Serikali inawekeza sana kwenye miundombinu na sio miradi ya kuondoa umasikini

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,505
Miradi ya miundo mbinu kama Barabara, reli, Madaraja ni tofauti na miradi ya kuondoa au kupunguza umasikini.Nchi zilio fanikiwa kuondoa umasikini wa viapto walikuja na miradi mwili na ikaenda sambamba, miradi ya miundo mbinu pamoja na miradi ya kuondoka umasikini wa vipato.

Sasa CCM kutafuta sifa wanawekeza sana kwenye miundombinu huku raia wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa, ni kawaida kukuta maeneo yana umeme, maji, Barabara za lami ila kuna umasikini wa kutisha.

Ukifuatilia China ana project za miundo mbinu na pia project za kuondoa umasikini wa Vipato kwa raia wake na amefanikiwa sana. unakuta wana project labda za ufugaji samaki, ufugaji kuku, Bata, uzalishaji wa uyoga na kadhalika.

Madaraja na Barabara hayawezi ondoa kamwe umasikini wa vipato, watu wanahitaji kuwezeshwa kwenye project zitakazo weza kuondoa umasikini wa vipato.

CCM hawataki kuona watu wanaondokana na umasikini wa vipato kwa sababu itakuwa mwisho wa wao kuhonga kanga. ndio maana wanakomaa na miradi ya miundo mbinu pekee.
 
Una nukta nzuri, usikilizwe.

Lakini tambua kwamba Tanzania inaweza kuwekeza kwa pamoja kwenye miradi mikubwa ya jumla na miradi midogo midogo iwagusayo wananchi moja kwa moja.

Tatizo wala siyo kipaumbele. Hapana. Hata hiyo miradi tunayodhani ni mikubwa, bado ni michache mno.

Nchi yetu ina shida ya ombwe la uwajibikaji na uadilifu.

Ubadhirifu ni mkubwa sana. Rushwa imetawala kila kona.

Wizi wa siri na wa wazi wa mali za umma umevuka mipaka.

Fedha nyingi za serikali zinaishia kinyemela mifukoni mwa watu binafsi.

Nchi yetu ikiweza kujidhibiti kwenye eneo hilo, Tanzania ina uwezo wa kufadhili miradi ya uchumi na maendeleo hata kwenye nchi zingine.

Naweza kusema kwamba sie kama taifa tuna utajiri mkubwa wa rasimali, ila tumeelemewa ufukara wa akili.

Mungu atunusuru kwenye kadhia hii ya kujitakia, isikitishayo!
 
Back
Top Bottom