Kumbe wanaume wanaolizwa na mapenzi bado wapo!

Kumbe wanaume wanaolizwa na mapenzi bado wapo!

Jana jioni nilikuwa mahali having dinner with a friend, sasa kuna vijana kama wa4 walikuwa meza ya jirani wanakula na kunywa, baada ya muda jamaa mmoja kati ya wale wa4 akaanza kulia hadi ikabidi mwenzao mmoja aondoke nae akampakia kwenye gari haoo wakaondoka.

Sasa ndio tukawa interested kujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mpaka mtoto wa kiume atoe chozi namna ile, ikabidi tujongee tupate kuuliza maana tulihisi ni msiba.

Ndio tukapewa story;
Jamaa alikuwa na mchumba wake ambae wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na miezi4 na walitaraji mwezi wa6 mwaka huu wafunge ndoa. Na katika mahusiano yao walikubaliana hakuna kugegedana hadi watakapofunga ndoa.

Awali walikubaliana kuanza mipango ya kutambulishana mwezi wa11, na kijana alimpeleka binti kwao, ikawa imebaki kijana kwenda kwa akina binti na walikubaliana waende mwezi wa12, ila baadae binti akahairisha na kumueleza kijana kuwa isingekuwa muda mzuri kwani kwao kuna matatizo ya kifamilia.

Kumbe binti kule alikokua alianzisha mahusiano na kijana mwingine na mapenzi yalikuwa motomoto kabisa na walikuwa wakila tunda kama kawaida, baadae binti akanasa ujauzito na ndio kisa cha kumwambia kijana asubiri kwanza kwenda kujitambulisha.

Baada ya kunasa ujauzito wakakubaliana wahalalishe mahusiano yao kwa kutambulishana na waanze michakato ya kufunga ndoa na mwanaume alompa ujauzito. Mipango ilianza vyema kabisa na wakapanga kufunga ndoa mwezi wa4 mwaka huu.

Binti alishindwa namna ya kumueleza kijana ikabidi aanze visa tu, kwanza akamwambia kijana ameamua kurudi kuishi nyumbani kwao kwa muda maana mambo hayaendi vizuri hivyo hawakuonana tangu disemba, akimuuliza kuhusu mipango ya kutambulishwa ukweni anamjibu asubiri.

Sasa kati ya hao friends wake aliokuwa nao jana alipata habari bibie anaolewa na mipango iko hatua za mwisho kabisa. Jana ndio katika maongezi ndio anamwambia rafiki yake kuwa "yaani wewe na J kwa jinsi mlivyokuwa mnapendana nilijua mngeoana kabisa, kwani nini kilitokea mkaachana?" Jamaa akamjibu, "J bado tunapendana na hatujaachana na mwaka huu lazima tufunge ndoa Mungu akijaalia".

Rafiki mtu akahisi jamaa anatania.
To cut the story short, jamaa akaelezwa kila kitu na ili kuthibitisha akampigia rafiki wa J simu na akamthibitishia kuwa J anaolewa, ndio jamaa kupatwa na mshtuko na kuanza kulia.
hahahaha haya mambo ya kusubiria tunda mpaka ndoa mm huo moyo sinaga kabsa
kuna manz tumepigana chn kisa hzo story heri nibaki single sasa kuna umuhim gan wa kuwa kwenye hio aina ya mahusiano
 
Ndio ile wanasema mapenzi hayajaribiki, inaelekea binti alitest tu apate tulizo kwakuwa jamaa yupo mbali basi ndio akanogewa mazima.[emoji85] [emoji85] [emoji85]
Kwaio mtu unaweza kumpenda mtu na ukawa na malengo.nae kumbe yeye anakutest tu kwamba anakua na wewe for a mission, lengo lake likitimia ana sign off kwa stail ya aina yake
 
Kuna watu tunayo ya moyoni sema bhac2 anaelia kwa ajili y mapenzi me simshangai coz kaz y moyo nikusukma damu ukipenda Ni kiherehere chako[emoji12] [emoji13] [emoji12] [emoji12]
Mmmh!!
 
hahahaha haya mambo ya kusubiria tunda mpaka ndoa mm huo moyo sinaga kabsa
kuna manz tumepigana chn kisa hzo story heri nibaki single sasa kuna umuhim gan wa kuwa kwenye hio aina ya mahusiano
Umuhimu upo mkubwa sanaaaa!! Basi tu haujautambua.
 
Kwaio mtu unaweza kumpenda mtu na ukawa na malengo.nae kumbe yeye anakutest tu kwamba anakua na wewe for a mission, lengo lake likitimia ana sign off kwa stail ya aina yake
Ndio hivyo bwana, unaweza shangaa mtu anapanga short term plan zake kwenye long term plan zako, ukijastuka kumekucha kweupeeee!!
 
Wewe wasema tu kuna watu hadi wanajinyonga kisa kuachwa
Kuachwa haijawa mwisho wa dunia, kuna maisha yanaendelea, kutoupa ubongo nafasi ya kufikiri kwa mapana ndipo watu wanapojinyonga, ni ulimbukeni wa hali ya juu, niliacha wazazi wangu nikajitegemea, niliachana na kila niliyemzoea tokea msingi mpaka chuo, sembuse MTU tu tumekutana ukubwani unaniambia nakuacha unalia, wanaume wengine hawajiamini aisee.
 
Umuhimu upo mkubwa sanaaaa!! Basi tu haujautambua.
tunaya kataa sio kwa sababu hayana umuhim upo nakubaliana na ww
lkn sio kwa akili za wasichana wa k-tz weng ni waongo mwisho wa siku utajutia na kujikuta umefanywa mjinga
hapo utakuta umesolve shda ndogo ndogo kibao
 
tunaya kataa sio kwa sababu hayana umuhim upo nakubaliana na ww
lkn sio kwa akili za wasichana wa k-tz weng ni waongo mwisho wa siku utajutia na kujikuta umefanywa mjinga
hapo utakuta umesolve shda ndogo ndogo kibao
Kutatua shida muhimu sana bwana, tenda wema nenda zako[emoji85] [emoji85]
 
Kweli anaongea tu,siku yakimkuta kama hatajinyonga basi atakuaja kuanzisha mada kali humu.
Tena atatuita majina yoote mabaya anayoyafikiria kama kuna mmoja niliona anatuita 'wadudu'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom