Sura ya Saba na ya mwisho wa kisa hiki cha kusisimua inakuja ndani sasa hivi.... zingatieni onyo.. nililotoa jana. Msichape mkaweka karibu na watoto.
Sura ya Saba na ya mwisho wa kisa hiki cha kusisimua inakuja ndani sasa hivi.... zingatieni onyo.. nililotoa jana. Msichape mkaweka karibu na watoto.
Sasa MMM nimwangukie character wa kwenye hadith jamani kivuli hicho ndugu yangu na enzi zile za kumfia Willy Gamba ilikuwa zamani bwana. But of course ninaheshimu utashi wako mpenzi you are not reachable ..... so najiweka pembeni nile kwa macho tu.... ntafanyaje sasa nami kukuteka siwezi.... lol.
Mwanakijiji mie na MJ1 tuko same boat ...hiyo sehemu ya saba naona PM zitajaa kwenye mail box yako ..
Aksante MMM kwa burudani. Nimefurahi kuwa at the end dada yangu Clementina akili yake imerudi haraka. Jamani ni kweli kabisa sometimes wanandoa tunajidanganya kutafuta faraja nje ya mahusiano yetu ya halali lakini huwa si suluhisho hata kidogo. Mambo yote yako kwa wenzi wetu wa halali.
Ila MMM ungemfunua kidooooogo Freddy kwa maswali alokuwa akijiuliza Clementina ningefurahi yaani tujue kama Freddy ni mtoto wa mjini au lah maana umetuacha na kiu shemeji.
Aksante shemeji sasaaa.............duh sijui ntaambiwa nina kimuhemuhe? ah naliza tu banaof course lazima kuna part 2...
Aksante shemeji sasaaa.............duh sijui ntaambiwa nina kimuhemuhe? ah naliza tu bana
Sasa MMM baba lini tutegemee Part 2 ya hii Kumbatio la Mwenye Makosa?
Oh ndio kwenye ile ilani ulotoa kumbe?? Sasa hata kunimegea lini nitarajie ili niharakishe uchangiaji jamani??mbona nimedokeza...? watakaopata "Uso kwa Uso" watashangaa suprise iliyomo...LOL
mwanakijiji mie nataka nije na ukosoaji wa kiuandishi ................ninaruhusiwa?
1. seriously mwanakijiji unatumia brackets kwenye story book...............seriously!
mwanakijiji kwa vile umetoa ruhusa mie nitakuja na ukosoaji wa kiuandishi
1. Matumizi ya Mabano (brackets)
Sijawahi kuona kitabu cha hadithi kuwa na bracket ndani yake. It doesnt sit well when u read. Kama maelezo hayo ya ndani ya Bracket ni muhimu basi ni bora kama ungeyatafutia njia ya kuyaandika nje ya bracket.
2. Kuelezea kwa undani vitu ambavyo havina athari kwenye plot moja kwa moja
Umeelezea vizuri sana na kwa kina kuhusu sherehe za muungano (zaidi ya nusu ya kurasa moja) ambayo haikuwa na haja hata kidogo kwa kuwa unamtoa msomaji wako kwenye maudhui yenyewe unampeleka kwenye kitu ambacho hakina athari kwenye hadithi yenyewe.
3. Kufananisha kitu kimoja na chengine mno kwenye hadithi
sijui ndo inaitwaje kwa kiswahili ........lakini mfano umesema something like 'akitizama paja langu lililonona kama punda milia wa serengeti' au 'kumsimamia mbele bila nguo sawa na panya kusimama mbele ya paka na kumshikia kiuono' na kadhalika na kadhalika.
Unapokuwa na hizi nyingi kwanza moja unampunguzia msomaji wako uhuru wa kufikiri
pili nafikiri pia zinamtoa msomaji kutoka hadithi yenyewe...............maana do u want us to think of the ugomvi baina ya hawa wawili au about panya kashika kiuono!
4: italics
Kwa kweli i didnt get the way you used italics. mwishowe nilihisi labda ni kwa ajili ya kushadidia jambo......but sometimes it felt like it wasnt the case. Sikuelewa matumizi yako ya italics katika hadithi hii..............naomba ufafanuzi