Kumbe Uturuki hamna Christmas!..

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
523
Reaction score
916
nimesikitika kuona baadhi ya nchi wanaendekeza udini kupita maelezo. nipo uturuki kwa mda kama mwezi kikazi. nimeshangaa kuona leo dunia inaadhimisha sikuku ya kuzaliwa yesu lakini kwa hii nchi tofauti kidogo. watu wameenda kazini, vyuoni, shule na shughuli zote za maendeleo zinaendelea kama kawaida. nimemuuliza dogo mmoja ananiambia ndo ilivo kwa kawaida hakuna mapumziko ya chrismas wala pasaka. mapumziko ni siku za eid tu. nimesikitika kwa kweli nimekumbuka tanzania yangu. sikutegemea kama udini upo juu kiasi hiki kwa nchi kama uturuki!!!
 

Uturuki ni taifa la kiislamu,chepuka ujerumani ukale sikukuu yako
 

Karibu moshi mkuu huku full shangwe
 
Kwani siwanamwamini issa bin mariam, sasa kwanini wasisherekee kuzaliwa kwake, hebu wakumbushe quran
 


Siku nyingine kabla ya kuandika mada au kulaumu kitu jaribu kujitafakari kwanza,

Hivi unafikiri kila nchi Duniani wanafuata utaratibu wa Sikukuu zote kama ilivyo Bongo?

Nafikiri nia yako kubwa ya kuanzisha hii thread ilikuwa ni kujitangaza kuwa na wewe upo Turkey kikazi.
 
Niliwahi kuwa Cairo Misri siku ya Christmass, hakukuwa na shamra shamra yeyote. Nilifanya ibada yangu kwenye chumba changu cha hoteli, nikawapigia simu ndugu na jamaa kuwatakia kheri,baada ya hapo nikatoka kwenda kula. Moyoni nilijua nimesherehekea Christmas
 
kila nchi na utaratibu wake! Wewe unajua ukristo na uislamu tu! Umewahi sikia wachina na wahindi kulalamika kuhusu sikukuu zao kutokwepo kwenye kalenda ya nchi yetu?
 

merry christmas
 

heri yako ulisherehekea ukiwa hotelini, huku kama ukitaka kusherehekea mpaka jioni saa kumi na moja after work
 
Waache waendelee na misimamo yao ndio maana laana za vita haziwaachi kila kukicha
 

Unashangaa nini Mbona western countries hawa sherehekei sikujui za Eid?
 
Hata somalia na Tajikstan jana wamepiga marufuku sherehe za xmas na mwakampya.

Kila nchi na mipango yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…