegy Tanzania kwa kuwafungulia fursa hiyo, na kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwapa mkopo wa ujenzi wa kituo hicho.

Pasco
P pale kawe situnayo ardhi?tuamue tutunataka kumiliki DODO au CODO
 
Kwa nini Watanzania mko obsessed sana na namba ya idadi ya watu ? Ni nani na wapi imesemwa kwamba tuko milioni 60? Hiyo namba umeipata wapi ? Sensa ya mwisho kipindi cha Kikwete tulikuwa ~ milioni 40, sasa tumeongezeka kwa milioni 20 ndani ya miaka michache tu ?

Ni nani aliwadanganya kuwa wengi ni sifa ? Watu wengi ni mzigo na siyo jambo la kujivunia hata kidogo kwenye nchi ambayo kila mtu anasubiri Serikali itangaze ajira!
 
Ni nani aliwadanganya kuwa wengi ni sifa ?
Imani za wazee wa enzi ya mwaka 47 kuwa Kila moto anakuja na bahati yake na kuwa ni ufahari🤔
 
lipia tangazo lako, hiyo total energy anataka kuongeza market share yake tu tanzania. leta ushaidi kama Total energy anajengea watu shell bure. bado gharama za ku import mafuta, kila biashara ni fursa kama kuna mtaji wa kutosha. elimisha watu namna ya kutafuta mtaji na uchaguzi wa fursa, sio kila fursa ni saizi yako.
 
Kaka Paskali...
Miaka ya nyuma tulikuwa tukisikia 'mfanyabiashara wa...' au 'mfanyabiashara maarufu'
Maneno hayo yalinipeleka kufanya biashara kwa nguvu, bidhaa yangu ipendwe, iuzike n.k nikijua kwa hayo hela itakua matokeo ya juhudi za kufanya biashara kwa weledi na nguvu zangu.

Leo hii watu wanataka kuwa 'mabilionea' kwanza kabla ya kuwa Wafanyabiashara.

...
na kutaka huko kunapeleka kuwa na wizi, ujambazi, ufisadi na mengine hasi yanayopeleka mtu kufikiria njia za kipanya panya kuupata 'ubilionea' badala ya kufikiria kufanya biashara au kuajiriwa ndio uwe bilionea.

Natamani kuwe na gag order ya matumizi ya Bilionea kama kiashiri cha mfanyabiashara maarufu.

Hatahivyo, uwezo tunao, nguvu tunayo, maliasili tunazo, rasilimali bwelele...na sasa miundo mbinu unateleza tu.
 
Kwa nini Watanzania mko obsessed sana na namba ya idadi ya watu ? Ni nani na wapi imesemwa kwamba tuko milioni 60? Hiyo namba umeipata wapi ? Sensa ya mwisho kipindi cha Kikwete tulikuwa ~ milioni 40, sasa tumeongezeka kwa milioni 20 ndani ya miaka michache tu ?

Ni nani aliwadanganya kuwa wengi ni sifa ? Watu wengi ni mzigo na siyo jambo la kujivunia hata kidogo kwenye nchi ambayo kila mtu anasubiri Serikali itangaze ajira!
Rate of population growth is directly proportional to the size of population ,solving first order differential equation ,population increases exponentially with time ie p= constant* e^time.
 
Rate of population growth is directly proportional to the size of population ,solving first order differential equation ,population increases exponentially with time ie p= constant* e^time.

Kwa hiyo kutoka 2012-2022 Tanzania imeongeza watu milioni 20 ? Yaani ndani ya miaka 10 tumeongeza watu karibia milioni 20 ?
 
Back
Top Bottom